Nakumbuka nikiwa darasa la 4 kipindi cha mwisho kabla ya mapumziko ya saa nne nimebanwa na mkojo hatari, kwenda kuomba ruhusa lazima useme kwa kingereza maana ilkua kipindi chake,
Uvumilivu ukanishinda nkatoka kwenda kwa mwalimu kuomba ruhusa, sasa lugha inanipiga chenga nkasema kwa kiswahili akanichapa fimbo mguuni akitaka niseme kingereza nikajikuta nimeumwaga palepale kiasi, nkatoka nduki sikurudi tena darasani nikaenda kujificha vichakani hadi kaptula ikauke maana ilkua ya kaki huko njiani wangeniona,
Na nilikua na demu darasani ambae ni binamu yangu, asubuhi nampitia tuende shule akanicheka huku akisema hanipi tena nkamtandika vibao akasema kwa shangazi yake sababu ya kumpiga nikajiongezea tena aibu kwa wajomba wakajua nilijikojolea shuleni.