Ahmad Nasibu
Member
- Oct 16, 2013
- 86
- 66
Mkuu kusema ukweli mi huwa napata ukakasi kweny haya mambo.
Yesu Ni issah??/
Yesu maana yake MUNGU MWOKOZI!
Isah maana yake nn?
Manabii wote walikuwa waislam.
Je! Na Mohammed mbona amekiri kuwa ameamrishwa kuwa wa kwanza kusiilimu?
Ukweli nimesoma yooote hayo uliyoyaandka mwisho nikagundua Yesu Alikuja kwa ajili yenu.
Pale Allah Alipowaruhusu kuua kuna tofaut gani na Daud kumuuaذ Goliath?; au Yoshua na wakanani?
- Jesus ni Yesu?
Tuliza kichwa halafu changanua majina yake yote katika mkorogo uliojipika wa Kilatini, Kigiriki, Kiebrania, halafu utuambie la Joshua aliliachilia wapi?
- Aya hii ni wazi sana. Mtume Muhammad s.a.w. ndiye aliyeileta dini ya Kiislamu kwa watu waliokuwa hawaijui. Ni dhahiri yeye mwenyewe ni mtu wa kwanza miongoni mwao aliyeshika Uislamu. Dini ya Kiislamu inakiri ya kuwa Manabii wote waliotangulia pamoja na wafuasi wao walikuwa "Muslimiin" yaani watu waliojitupa kwa Mwenyezi Mungu.
7:144). Je, itakuwa ni uaminifu kufumba macho na kufasiri maneno hayo kuwa Musa ndiye alikuwa Mwisraeli wa kwanza kuamini, na kabla yake hakukuwa mtoto mwingine wa Yakubu aliyeamini? Maneno haya hayaonyeshi ila ya kwamba, katika umati wake Musa mwenyewe ndiye alikuwa wa kwanza kuamini.
Wachawi wa Firauni pia, waliposhindwa na Musa, walisema: "Tunatumai ya kwamba Mola wetu Atatusamehe makosa yetu, maana sisi tumekuwa wa kwanza wa waaminio" (sura 16:52).
- YESU ALITUMWA KWA WANA WA ISRAELI TU
Yeye hakupewa ujumbe wa utume kwa ajili ya watu wote wa kabila zote. Bali yeye alikuwa
Mtume kwa ajili ya wana wa Israeli tu. Mwenyewe alijua mipaka ya utume wake. Kwahiyo alisema: 1. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:24).
2. Wakati mwanamke mmoja asiyekuwa mwana wa Israeli alipokuja kwa Yesu Kristo kuomba baraka zake, Yesu akakataa na zaidi ya kukataa aliwatusi wasiokuwa Waisraeli. “Akasema si vyema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia m’mbwa.” (Mathayo 15:26, Marko 7:27).
3. Hao thenashara (kumi na mbili) Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, katika njia ya mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 10:5-6).
4. Baadhi ya Wakristo wanadhani kwamba wakati Waisraeli wote wamefikishiwa ujumbe, kisha makabila mengine pia yahubiriwe. Lakini dhana hii si sahihi bali ni kinyume cha mafundisho ya Bwana Yesu. Yeye amesema kwamba: “Lakini watakapo wafukuza katika
mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawambia, hamtaimaliza miji ya Israeli hata ajapo mwana wa Adamu. (Mathayo 10:23).
5. Bwana Petro mwanafunzi wa Yesu Kristo aliwahubiri wasiokuwa Waisraeli. Wanafunzi wengine, baada ya kupata habari hii walimpinga Bwana Petro kwa kosa lake. Biblia inasema kwamba: “Basi mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa mataifa nao wamelipokea neno la Mungu. Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye, wakisema, uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. “ (Matendo 11:1-3).
6. Aya za Biblia zifuatazo zinaeleza kwamba Bwana Yesu alikuwa mfalme na mtawala wa Mayahudi. (Mathayo 2:6, 27:29, 27:42, Yohana 1:49.
7. Bwana Paulo ambaye ni mpinzani na mhalifu (anti Christ) wa Bwana Yesu, baada ya kuchukia alianza mahubiri nje ya Wasiraeli. Biblia inasema kwamba: “Hata Sila na Timotheo walipoteremka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na bila neno, aliwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo walipopingana naye na kumtukana Mungu,
akakung'uta mavazi yake, akawaambia, damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu, mimi ni safi; tangu sasa ninakwenda kwa watu wa mataifa. (Matendo 18:5-6).
