Sijafahamu na ndio maana naomba unifahamishe
Kuelewa kuhusu Mbingu na ilipoishia muktadha wake ni huu, na itakuwa ni bora zaidi tukifahamishana kwa mifano.
Kuna Mbingu na kuna Mawingu. Mawingu si kitu kigeni ukitizama juu yale unayoyaona kama moshi unaoelea juu angani yale ndiyo mawingu. Kingeni ambacho kina umiza watu kichwa ni Mbingu. Mbingu ni nini? Iko wapi? Na fikra ama tasirwa ya kusema kuna mbingu wanadamu wameitolea wapi?
Hayo yote maswali binadamu wanajiuliza na tafiti zinafanyika na kuendelea kufanyika ili kuthibitisha Mbingu kama kweli ipo, na asili ya hii dhana yenye kuleta tafakari imetokana na Dini. Binafsi naamini Mungu yupo na ni muumini wa Dini ya Kiislam. Kwa vile bado sayansi(ambayo wengi wao tunaiamini kwamba ndiyo kikomo cha mambo yanayotusumbua) haijaweza kujumuisha tafiti na kuelezea kwa mapana ipo wapi Mbingu na ni nini(?), Binafsi nitalijibu kutoka na Dini yangu inavyoeleza kuhusiana na Mbingu ni nini. Waislam tuna kauli ambayo ni sehemu ya aya katika sura inayosema;
"Al hamdulillahi rabbil' aalamiin"
Tafsiri yake ni, " Sifa njema ni zake yeye Mungu au Anastahiki yeye Mungu au Apasaye kushukuriwa ni yeye Mungu bwana(mlezi) wa ulimwengu wote.
Hapo juu kwenye hiyo aya tumepata neno " Al aalamiin" kwenye hiyo aya inasomeka kama "Aalamiin" ikiwa na maana "Ulimwengu" Pengine tujiulize "Ulimwengu" ni nini? Mungu ametupa akili anatutaka tutafakari kwa yale anayotuambia. Ulimwengu kwa maarifa na juhudi za mwanadamu alizopewa na Mungu, akajaribu kufafanua Ulimwengu ni nini(?). Wanasayansi wanatuambia kwamba "Ulimwengu ni sehemu ya wazi ambayo ni kubwa, ambayo isiyokuwa na mwanzo wala mwisho, sehemu ambayo imekusanya Sayari(Dunia yetu ikiwemo), Nyota, Galaxies n.k; Kwa Kingereza inaitwa Universe( angalizo: ufafanuzi kuhusu Ulimwengu zipo fafanuzi za aina mbalimbali).
Katika aya hiyo hiyo Mungu anasema yeye ni " Rabbi" kwa maana ni mlezi, Kwa nini amesemea hivyo? Tunafahamu kwamba katika Ulimwengu kuna Laws or principles by which everything in the Universe(Ulimwengu) is governed. Kama Immutable and the mutable law na nyenginezo. Sisi Waislam tunasema ni "Mwenendo wa Mungu" kwa maana ndiye amekadiria ziwe hivyo, na yeye ndiye anayeziongoza na tafsiri ya kuongoza haina tofauti na "Rabbi" kwa maana "Mlezi". Kwa mantiki hiyo, tukisafiri kwa aya hiyo hiyo inayosema;
" Alhamdulillahi rabbil aalamiin"
Tafsiri yake ni "Sifa njema ni zake yeye Mungu au Apasaye kushukuriwa ni yeye Mungu mlezi wa Ulimwengu wote. Kwa maana zile kanuni zote zinazoendesha Ulimwengu yeye ndiye Mlezi(bila shaka maana ya Ulimwengu unaifahamu vizuri kuliko mimi)
Turudi kwenye kiini cha swali lako, ni nini Mbingu? Kuna aya katika Qur'an Mungu anasema;
" Ameumba Mbingu na Ardhi na vilivyomo baina ya hivyo"
Tafsiri ya ardhi katukusudia sisi binadamu kwa maana tunaishi katika hii ardhi katika hii Dunia. Dunia ni miongoni kwa Sayari iliyopo katika Ulimwengu. Kwa maarifa na juhudi tuliyopewa na Mungu ama wengine wakijinadi kwamba ya kwao, lakini bado hatujajua Ulimwengu umeanzia wapi na umeishia wapi. Katika Uislam Mtume Muhammad rehmani na amani ziwe juu yake anasema; " Masafa yaliyopo baina ya Mbingu na ardhi ni sawa sawa na chombo kinachokimbia kwa kasi kwa miaka 500" ardhi amekusuduia ni Dunia. Turejelee kwenye aya yetu inayosema;
"Ameumba Mbingu na Ardhi na vilivyomo baina ya hivyo"
Ardhi ni Dunia, na ipo katika Ulimwengu. Kwa maana ukitoka katika hii Dunia ambayo ipo katika Ulimwengu na Dunia yetu ipo katika galaxy ya milk way katika Ulimwengu kwa, tafsiri ya maana: Tukitoka katika hii Dunia vipo ambavyo vipo katika huu Ulimwengu ambavyo ni vipo. Ambapo zipo zillions na zillions za Sayari, zillions na zillions za Nyota na zillions na zillions za Galaxies. Kwa huruma yake Mungu ili atupe tasirwa juu yetu sisi ili kuelewa kile anachotuambia, akasema " Vilivyomo baina ya Mbingu na ardhi" na sisi tukiangalia ukitoka kwenye Dunia ni vingi na hali ya kustaajabisha. Lakini ukirudi mwanzoni mwa hiyo aya Mungu anasema;
" Ameumba Mbingu na Ardhi na vilivyomo baina ya hivyo"
Kwa mantiki hiyo, haya yote tunayoyaona(Sayari, Nyota, mifumo ya Jua, Galaxies) hivyo vyote vipo chini ya Mbingu. Sasa pima umbali tu wa kutoka Sayari kwa Sayari, Galaxies kwa Galaxies, mfumo huo wote ukiupita ndipo unapofika Mbinguni. Lakini Mtume rehma na amani ziwe juu yake, yeye ametuambia; " Masafa yaliyopo baina ya Mbingu na Ardhi ni sawa sawa na chombo kinachokimbia kwa kasi kwa miaka 500" Mtume yupo sahihi, wa kujiuliza ni sisi wenyewe. Alivyosema kasi alimaanisha ni kasi ya km ngapi kwa saa(??) Ila makadirio ndiyo hayo miaka 500 ndipo utakapofika Mbinguni na Mbingu zipo 7. Unataka kujua baada ya Mbingu kuna nini?, na baada ya kuna nini kuna nini?
Nitarudi baadae.