Je uhusishwaji wa ugaidi na uislam ni mpango wa watu fulani au ni ukweli usio na shaka??

  • Jesus ni Yesu?
Jesus maana yake nini? Ndio huyu huyu Yesu mnayemnadi na kule aitwe Jesus?
Tuliza kichwa halafu changanua majina yake yote katika mkorogo uliojipika wa Kilatini, Kigiriki, Kiebrania, halafu utuambie la Joshua aliliachilia wapi?

  • Aya hii ni wazi sana. Mtume Muhammad s.a.w. ndiye aliyeileta dini ya Kiislamu kwa watu waliokuwa hawaijui. Ni dhahiri yeye mwenyewe ni mtu wa kwanza miongoni mwao aliyeshika Uislamu. Dini ya Kiislamu inakiri ya kuwa Manabii wote waliotangulia pamoja na wafuasi wao walikuwa "Muslimiin" yaani watu waliojitupa kwa Mwenyezi Mungu.
Nabii Musa pia alisema maneno ya namna hiyo, "Na mimi ni wa kwanza wa waaminio" (sura
7:144). Je, itakuwa ni uaminifu kufumba macho na kufasiri maneno hayo kuwa Musa ndiye alikuwa Mwisraeli wa kwanza kuamini, na kabla yake hakukuwa mtoto mwingine wa Yakubu aliyeamini? Maneno haya hayaonyeshi ila ya kwamba, katika umati wake Musa mwenyewe ndiye alikuwa wa kwanza kuamini.
Wachawi wa Firauni pia, waliposhindwa na Musa, walisema: "Tunatumai ya kwamba Mola wetu Atatusamehe makosa yetu, maana sisi tumekuwa wa kwanza wa waaminio" (sura 16:52).

  • YESU ALITUMWA KWA WANA WA ISRAELI TU

Yeye hakupewa ujumbe wa utume kwa ajili ya watu wote wa kabila zote. Bali yeye alikuwa

Mtume kwa ajili ya wana wa Israeli tu. Mwenyewe alijua mipaka ya utume wake. Kwahiyo alisema: 1. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:24).

2. Wakati mwanamke mmoja asiyekuwa mwana wa Israeli alipokuja kwa Yesu Kristo kuomba baraka zake, Yesu akakataa na zaidi ya kukataa aliwatusi wasiokuwa Waisraeli. “Akasema si vyema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia m’mbwa.” (Mathayo 15:26, Marko 7:27).

3. Hao thenashara (kumi na mbili) Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, katika njia ya mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 10:5-6).

4. Baadhi ya Wakristo wanadhani kwamba wakati Waisraeli wote wamefikishiwa ujumbe, kisha makabila mengine pia yahubiriwe. Lakini dhana hii si sahihi bali ni kinyume cha mafundisho ya Bwana Yesu. Yeye amesema kwamba: “Lakini watakapo wafukuza katika

mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawambia, hamtaimaliza miji ya Israeli hata ajapo mwana wa Adamu. (Mathayo 10:23).

5. Bwana Petro mwanafunzi wa Yesu Kristo aliwahubiri wasiokuwa Waisraeli. Wanafunzi wengine, baada ya kupata habari hii walimpinga Bwana Petro kwa kosa lake. Biblia inasema kwamba: “Basi mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa mataifa nao wamelipokea neno la Mungu. Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye, wakisema, uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. “ (Matendo 11:1-3).

6. Aya za Biblia zifuatazo zinaeleza kwamba Bwana Yesu alikuwa mfalme na mtawala wa Mayahudi. (Mathayo 2:6, 27:29, 27:42, Yohana 1:49.

7. Bwana Paulo ambaye ni mpinzani na mhalifu (anti Christ) wa Bwana Yesu, baada ya kuchukia alianza mahubiri nje ya Wasiraeli. Biblia inasema kwamba: “Hata Sila na Timotheo walipoteremka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na bila neno, aliwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo walipopingana naye na kumtukana Mungu,

akakung'uta mavazi yake, akawaambia, damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu, mimi ni safi; tangu sasa ninakwenda kwa watu wa mataifa. (Matendo 18:5-6).

