Je ukiwa mpagani, siku ukifa hauzikwi?

Je ukiwa mpagani, siku ukifa hauzikwi?

under timer

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2021
Posts
389
Reaction score
595
Habari?
Ni wazi mazishi mengi hapa tz yanaitimishwa chini ya dini mbalimbali hata km mhusika alikuwa sio mshirika mzuri basi inaundwa michongoko ili kumlinda na atimaye azikwe kwa iman fulani
Je yule asie na imani ya kidini hata kidogo akifa ni nan husimamia ilo,
Binafsi sijawahi kuona mazishi ya raia wa kawaida yakiendeshwa na serikali hata ya mtaa
 
utazikwa kimyakimya bila ibada ya mazishi ya dini
 
Habari?
Ni wazi mazishi mengi hapa tz yanaitimishwa chini ya dini mbalimbali hata km mhusika alikuwa sio mshirika mzuri basi inaundwa michongoko ili kumlinda na atimaye azikwe kwa iman fulani
Je yule asie na imani ya kidini hata kidogo akifa ni nan husimamia ilo,
Binafsi sijawahi kuona mazishi ya raia wa kawaida yakiendeshwa na serikali hata ya mtaa
Ndio huzikwa mkuu!Kule kwetu Mbeya Miaka ya 1988,Nikiwa huko, Tukuyu chifu alifariki ,alizikwa vizuri sana Tena Ngoma zilialikwa Toka Sehemu mbalimbali za mkoa huohuo,kwa kilugha tunaita Lingoma,lipenenga,magosi na kibhota.
 
Kama huendi kanisani/msikitini na ni mwanachama wa chama cha siasa wanachama wenzako watakuja kukuzika na wataongea abrakadabra za kisiasa katika mazishi yako.tena watakuimbia nyimbo za maombolezo wanazo wamerekodi. Ukiwa muhuni utazikwa na wahuni wenzako, mpagani naye huzikwa na wapagani wenzake
 
Habari?
Ni wazi mazishi mengi hapa tz yanaitimishwa chini ya dini mbalimbali hata km mhusika alikuwa sio mshirika mzuri basi inaundwa michongoko ili kumlinda na atimaye azikwe kwa iman fulani
Je yule asie na imani ya kidini hata kidogo akifa ni nan husimamia ilo,
Binafsi sijawahi kuona mazishi ya raia wa kawaida yakiendeshwa na serikali hata ya mtaa
Unazikwa tu.
Ukiwasikiliza watu wengi, wanaensa kansani kwa hoja nikifa sitozikwa sio kwamba wanamwoga Mungu wanaenda kumwabudi. They just want to be a part of the community.
 
Kuna Yule jàmaa aliua mke na watoto wanñe alizikwa kibabe, maana vijana walibeba jeneza lake wakatimua mbio likawaponyoka likadondoka mwili ukatoka wakaurudisha ndani. Kufika kaburini wakatupia jeneza ndani wakafukia. Mazishi tayari.
Kila mtu atazikwa tu.
 
Ila nimeona watu wengi ambao walikuwa hawaendi knisani /msikitini huwa wanaangalia jina na imani za wazazi wako then anaitwa sheikh au mchungaji unazikwa.
kuna mtu alijifia kichakani, shughuli pevu ikawa ni kutafuta ndugu zake, suluhisho ikawa ni jina lake liliakisi dini gani? Wakaona ni uislam. Fasta akazikwa kwa dini ya kiislam
 
Juzi kati kuna jamaa alikufa kwa ajali ya bodaboda. Tukajiuliza atazikwa kwa taratibu gani? Huko nyuma alikuwa mkristo ila aliacha kwenda kanisani kitambo sana. Kwa kuwa aliwahi kuwa mkristo msiba wake kulipigwa nyimbo za maombolezo za kikristo sambamba na nyimbo za chama fulani. Wachungaji hawakujitokeza badala yake viongozi wa chama ndio waliochukua nafasi za wachungaji wakamzika kichama huku wakiwa wamevaa sare za chama na sanduku likifunikwa kwa bendera ya chama.
 
Wanasiasa wameibuka kuchukua nafasi za wachungaji/mapadri/mashekh kuwa ndio waongeaji wakuu katika misiba ya wanachama wao. Wanajifanya ndio wahubiri, wanamsema vizuri marehemu na kumtetea hata kama alikuwa haendi kanisani au msikitini mbinguni ataingia vizuri tu kwani hakuna ajuaye marehemu alipatanaje na Mungu wakati anakufa. Marehemu hasemwi vibaya husemwa vizuri na huzikwa kwa heshima zote za kichama
 
Unazikwa tu.
Ukiwasikiliza watu wengi, wanaensa kansani kwa hoja nikifa sitozikwa sio kwamba wanamwoga Mungu wanaenda kumwabudi. They just want to be a part of the community.
Sahihi
 
Kuna kuzikwa na kufukia ..

Kuzikwa ni ibada na kufukiwa ni kama kuku mzoga anachimbiwa shimo na kuwekwa humo.
Kwani huwezi kufanyia ibada ya mazishi kiumbe? Maandiko yanasema binadamu Hana Cha kumzidi Mnyama anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa yule.

Nimeona mara kadhaa mbwa wakizikwa Kwa ibada kabisa huko tunakoiga Kila kitu.
 
Back
Top Bottom