Malaika ni miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa na Mungu na malighafi iliyotumika kuumbwa kwa hao Malaika ni malighafi ya Nuru. Na Nuru huwa ni yenye kung'aa na yenye kuangaza. Malaika ni viumbe ambao wapo tofauti na viumbe wengine, kwa nini? Hii inatokana na malighafi iliyotumika kuwaumbia, maumbile yao, kazi zao n.k.
Malaika hana jinsia, hali, hanywi, hamuasi Mungu lakini anapenda na kuchukia. Kupenda kwake akiona kiumbe cha Mungu hususan binadamu akifanya mema na kuchukia kwake ni kinyume cha hivyo. Kingine Malaika hawana maumbile kama ya binadamu wao wana maumbile ya kwao maalum. Hii inatokana na malighafi yao na kazi zao.
Tukirudi katika kuhusu maumbile makubwa ya binadamu wa kale maumbile yao hajasababishwa na kuingiliana na Malaika, bali ni hekima yake Mungu. Ukitizama katika Qur'an kuna aya 2 za sura tofauti. Mungu anatupa habari kuhusu viumbe(binadamu) alivyoviumba ambavyo vina miili mikubwa kuliko binadamu wa sasa . Ila kwa sasa hivi miili yetu Mungu anaifanya ya kawaida, hiyo mosi. Pili ni kwamba kuna aya katika Qur'an Mungu anasema " Tumeijenga Mbingu(ulimwengu) kwa uimara zaidi na tunaendelea kuitanua"
Hizo aya 2 hapo za juu tafuta kongamano moja kati ya Wanasayansi na viongozi wa dini wa Kiyahudi. Wanasayansi walielezea kwa nini viumbe wa kale walikuwa giant na uzito wa Dunia ulikuwa ni mdogo kwa kipindi hicho na hao watu(giant) au binadamu kwa ujumla walikuwa wachache. Na kwa sasa hivi kwa nini watu wana maumbile madogo na wapo wengi na ina uhusiano upi na kutanuka kwa Dunia(expanding earth theory).
Tukija kwenye suala la kuwa na viumbe wengine kwenye sayari nyengine hilo suala nitalijibu kimtindo huu;
Miongoni mwa wana wa zuoni wa Kiislamu wa kisunni kuna mmoja anaitwa Ibn Arab au al shaykh al-kabir ibn Arab Abuu Bakr Al qadir, Wana wa zuoni wanasema huyu Sheikh alikuwa ni Waliy wa Allah. Kuna ahadithi moja kutoka kwa Abdullah ibn Abbas na huyu sheikh ibn Arab ameikoti. Hiyo ahadith inasema kutoka kwa ibn Abbas kutoka kwa Mtume, Mtume anamwambia "Kuna viumbe waliyopo ulimwengu(kwa maana ulimwengu wa tofauti nasi) ewe ibn Abbas ambao wapo kama mimi" ana maanisha maumbile na si Utume. Katika Uislam mmoja miongoni mwa watu akizungumza jambo we have to look in Sharia: Sheikh ibn Arab kutoka kwenye hii ahadith akasema na akapambanua kwamba kuna Dunia(Sayari) nyengine Allah subhanu wataala created na kuna viumbe. Akaendelea akasema " Hao viumbe wapo kama sisi(binadamu) lakini wapo Dunia(Sayari) nyengine.
Sheikh ibn Arab alikuwa na elimu ya ziada kuhusu hii Sayari nyengine, yeye akaiita "Aalam simsima" . Sheikh Ibn Arab Abuu Bakr Al Qadir akasema; Allah subhanahu wataala baada ya kumuumba Adam alayhi ssalaam katika sehemu ya udongo ule ule uliyobaki uliumbiwa Mti wa Mtende. Akatoa ahadith kutoka kwa Mtume swalallahu alayhi wasallam inayosema" Akrimu Ammatakum nakhla": maana ya "Amma" kwa tafsiri nyepesi ni kama kuna udugu fulani hivi. Wataalamu wanasema Tende ndiyo tunda pekee ambalo limejitosheleza amino acid kwa kiasi chake ambacho ndichi kinachohitajika katika mwili wa binadamu. Kwa hiyo, hapa inaonesha ukaribu tuliyokuwa nao kati ya mtende na mwili wetu, yote imetokana na sehemu ya udongo uliyobaki uliyoumbiwa Adam alayhi ssalam.
Sheikh ibn Arab akasema tena, Sehemu ya udongo uliyobaki aliyoumbiwa Adam, ambayo sehemu ya udongo uliyobaki ukaumbiwa mti wa Mtende na sehemu ya udongo uliyobaki ndiyo ikaumbiwa hiyo Sayari ambayo Mtume aliyoizungumzia kwa kusema kwamba "Kuna viumbe wengine katika ulimwengu mwengine ambao wapo kama mimi ewe ibn Abbas" Vile vile akaeleza namna gani ya kufika huko na kurudi. Hili suala hili bila shaka Mawalii wa Mungu ndiyo wanaliweza na Uwalii nao umetofautiana daraja.
Kuhusu Dunia kuwa na tundu na kuna viumbe vingine vinaishi hili suala sina ujuzi nalo.
Mungu ndiye mjuzi zaidi.