Je ukiwa mpagani, siku ukifa hauzikwi?

Kuna wale ambao hawaendi kanisani wala msikitini na hawana vyama au vikundi wapo wapo tu. Hawa wakifa huzikwa kimya kimya bila ibada. Inaweza ikatokea mchungaji fulani from no where akauteka msiba na kuendesha ibada ya mazishi as if marehemu alikuwa mshirika wake, lengo likiwa ni kuwahubiria habari za injili / wokovu walio hai
 
Mtu atazikwa kwa heshima kulingana na status yake aliyo nayo katika jamii alimoishi nayo. Uliacha kwenda kanisani mchongo utafanywa ili tu uzikwe kikristo kwa heshima yako. Kama ni kapuku hujulikani ulikuwa unajumuika na kikundi gani basi utazikwa hivyo hivyo kama desturi ya kuzika mfu ilivyo, mradi tu ufukiwe
 
Kuna viongozi wa dini hufanya ibada ya mazishi nusu au hukataa kabisa kufanya ibada hiyo na kuzua sokomoko na kasheshe msibani. Hudai marehemu alikuwa si mhudhuriaji kanisani wala jumuiya alikuwa haendi, michango yake haijulikani alikuwa anatoa wapi. Nusura kiongozi mmoja wa dini apigwe kwa kukataa kwenda kumalizia ibada makaburini. Aliokolewa ghafla kwa kutoroshwa eneo la msiba kulikokuwa na waombolezaji wenye hasira wakihoji kwa nini akatae kumalizia ibada ya mazishi kwa madai hayo? Waombolezaji wakauchukua mwili kuelekea makaburini huku wakiimba parapanda italia, wakauzika na kuweka mashada bila mahubiri ya kidini
 
Kwani kinachozikwa ni imani au nyamafu?
 
Waislam nao ni walewale wa kukataa kuzika mwenzao kikamilifu. Jamaa mmoja alikufa maji, kwenye msiba sheikh mmoja akasema watamfanyia mambo ya msiba nusu, mengine ndugu zake watajua huko watafanyaje. Sheikh alidai marehemu alikuwa haendi msikitini wala hahudhurii kwenye vikao vya waumini wao. Akasema watamzika kwa taratibu za kidini ila mengine huko nyumbani kwake hawatamfanyia
 
Mi bwana nachukia sana unafki wa binadamu.ukiwa hai hakuheahimu,dharau matusi,mara kakuzushia hili mara akufanyie fujo.
Siku ukifa wanahangaika oh azikwe Kwa heshima,heshima za mwisho,mara tumuombee heri.
Umekufa umelala ndani huna hata chakula na dawa ila masaa machache ukifa watu watakula na kusaza.
Ndio dunia
 
Kwa kifupi ni kwamba misibani kuna vituko vingi sana, hutegemea na marehemu aliishi staili gani ya maisha na watu wanaomzunguka
 
kuna mtu alijifia kichakani, shughuli pevu ikawa ni kutafuta ndugu zake, suluhisho ikawa ni jina lake liliakisi dini gani? Wakaona ni uislam. Fasta akazikwa kwa dini ya kiisl
je bila dini mtu hawez zikwa, kwanini dini?
Yote NI Yale Yale, hizi DINI zimeshawaharibu akili
Ndo hapo najiuliza maana kuzaliwa haiulizwi dini ila kuzikwa had dini
 
ila alizikwa
 
Labda uje na kaburi lako, Tanzania yametengwa makaburi ya waisilamu na ya wakiristu, sasa wewe mpagani uzikwe wapi?
 
Mi nikifa wanitupe ziwa Tanganyika niwe chakula cha samaki
 
Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…