Je ubongo una back up memory? Je ni ule mlango wa nane wa fahamu?

Je ubongo una back up memory? Je ni ule mlango wa nane wa fahamu?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Soma hii kwanza kabla sijaendelea ili upate msingi wa kile nitakachoandika
Mawasiliano ya kiroho katika milango nane ya fahamu - JamiiForums

Nitatoa mifano michache lakini kwanza pata picha ya kile ninachokiongea

Mwili wa binadamu unaendeshwa na control box iitwayo ubongo... Hapa ndio mawasiliano yote huanza.. Yaani michakato yote ya mwili msingi wake ni hapa

Mojawapo ya kazi za ubongo ni kutunza kumbukumbu.. Kumbukumbu hizi hutunzwa kulingana na umuhimu wake, ukali na uzito. Na milango fahamu ya sita mpaka ya nane ndio huhusika na utunzaji huo.

Uzito na umuhimu wa kumbukumbu husika ndio huamua tukio gani litunzwe kwenye mlango upi wa fahamu na kwa muda gani. Ndio maana kuna matukio ya miaka mingi iliyo pita unaweza usiyasahau lakini ukasahau la last week

Kichwa ni jumba muhimu sana kwenye uhifadhi wa ubongo. Ndio maana hata kwenye boda boda ni muhimu kuvaa helmet. Kichwa kikipata pancha ni sawa na kudisturb mlango wa fahamu. Mlango huu ukishapata shida watu hupoteza kumbukumbu moja kwa moja ama kwa muda

Watu wanaopata ajali na kuumia sana kichwa lakini wakapona kifo huwa na hili tatizo kubwa la kupoteza kumbukumbu. Lakini kiwango cha kupoteza kumbukumbu hutegemeana na athari zilizopatikana kwenye ubongo

Cha kushangaza ni kwamba ubongo una backup ya selihai zenye kuhifadhi matukio yote ya nyuma kama ikitokea tatizo kubwa kwenye ubongo linalosababisha kumbukumbu zote kufutika

Watu wanaopata ajali mbaya na kuzirai kwa muda mrefu sana. Bongo zao hu-corrupt na kufuta ama kusimamisha kumbukumbu zote. Na wanapokuja kuzinduka ni kama vile ubongo unakuwa umefanyiwa format na kuanza upya kabisa
Baadhi huanza hata kujifunza kuongea upya lakini kadiri mifumo ya mwili inavyotengemaa na ndio kumbukumbu zinavyorudi

Baadhi ambao huzirai ndani ya miezi miwili wakizinduka kumbukumbu ya kwanza kurudi ile ile ya tukio muhimu la mwisho kabla ya kuzima.. Hili inaweza kuwa tukio la nusu saa kabla ama dakika chache. Wale wakuzima muda mrefu kuanzia miezi mitatu na kuendelea hawa kadiri mifumo ya mawasiliano inavyotengemaa ndio kumbukumbu huwarudi lakini cha kushangaza sana ni kwamba kumbukumbu zote muhimu hujichuja na kuwa restored huku ambazo sio muhimu zikiwa sio za kukumbukwa sana

Kwa mantiki hii ni wazi kabisa ndani ya ubongo kuna mlango wa fahamu unaodili na kuhifadhi matukio yote ya nyuma.. Na mlango huu ni mlango wa fahamu wa nane unaofanya kazi kama backup...

Nitatoa mifano

====
Mifano iliyotolewa

Mfano wa kwanza ajali ya mtu aliezimia kwa siku 45
Mfano wa pili mtu aliyezimia Miezi 6
Jr[emoji769]
 
Ilikuwa mwaka 2014 siku ya Jumamosi. Siku hiyo kuna jamaa yangu tulikuwa tunapiga wote vyombo tangu asubuhi. Tulianzia mabibo External baadae tukahamia River side bar. Halafu mimi nikaenda Mabibo makutano na yeye akaenda Mlimani City