Baadhi ya Wakristo wanayo shauku ya kugonganisha aya za Biblia. wanasema kwamba Bwana Yesu aliagiza kwamba “Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi.” (Mathayo 28:19).
1. aya hii inapinga maagizo yote ya Bwana Yesu yaliyotajwa juu. Kwahiyo haiwezi kuwa
agizo la Yesu wala aya ya Injili.
2. Ya pili aya hii imeandikwa mwishoni mwa Injili ya Mathayo, na nitathibitisha baadaye kidogo kwamba aya za mwanzo na za mwisho za kila kitabu ni za kuongezwa baadaye. Aya zile siyo aya sahihi za Biblia.
3. Ya tatu katika aya 28:19 ya Mathayo neno mataifa limetumika kwa maana ya mataifa ya Israeli. Kama Biblia inavyosema kwamba: “Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu. (Luka 2:1). Kaisari
Augusto alikuwa mtawala wa Roma tu. Hakuwa na mamlaka yoyote nje ya nchi yake juu ya ulimwengu.
Katika aya hii amri iliyotolewa kwa ajili ya ulimwengu na ya nchi ya Roma tu iliyokuwa chini ya utawala wa Kaisari wala siyo ulimwengu wote. Hivyo ndivyo inavyoeleweka kauli ya Bwana Yesu aliposema: “Enendeni mkawafanye mataifa yote (ya Waisraeli) kuwa wanafunzi. (Mathayo 28:19).
- Tofauti ni Pale Allah Aliporuhusu Waislam kujilinda: "Imeruhusiwa (kupigana) kwa wale wanaopigwa, kwa sababu wamedhulumiwa; na kwa yakini Mwenyezi Mungu Anao uwezo wa kuwasaidia;" (Al Hajj:40)
Lakini, jambo linalosikitisha ni kuona ya kuwa fundisho hili la dini ya Kiislamu limekosewa kabisa kufahamiwa hata na baadhii ya Waislamu. Wao wanaeleza juu ya habari za Jihadi mambo ambayo si mafundisho ya Kiislamu hata kidogo, na kwa kufanya hivi wamewapa mapadre silaha ya kuupiga Uislamu. Tunatumai Waislamu hao watafumbua macho yao sasa.
Ukristo ndiwo unaoweza kulaumiwa kwa dhuluma za karaha za namna mbaya kabisa. Yesu aliwaambia, "Msidhani ya kuwa nalikuja kuleta amani duniani; la! sikuja kuleta amani, bali upanga" (Mat 10:34). Maneno haya yanaonyesha kwamba Yesu hakuleta amani bali machafuko. Lakini Wakatoliki katika Injili yao wameshindwa kufanikiwa kujaribu kufasiri maneno haya kuwa mradi
wa maneno haya ni wanafunzi wa Yesu kutaabishwa na watu kwa sababu ya kumfuata. Maneno ya Yesu, "Nimeleta upanga" hayakubali tafsiri hiyo. Kadhalika alisema, "Mtu asiye na upanga, auze nguo yake anunue." (Luka 22:36). Maneno haya yanaonyesha waziwazi kuwa anawahimiza wajiandae kwa ajili ya mapigano, siyo wao kuonewa bure kama wateteavyo Wakatoliki.
Ukitazama nyuma katika historia jinsi ma-Papa wa Rumi na maaskofu na wakubwa wa makanisa walivyotumia upanga na moto kwa kuua watu waliohitilafiana nao itikadi, kwa kuwachinja, kwa kuwachoma, kwa kuwatesa mateso ya kila namna, kwa kuwatosa majini, kwa mamia na kwa maelfu, ni mambo ambayo wenye roho ndogo husoma huku miili ikiwatetemeka, mioyo ikiwajaa hofu na huzuni kuwaelemea. Haya yote yanaonekana katika historia walizoandika wenyewe. Watu waliouawa hivi na Wakristo kwa sababu ya dini ni zaidi kuliko 50,000,000.
Wajuao Kingereza watafute vitabu hivi na wasome: (1) Historians History of the World jalada la viii, uk. 352. (2) Encyclopaedia of Religions and Ethics, habari za Inquisition. (3) Buck's Theological Dictionary art. Persecutions. (4) Oswald's Kingdom, etc., pp. 107-133. (5) Dowling's History of Romanism. (6) Fox Book of Martyrs. (7) Charlote Elizabeth's Martyrology. (8) The War of the Huguenots (9) The Great Red Dragon. (10) Histories of the Reformation, na vinginevyo, nao wataona ya kuwa hawa walio vinywa wazi kuusingizia Uislamu karaha, historia yao ni nyeusi kabisa haitazamiki.