Pre GE2025 Je, Ulishangaa siasa za Makonda na Ally Hapi? Ya Nape na Makamba utayapata uchaguzi wa 2024 na 2025

Pre GE2025 Je, Ulishangaa siasa za Makonda na Ally Hapi? Ya Nape na Makamba utayapata uchaguzi wa 2024 na 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
3,880
Reaction score
11,134
Tukumbushane zile kelele zenu za DP world ziliishia wapi? Na zile kelele za report ya CAG ziliishia wapi?

Kwa ufupi watanzania wengi ni wasahaulifu na bendera fuata upepo,
Ni vyema vijana wakaendelea kujikita kwenye mambo ya simba na Yanga ,

Vichekesho ni pale watu wa upinzani badala ya kusikitika Nape na Makamba January wanapelekwa kujikita kwenye kuratibu chaguzi za serikali za mitaa na serikali kuu 2025 wao wanawaza wamekomolewa,CCM ni ile ile na watu ni wale wale akina Makonda ,Ally happy

Siasa za Dar es Salaam hazihitaji kutumia nguvu,Hakuna jambo ndani ya ccm linatokea kwa bahati mbaya ,Kila kitu kinafanyika kwa majadiliano
Lengo kuu la ccm ni kushika dola na kuendelea kutawala
January Makamba na Nape Nnauye ni strategical Personel kwenye mambo ya uchaguzi ,Ni Team inayokuwezesha kushinda bila kumjeruhi wala kumuumiza mpinzani

January na Nape wamepunguziwa nguvu za uwaziri na kuachwa huru ili kuondoa mgongano wa kimaslahi na kuonekana wameanza kampeni mapema kumtengenezea mwenyekiti njia

Siasa ni sayansi kama sayansi zingine,Kuondolewa kwa Nape na Makamba kwenye uwaziri ni mkakati maalum kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu wa 2025
Hakuna kura za uhalali wala uchaguzi halali,Kura halali ni ile unayopiga mwenyewe lakini pia inaweza kufanywa kura haramu ingawa ulipiga mwenyewe ikatangzwa hujapata kura yeyote ingawa ulijipigia mwenyewe
Hakuna uchaguzi rahisi bila kuwa na watu wa mbinu na mikakati

Uchaguzi wa 2025 sio rahisi sana labda zitumike mbinu kama zile za 2020,Lakini kwa demokrasia ya Mama Samia January na Nape ni watu sahihi sana kufanikisha ushindi ambao ni halali mbele ya macho ya kimataifa
 
Back
Top Bottom