Je, ulikuwa unalijua hili kuhusu Wachawi?

Huu uzi mbona huwa una trend mida ya night kali tu? Kuna jambo si bure πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wakupinga apinge ila wachawi wapo mtu ambaye anajidai hamna uchawi anaweza pia alishawahi kurogwa na hata asijue anakazana tu uchawi haupo
 
Takwimu za wachawi hasa Kwa nyumba za vijijini kwa baadhi ya mikoa unaweza kukuta katika nyumba kumi,basi saba zinamilikiwa na wachawi,na katika sensa ya wachawi idadi yao inazidi kuongezeka Kwa kasi Sana
Hapa kuna kundi la kurithishwa ndiyo wengi Zaidi,na kundi la kununua kama wanawake waenda kwa waganga wakifuatiwa na wafanyabiashara
Hili kundi la wafanyabiashara naweza kusema katika watu kumi basi tambua saba ni wachawi,humo tunajumuisha Viongozi wa dini hata wale unaowaona wanasali sana na kuheshimiwa na jamii
Mnyama anayeongoza kwa kutumika na wachawi ni paka,yaani mchawi anaweza kujibadilisha na kuwa paka,na kama uko makini utamgundua kwa mapozi yake ya kutembea, mfano ukakutana hasa usiku paka wameongozana wawili wakitembea kwa usawa kama watu tambura hao ni wachawi
 
Wakupinga apinge ila wachawi wapo mtu ambaye anajidai hamna uchawi anaweza pia alishawahi kurogwa na hata asijue anakazana tu uchawi haupo
Asilimia kubwa ya wanaopingaga uchawi basi ni wachawi wenyewe,siyo kwa Tanzania hii
 
Binadamu tumegawanyika, kuna wachawi hawa kazi Yao ni kuwapoteza watu,nikisema kuuwa nitakuwa nakosea,mchawi Hana uwezo wa kutoa roho ya mtu,mwenye uwezo wa kutoa roho ni Mwenyezi Mungu peke yake,mchawi anachokifanya anakuchukua kimazingara,unaonekana umekufa,lakini hujafa na utaenda kumtumikia ukiwa mzima na utakutana na wenzako,na siku aliyekuandikia Mwenyezi Mungu ikifika ya kufa utakufa, yeye hana uwezo wa kuzuia usife,maana yake ndugu yenu mnaweza kuzani alikufa akiwa na umri mfano miaka 35 na mkaandika tarehe ya kuzaliwa na kufa wenda kule kwa mchawi ataenda tena kuishi hata miaka 50,inamaana atakufa na miaka 85
Huko maisha yake ni kutumikishwa tu,kama ni uvuvi wa samaki,au kulima inategemeana na eneo la uchumi husika

Kundi la pili ni hili la binadamu wahanga yaani wasiokuwa na Masada wowote ule,tena wenye elimu,kipato,vyeo na Masada katika famΓ­lia zao,hawa wanachukuliwa sana na wachawi
Kundi la mwisho ni binadamu washika dini,na wenye macho matatu,hawa inakuwa tu bahati ulizariwa na ulinzi maarumu,mara nyingi huwa unarithishwa kizazi mpaka kizazi,hapa kama mume au mke unaweza kubahatika ukamuowa au ukaolewa na mtu kama huyu,utafaidika na ulinzi wake
Sasa vita inakuwaga kubwa familia yako ni ya kichawi inataka kukutoa msukule halafu umeowa au umeolewa na mwenye nguvu ya macho matatu anayekulinda,ndugu yangu utaona kila kitu,vita inavyopiganwa yaani unaona live jinsi mama au dada anavyohangaika kukuuwa, ndiyo maana nikasema Vita ya uchawi siyo lelemama itafikia Makati mpaka hamsalimiani Wala kutembeleana,halafu kuna mtu anakuja anasema hakuna uchawi
 
Kwanini wanawake wengi wanapenda uchawi, asirimia kubwa mwanawake?
 
Hapa mtaani kuna kamjamaa kana familia ni kashirikina hatari! Kanaloga hata kijiji
 
EPUKA MIKUSANYIKO YA KUPANGA βœ…βœ…
 
Pole mkuu labda hujaishi vijijini na umri wako bado nahofia, na bado upo nyumbani kwa wazazi, bado hujaanza harakati ya kutafuta maisha na mali. Ukiaza hapo ndo utajua uchawi upo ?
Mkuu ungejadili hoja badala ya kumshambulia mleta hoja

Tunaonglea kuhusu FACT hapa mkuu hatuongelei uzoefu wa maisha

Uchawi na imani za Mungu ni ngano za simulizi za kusadikika kama zilivyo hadithi za sungura na fisi au hekaya za Bulicheka

NO PROOF
 
Wewe unajua maana ya kusadikika, kukihisi kitu ambacho hakionekani make uchawi ni jambo jingine kabisa na linathibitika, mchawi anaweza kufanya kitendo na huku na ww unaona na kikathibitika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…