Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Nimetafakari sana na kujiuliza juu ya hili swali. Maana hata kabla ya kurudi kwa mfumo wa vyama vingi hapa Tanzania na nchi nyingine nyingi za Africa, sababu kubwa iliyoletwa na taasisi kama World Bank na nchi nyingi za wahisani ilikuwa ni kudhibiti ubadhirifu na ufisadi.
Wahisani na World Bank walisema kuwa nchi nyingi za kiafrika zilikuwa na mfumo wa Chama kimoja na kwa sababu hii watawala walikuwa wakifisadi mali za umma na hakuna aliyekuwa akihoji. Ndio maana walazimisha nchi za Africa ziwe na mfumo wa vyama vingi ili kama kuna ubadhirifu au ufisasi, vyama vya upinzani viweze kuibua huo ufisadi.
Hapa Tanzania tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi wapinzani wamekuwa wakipata nguvu pale tu Chama tawala kinapokumbwa na kashfa za kifisadi. Mfano NCCR Mageuzi mwaka 1995 Lyatonga Mrema kila alipokuwa akisimama jukwaani alikuwa lazima agusie kashfa ya mtanzania mwenye asili ya Asia aliyekuwa anaitwa Chavda, ambaye alijipatia mashamba ya mkonge kwa njia ya kifisadi. Na hili lilimpa nguvu sana kisiasa.
Chadema nao wakaja na list of shame ambayo Dk. Slaa alipewa na raia wema. Na hii nayo iliwapa nguvu sana Chadema. Sasa swali linakuja bila kuwepo ufisadi na ubadhirifu ndio kusema upinzani hauna hoja za kuhoji?
Maana tokea Magufuli aingie madarakani mwaka 2015 wapinzani wamekuwa kama hawana hoja kabisa. Hii ni kwa sababu ubadhirifu, ufisadi, rushwa na uzembe kazini umezibitiwa. Serikali ya CCM inatekeleza ilani yake kama ilivyoahidi. Mfano kujenga mradi mkubwa kama JNHPP kwa pesa za ndani sio jambo dogo.
Je, wapinzani hasa Chadema, kama KUB ,hawana hoja nyingine za kuhoji zaidi ya ufisadi na ubadhilifu? Maana walijaribu ishu ya Tril 1.5 lakini ikabuma.