Baadhi ya Wakristo wanayo shauku ya kugonganisha aya za Biblia. wanasema kwamba Bwana Yesu aliagiza kwamba “Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi.” (Mathayo 28:19).

1. aya hii inapinga maagizo yote ya Bwana Yesu yaliyotajwa juu. Kwahiyo haiwezi kuwa

agizo la Yesu wala aya ya Injili.

2. Ya pili aya hii imeandikwa mwishoni mwa Injili ya Mathayo, na nitathibitisha baadaye kidogo kwamba aya za mwanzo na za mwisho za kila kitabu ni za kuongezwa baadaye. Aya zile siyo aya sahihi za Biblia.

3. Ya tatu katika aya 28:19 ya Mathayo neno mataifa limetumika kwa maana ya mataifa ya Israeli. Kama Biblia inavyosema kwamba: “Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu. (Luka 2:1). Kaisari

Augusto alikuwa mtawala wa Roma tu. Hakuwa na mamlaka yoyote nje ya nchi yake juu ya ulimwengu.

Katika aya hii amri iliyotolewa kwa ajili ya ulimwengu na ya nchi ya Roma tu iliyokuwa chini ya utawala wa Kaisari wala siyo ulimwengu wote. Hivyo ndivyo inavyoeleweka kauli ya Bwana Yesu aliposema: “Enendeni mkawafanye mataifa yote (ya Waisraeli) kuwa wanafunzi. (Mathayo 28:19).

  • Tofauti ni Pale Allah Aliporuhusu Waislam kujilinda: "Imeruhusiwa (kupigana) kwa wale wanaopigwa, kwa sababu wamedhulumiwa; na kwa yakini Mwenyezi Mungu Anao uwezo wa kuwasaidia;" (Al Hajj:40)
Kwa mujibu wa Hadithi zilizo sahihi, hii ndiyo amri ya kwanza kuwaruhusu Waislamu kupigana (Zurkani). Maneno ya Aya hii yanaonyesha waziwazi ya kuwa Waislamu ndio waliopigwa vita kwanza, na tena walikuwa wametaabishwa sana na maadui zao. Tena inaonyesha ya kuwa ruhusa ilipotolewa Waislamu walikuwa dhaifu sana, ndiyo maana Mwenyezi Mungu anawaambia maneno ya kuwafariji kuwa Atawasaidia.

Lakini, jambo linalosikitisha ni kuona ya kuwa fundisho hili la dini ya Kiislamu limekosewa kabisa kufahamiwa hata na baadhii ya Waislamu. Wao wanaeleza juu ya habari za Jihadi mambo ambayo si mafundisho ya Kiislamu hata kidogo, na kwa kufanya hivi wamewapa mapadre silaha ya kuupiga Uislamu. Tunatumai Waislamu hao watafumbua macho yao sasa.

Ukristo ndiwo unaoweza kulaumiwa kwa dhuluma za karaha za namna mbaya kabisa. Yesu aliwaambia, "Msidhani ya kuwa nalikuja kuleta amani duniani; la! sikuja kuleta amani, bali upanga" (Mat 10:34). Maneno haya yanaonyesha kwamba Yesu hakuleta amani bali machafuko. Lakini Wakatoliki katika Injili yao wameshindwa kufanikiwa kujaribu kufasiri maneno haya kuwa mradi

wa maneno haya ni wanafunzi wa Yesu kutaabishwa na watu kwa sababu ya kumfuata. Maneno ya Yesu, "Nimeleta upanga" hayakubali tafsiri hiyo. Kadhalika alisema, "Mtu asiye na upanga, auze nguo yake anunue." (Luka 22:36). Maneno haya yanaonyesha waziwazi kuwa anawahimiza wajiandae kwa ajili ya mapigano, siyo wao kuonewa bure kama wateteavyo Wakatoliki.

Ukitazama nyuma katika historia jinsi ma-Papa wa Rumi na maaskofu na wakubwa wa makanisa walivyotumia upanga na moto kwa kuua watu waliohitilafiana nao itikadi, kwa kuwachinja, kwa kuwachoma, kwa kuwatesa mateso ya kila namna, kwa kuwatosa majini, kwa mamia na kwa maelfu, ni mambo ambayo wenye roho ndogo husoma huku miili ikiwatetemeka, mioyo ikiwajaa hofu na huzuni kuwaelemea. Haya yote yanaonekana katika historia walizoandika wenyewe. Watu waliouawa hivi na Wakristo kwa sababu ya dini ni zaidi kuliko 50,000,000.