Kwenye saa kumi na moja akanifuata Mabibo alikuwa na pikipiki lakini mara akaitwa external kuchukua pesa fulani. Nikamsihi aendeshe taratibu akajisifu kuwa yeye ni dereva mzuri hasa anapopiga vyombo. Akaacha bia zake mezani akaondoka

Kwenye saa kumi na mbili nikapigiwa simu na mtu nisiyemjua akinipigia simu akiniuliza kama namfahamu mwenye hiyo number kwakuwa kapata ajali ( kumbe ni yule rafiki yangu lakini number yake ya tigo nilikuwa sina.... Mimi nikajibu hapana na kuendelea na zangu

Kwa mawazo yangu nikajua huko aliko jamaa lazima na hawezi kurudi tena. Nilikuja kujua Jumanne kama kapata ajali mbaya Mabibo mwisho siku ya Jumamosi.. Nikakumbuka kila kitu. Jamaa alikaa ICU siku 45 bila fahamu na siku aliyozinduka cha kwanza kuuliza ilikuwa Mshana yuko wapi

Jr[emoji769]
 
Mfano wa pili.

Jamaa yetu mtu mzima alipata ajali Dodoma akitoka kuapishwa baada kupandishwa cheo. Ilikuwa before last year. Akakaa ICU miezi sita bila kuzinduka. Baada ya kuzinduka na kupata nafuu na hatimaye kupona kabisa sasa hivi ana kumbukumbu ya hali ya juu mno. Anakuelezea mambo ya uhuru mwaka 1961 kwa usahihi mno

Jr[emoji769]
 
Mfano wa pili... Jamaa yetu mtu mzima alipata ajali Dodoma akitoka kuapishwa baada kupandishwa cheo... Ilikuwa before last year ... Akakaa ICU miezi sita bila kuzinduka.. Baada ya kuzinduka na kupata nafuu na hatimaye kupona kabisa sasa hivi ana kumbukumbu ya hali ya juu mno.. Anakuelezea mambo ya uhuru mwaka 1961 kwa usahihi mno

Jr[emoji769]
Hii nakubaliana na wewe, mimi kuna jamaa yangu alipata dharura ya maradhi fulani ya ghafla, na akahitajika kufanyiwa oparesheni haraka sana, mimi nilimsindikiza mpaka Muhimbili bila mkewe wala nduguze kujua wala kuwepo alipodungwa dawa za usingizi alikuwa anaiita kila mara na kuomba nisimwache peke yake, baada ya kulala fo fo fo, mimi nikaondoka zangu kuwafuata familia yake, wakaenda

Siku ya pili alipozinduka vizuri jina la kwanza kuanza kuita kwa sauti ni langu! na mimi sikuwepo na mara ndio nikafika Muhimbili, hivyo inaonyesha kuna huo mlango wa kumbukumbu ulifunguka palapale ulipojifungia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jambo lingine upande wa kumbukumbu ya mwanadamu linawaumiza sana kichwa wanasayansi kutokana na visa mbalimbali vya kitabibu.

Kuna kisa cha mtoto wa miaka 7 alibadilishiwa moyo na kuwekewa moyo wa mtoto mwingine wa miaka tisa ambae ulitolewa katika dakika zake za mwisho baada ya kupata ajali.

Huyo mtoto aliewekewa moyo wa mtu mwingine baada ya kuruhusiwa kutoka hospital, alianza kuonyesha mabadiliko kadhaa ya kitabia ambayo hapo awali hakua nayo,

Alianza kua na uoga wa hali ya juu kila alipokua akiona swimming pool au bahari, wakati hapo awali kabla ya matibabu yake ya kubadilishiwa moyo alikua anapenda sana kuogelea, hili liliwashtua sana wazazi wake na kila walipokua wakienda clinic walimuelezea docta tofauti ya mienendo na mabadiko yake kabla na baada kubadilishiwa moyo.

