Je, ubatizo kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu ni sahihi?

Je, ubatizo kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu ni sahihi?

Maana sijaona kifungu chochote ulochoweka kwa hoja yako au unataka tujadili maneno ya mtu?
 
Matendo ya mitume 2:38,8:1610:47 - 48,19:5
Matendo ya Mitume 2:38
[38]Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


Hoja ni nini sasa, yaani wanaosema Baba, mwana na roho mtakatifu wanakosea wapi? leta hoja
 
Matendo ya mitume 2:38,8:1610:47 - 48,19:5
Hili ndilo tatizo lenu,Huwa mnakurupuka na kafungu kamoja ili kuhalalisha hoja zenu pasipo kuweka bayana muktadha wa Sura nzima,nenda kasome Sura nzima hiyo ya 2 ya kitabu Cha Matendo utafahanu muktadha wa alichokuwa akiwaambia hao watu!

Dhambi inaondolewa na Yesu peke yake ndiyo maana akawaambia "Tubuni mkabatizwe na katika jina la Yesu mtapata ondoleo la dhambi!"

Hicho ndicho alichomaanisha Petro!



JESUS IS COMING AGAIN

Get prepared!
 
Back
Top Bottom