Wajuao Kingereza watafute vitabu hivi na wasome: (1) Historians History of the World jalada la viii, uk. 352. (2) Encyclopaedia of Religions and Ethics, habari za Inquisition. (3) Buck's Theological Dictionary art. Persecutions. (4) Oswald's Kingdom, etc., pp. 107-133. (5) Dowling's History of Romanism. (6) Fox Book of Martyrs. (7) Charlote Elizabeth's Martyrology. (8) The War of the Huguenots (9) The Great Red Dragon. (10) Histories of the Reformation, na vinginevyo, nao wataona ya kuwa hawa walio vinywa wazi kuusingizia Uislamu karaha, historia yao ni nyeusi kabisa haitazamiki.
 
Maneno yako ya mwishoni 'nikama Yale ya waisrael kupitia musa' yanaonyesha huna adabu hata kwa yule aliyeipokea sheria ile ambayo Yesu pia alikuwa chini yake... Lakini si kosa lako, ni shauri ya upapiaji mambo. Musa au Muhammad na kuabudu masanamu wapi na wapi?
Ugaidi na Quran au Taurati wapi na wapi?
Eh! Weka hata rejea basi hoja yako iwe na kichwa kama si magoti...
 
Jf kuna watu wana elimu humu ila wamejificha....asante na ubarikiwe kwa elimu hii uliyotupa
 
Hapo ndio Allah wanapotofautiana na BWANA wa MAJESHI "YEHOVA" anaposema kupitia kwa mwanae mpendwa kabisa yesukristo wa nazareti mfalme wa uyahudi kuwa samehe 7x70 kabla halijachoea na ukipigwa shavu LA Julia geuza na LA kushoto

Na mnao uzima katika kisasi enyi wenye akili, ili msalimike. (2:180)

Dini ya Kiislamu haikubali mtu ashambulie mwenzake pasi na sababu. Akifanya hivyo na kuuwa basi naye pia auwawe. Linganisha fundisho hili lenye thamani na fundisho la Injili inaposema,"Msishindane na mtu mwovu. Kama mtu anakupiga shavu la kuume, mwelekezee la pili. Kama mtu anataka kushindana nawe katika hukumu na kukutoza kanzu yako, mwachilie na joho vile vile." (Matei 5:39, 40). Fundisho hilo la Injili linapendeza masikioni na pengine mhubiri pia anaweza kusifiwa na wasikilizaji wake, lakini hapajawa na serikali yo yote iliyofuata amri hii kisha ikastawi na kufaulu kuleta amani duniani. Serikali ya Kikristo hasa ndiyo ya kwanza kuua mwuaji na kuadhibu mhalifu. Na kama ingevumilia uasi na uuaji isingeendelea kwa muda mrefu. Kwa ajili hii Mwenyezi Mungu alipoeleza amri ya kulipiza kisasi, alitaka watu watumie akili yao na kufikiri, je, kumwua mwuaji mmoja ni bora au kuacha watu wote katika hali ya kutosalimika. Kweli amri hii ya Qur'an kufuatwa ndiyo amani inaweza kuwapo duniani.


Lengo la kusamehe ni kumpa nafasi mkosaji ajirekebishe. Ikiwa msamaha kwa mkosaji hautakuwa na chochote isipokuwa kuongeza dhara zaidi basi ni dhambi kuutoa msamaha huo...
 
Uislamu na ugaidi sawa na pilau na kachumbari...
 