Wataalamu baada ya kufatilia sana upande wa yule mtoto wa miaka tisa aliyefariki na moyo wake kuwekewa huyu mwingine wakagundua vitu tofauti tofauti vyenye kuleta wasiwasi kua huenda moyo pia una sehemu inayotunza vitu/kumbukumbu ya mambo yaliyopita.

Walikuja kugundua Yule mtoto aliefariki kuna wakati alizama kwenye swimming pool na ikapelekea kua ni mwenye kuogopa sana maji.
 
Kuna jambo lingine upande wa kumbukumbu ya mwanaadamu linawaumiza sana kichwa wanasayansi kutokana na visa mbalimbali vya kitabibu.
Kuna kisa cha mtoto wa miaka 7 alibadilishiwa moyo na kuwekewa moyo wa mtoto mwingine wa miaka tisa ambae ulitolewa katika dakika zake za mwisho baada ya kupata ajali.
Huyo mtoto aliewekewa moyo wa mtu mwingine baada ya kuruhusiwa kutoka hospital, alianza kuonyesha mabadiliko kadhaa ya kitabia ambayo hapo awali hakua nayo,
Alianza kua na uoga wa hali ya juu kila alipokua akiona swimming pool au bahari, wakati hapo awali kabla ya matibabu yake ya kubadilishiwa moyo alikua anapenda sana kuogelea, hili liliwashtua sana wazazi wake na kila walipokua wakienda clinic walimuelezea docta tofauti ya mienendo mabadiko yake ya kabla na baada kubadilishiwa moyo.
Wataalamu baada ya kufatilia sana upande wa yule mtoto wa miaka tisa aliyefariki na moyo wake kuwekewa huyu mwingine wakagundua vitu tofauti tofauti vyenye kuleta wasiwasi kua huenda moyo pia una sehemu inayotunza vitu/kumbukumbu ya mambo yaliyopita.
Walikuja kugundua Yule mtoto aliefariki kuna wakati alizama kwenye swimming pool na ikapelekea kua ni mwenye kuogopa sana maji.
Naweza nisiwe sahihi sana lakini ni kama ulinganifu wa RAM na ROM je kuna mahusiano gani ya ki mawasiliano kati ya moyo na ubongo?( roho na ufahamu) na ni kipi kati ya hivi viwili chenye nguvu ya uhawalisho na kichocheo chanya ama hasi dhidi ya kingine?

Jr[emoji769]
 
Aiseh hii inasisimua... Moyo na ubongo ni organs za aina yake


Sent from my iPhone using JamiiForums
Hapo awali tuliaminishwa kazi pekee ya moyo ni kusukuma damu, ila baada ya kugundulika matibabu ya kupandikiza na kubadilisha moyo toka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine yamegundulika mambo mengi sana kuhusu moyo.

Kipo kisa kingine cha kiongozi wa dini aliebadilishiwa moyo na kuwekewa wa mtu mwingine, ila huyu hakuishi muda mrefu aliamua kujiua yeye mwenyewe baada kujikuta yupo na mabadiliko makubwa kitabia na kumbukumbuku ambazo zilikua zinamkosesha raha na kumtia simanzi na sononeko kubwa ndani ya nafsi yake.
 
Ningeweza kutoa mchango mkubwa sana

Maana ndo fani yangu

Ila ngoja kwanza , mshana bado tuna ugomvi mzee. ??

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kwanini unatumia nguvu nyingi kutaka kuonesha kuna ugomvi kati yetu wakati sikufahamu zaidi ya ID yako ambayo hata hivyo sio halisi?

Hii ni forum ya hoja na malumbano kwa wenye kufikiri zaidi ya kufikiri (great thinkers) ni mahali ambapo wanakutana watu wa kada zote, ufahamu na maono tofauti kila mmoja wetu kwa kipawa chake.. Hatuwezi kufanana

Ni kwa muktadha huo siwezi kujipa stress ninapokutana na mtu ambaye mitazamo yake ni kimo cha mbilikimo.. Nunachoweza kufanya ni kumpuuza ili nisianze malumbano yasiyo na tija na kuanza kuoneshana misuli ya ujuaji

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom