Napingana na wewe aisee kuhusu EU, kwanini
1. Nchi za magharibi haiiogopi Russia kama vile ambavyo mwanzo tulivyokuwa tukiamini, na hii inatokana pale nchi za magharibi kuisaidia Ukraine licha ya putin kutoa mkwara mzito kwa atakayemsaidia Ukraine. Je, nchi za magharibi hazitoi misaada, tena kwa kujitangaza kabisa? Kuna hatua Russia amechukua kama alivyosema?
2. UK alishasema kuwa, endapo Putin akaendelea na vitisho vya Nuclear, UK iko tayari kupeleka silaha za Nuclear Poland. Mpaka muda huu ninaamini nchi za NATO zilizo jirani na Russia zitakuwa zimehifadhi hizo nuclear, putin aliviziwa, nae akaingia kwenye 18 huku akijiaminisha hakuna mbabe zaidi yake.
3. EU ni ngumu sana kukiuka matakwa ya US sababu ndie baba yao, uchumi wao upo hapo kutokana na US after WW II. Unajua watu tunaichukulia simple sana US, hasa huku Afrika. US ni kitu kingine in terms of military, tecs, science, economic etc