Uislamu ndio tatizo kubwa linaloikabili dunia kwa sasa.
Hizi ndio kendembwe bila viashiria vyovyote. Yaani unaleta nukuu zako za wapinzani wa Islam kujengea nyumba yako ya barafu ya hoja baharini...!! Leta viashiria hata viwili kama unasema kweli
 
Hivi akitokea chizi mmoja akawaita nyote mnaoamini katika Yesu mkafanye vurugu fulani itakuwa na maana mna usuhuba naye huyo?
Mambo ya kujitekenya mwenyewe halafu unacheka ndio nini sasa! Mbona Bwana Yesu ameamrisha haya yanayofanyika leo lakini haufuati hata chembe?
Bwana Yesu alitayarisha wafuasi wake kwa ajili ya kuleta fujo na vurugu na aliwaamrisha akawaambia: “Lakini sasa mwenye mfuko na auchukuwe, na mwenye mkoba vivyo hivyo, naye asiye na upanga akauze joho lake akanunuwe upanga. (Luka 22:36).
Siyo maneno tu bali katika maisha yake alionesha hata kwa vitendo vyake kwamba alikuwa mtu wa fujo. Biblia inasema kwamba: “Yesu aliingia ndani ya hekalu akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni. Akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa.” (Mathayo 21:12). Akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akizipindua meza zao. (Yohana 2:15).
Kwa sababu ya mafundisho yake, wanafunzi wake walikuwa wajeuri kiasi hiki kwamba walikuwa wakitumia upanga kwa ujasiri. Biblia inasema: ”Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja ya Yesu akanyoosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa kuhani mkuu, akamkata sikio.” (Mathayo 26:51).
Sasa mmesoma historia ya Bwana Yesu Kristo na
mafundisho yake kuhusu kuleta fitina na fujo duniani na kuharibu amani ya watu. Na inashangaza wakati baadhi ya Mapadri wanatangaza au inaandikwa juu ya ‘sticker’ za magari kwamba “There is peace in the blood of Jesus” yaani ipo amani katika damu ya Yesu. Ilhali yeye alikuwa siyo mwenye kuleta amani duniani bali upanga, fujo na fitina.
Sisi Waislamu tunaamini kwamba Bwana Yesu (Masihi) alikuwa Nabii wa Mwenyezi Mungu na alitumwa kwa lengo maalum, lililotajwa kwa ulimi wake katika Qur'an Tukufu kwamba: “Nisadikishaye yaliyo mbele yangu katika Taurati na kutoa habari njema ya Mtume atakayekuja nyuma yangu jina lake ni AHMAD.” (QUR'AN 61:7).
 
Wapi katika Quran? Yaani utachoka hizi rejea zake. Labda ungeuliza wapi kwenye Biblia ametabiriwa.
Halafu Qur'an Tukufu ina tambio moja maarufu sana kwenu nyie mnaoikebehi na kuinadia kutungwa n.k.:
"Je, wanasema ameitunga? Sema: Basi leteni sura moja mfano wake na waiteni mwezao badala ya Mwenyezi Mungu, kama ninyi mnasema kweli" (10:39)
Lakini ajabu unasema imechakachuliwa toka kwenye Biblia! Bado iseme: "2. Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni Mmoja. 3. Mwenyezi Mungu Asiyehitaji, Ambaye wote wanahitaji Kwake. 4. Hakuzaa wala Hakuzaliwa. 5. Wala Hana anayefanana naye hata mmoja.". Utapata wapi aya kama hizo kwenye Biblia? walau hata mfano basi
 
Chanzo si mtume muhamadi na vita yake ya jihad
Hebu anzia mwanzo kidogo. Unasema chanzo? Miaka 13 katika mateso, kuuliwa ndugu au jamaa za karibu na bughudha ya hatari ilipita kisha ukafuata UHAMAJI (HIJRA). Na bado wakafuatwa ili wawatoweshe duniani kabisaa. Ndipo ilipotoka ruhusa ya watu kujilinda lakini masharti hayakukosekana pamoja na vigezo. Jihadi hii ya kuulinda usalama binafsi ilifanyika baadaye sana, chanzo kikiwa wapinzani tu. HEBU REKEBISHA KAULI MKUU!
 
Sikubalk Uislamu kwa kitu kimoja
-Kuwa Dini mona na majini(sisi tunayaona ni mashetani na yameshalaaniwa)
-Peponi kuna mito ya pombe, kufanya mapenzi na wanawake mwanzo mwisho......yaani starehe zilizokatazwa duniani, mbinguni kwa allah ni ruksa
 
hawa jamaa huwa ni waoga sana kama wao ni vidume kweli kwanini wasipigane na hayo majeshi ya marekani wao wanakimbilia kuua watoto na wanawake wasio na hatia
 
Sikubalk Uislamu kwa kitu kimoja
-Kuwa Dini mona na majini(sisi tunayaona ni mashetani na yameshalaaniwa)
-Peponi kuna mito ya pombe, kufanya mapenzi na wanawake mwanzo mwisho......yaani starehe zilizokatazwa duniani, mbinguni kwa allah ni ruksa
😂😂😂😂 wanadai mungu wao kawaandalia wanawake wakutosha
 
Kinachouponza uisilamu ni kitabu chake chenyewe na hasa kuhusi jihad.
 
Hongera ndg, natumai na upande wa pili nao utakuja kwa hoja mujarabu kabisa.
 
Nianze na hoja yako kwamba Qur'an iliandikwa na wahuni. Kwanza kwa maneno yako hayo ya kashfa halafu unajinasibisha na Yesu ni dhahiri umepotoka kwa sababu Yesu hakuwahi kuwakashifu wale ambao hawakumfuata katika mafundisho take.

Kuhusu Qur'an na Biblia ni kitabu kipi kiliandikwa na wahuni? Nitakusaidia ukafanye rejea kwenye Biblia then urudi tena na hoja zikizo wazi badala ya kashfa na kejeli. Jibu utakalolipata, iwapo utakuwa na ufahamu wa kutosha wa biblia utajua kati ya Qur'an na Biblia ni kitabu kipi kati ya hivyo kimeandikwa na wahuni.
A. Ni sehemu gani ya Torah (Old testament) dini ikitajwa kwa jina la mtume kama ambavyo mnajiita Christians? Kwa nini kusiwe na dini ya Adamity, Abrahamity, Mosanity, nk. Hii Christianity imetoka wapi?

B. Ni sehemu gani yabiblia imetaja christianity au Yesu kujiita Christian? Neno christianity lilitumiwa na pagans dhidi yawafuasi wa yesu miaka mingi baada ya yesu kuondoka duniani (Acts 11:26, Acts 26:28, 1 Peter 4:16)

C. Kwa nini mnatumia biblia nyingi tofauti kwa makundi tofauti miongoni mwa wakristo na kila kundi linadai kitabu chake ndio neno sahihi la Mungu. Mfano Revised standard version 1952 na 1971; new american standard bible, the holy bible; new international version, the living bible, new world translatiI on of the holy scriptures (jehovah witnesses), roman catholic version na king james version. Ni wapi katika vitabu hivyo vimetaja neno bible au kujitambulisha kwa mfano "hii ni new au old testament?

D. 8 sept 1957 jehovah witnesses kwenye gazeti lao "Awake" liliandika kichwa cha habari "50,000 ERRORS IN THE BIBLE" , jee makosa hayo yalitendwa na Mungu mwenyewe na yamerekebishwa na nani? Jee bibilia yenye makosa utainasibisha vipi na Mungu aliye mkamilifu kwa kila jambo?

E. Kasome aya zifuatazo uone namna biblia inavyojichanganya:
Matthew 27:50-51; Mark 15:37-38 vs luke 23:45-46
Luke 23:43 vs john 20:17
Metthew 27:5 vs Acts 1:18
Luke 23:46 vs john 19-30

Kwa uchache tambua wasomi wakubwawa biblia wanakubali na wathibitisha kuna maneno ya binadamu kwenye biblia (Curt Kuhl, the old testament; its origin and composition pp.47, 51 na 52). Kwa mantiki hiyo wakristo wenzako walioisoma biblia na wakaifahamu wanaamini SI kila aya ya biblia ni neno la Mungu.
 
Muhammad hakuwa mzao wa Ismail.
 
Mimi naona kwa jicho tofauti. Kuna watu wana maslahi mapana ya kiuchumi na kisiasa ambao huwatumia vijana wafia dini bila wao kujua kutekeleza ugaidi kwa maslahi ya hawa wenye maslahi na ugaidi

Maskini ya Mungu wafia dini hawa wanafikiri kwamba wanachopigana ni jihad
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…