Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

[emoji23] [emoji23] madem waga ni wajabu mda mwingine, yani mbwembwe zote nabado ukaja ukang'oa..! Mie ningelipiza sio kwa kuabishana uko
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Mimi mwaka 2011 nilikua mkaka fulani ivi... Nilikua nasoma kozi ya computer pale New Horizon mnazi mmoja, nikakutana na kioenzi changu tukatembea mpaka maeneo ya posta na kutulia kwenye mgahawa flani. Tukaagiza pepsi wenyewe, hatukutaka makuu. Bili imekuja tunadaiwa buku mbili... Wacha kaka jasho limtoke! Kumbe alikua na hiyo buku jero tu mfukoni, nikaongezea hela tukalipa. Ikabidi nimpe ata na hela ya nauli. Tuliona aibu sana ila mkaka aliona aibu zaidi. Ila tukawa pamoja kwa mda mrefu tu!
 
Me niliwah kugombania daladala yan ule mbanano na mvutano wa mlangoni mpaka nafika kwenye siti vifungo vya blauzi vyote vimetatuka brazia hii hapa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ndo ukute wale wa kuvaa bra na shati tu!!! Full aibu
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Yaan tangu nianze kusoma posts kwa hii maada hii imenifanya kucheka mpaka machozii[emoji4] [emoji4] [emoji4]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji15] [emoji15]
 
Form 1 hiyo ndio nimeingia, mikoa ya baridi nkajikojoleaga kitandani, kuitwa ofisini mwa mkuu wa shule
Akauliza, what did you do last night? Inabd kujibu kingereza Mimi nimetokea kayumba, ikabd ni-mute kudadeki
Mpaka alivyoniuliza kiswahili, ndio nkamjibu nimekojoa [emoji23]
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Hahaha....ila ulimwelewa jamaa maana wanawake wengine atakuchambaaa
 
Hahaha ulikuwa kilaza balaaa...wewe me au ke
 
Me niliwah kugombania daladala yan ule mbanano na mvutano wa mlangoni mpaka nafika kwenye siti vifungo vya blauzi vyote vimetatuka brazia hii hapa
Ningekuwepo ningekuvulia shati najua siku moja ungenikumbuka ktk ufalme wako wa mahaba.
 
Mm iliwahi nikuta moja hio nimesahau neno moja la kiingereza tulikua kwa bus tunasafiri.
So tukawa tunagombea siti na binti flani anataka aniweke mm siti ya dirishani wakati mm nimekata ya mwanzoni.
So katika kumuelekeza (hapo nabong'oa ngeli tu) nikamwambia "go check the nanii" hio nanii nikiwa namaanisha wao wa mabus wanaita chart. Daaah nilijikuta mwenyewe nimenywea ikabidi nisogee dirishani tu daaah. Sikutia tena story na yule mtoto hadi tunafika mkoa.

Maajabu asubuhi nawahi stand niende wilayani kwenye bus nlopanda tena namkuta yule binti. Sikutia neno hadi nafika wilayani.

Nnazo kibao. Ila ya kwanza hio.
 
Daah me nakumbuka secondary fom foo iyo kimtindo nilikuwa muhuni flani ivi kaya sana (bangi) mixer na ugoro na vilevi vyingine vikali. Nilikuwa nna tabia ya kuchelewa shule kutokana na hangovers za viroba mixer na value ...nakumbuka mpk namaliza foo niliwahi ingia paredi mara mbili tu. Sasa kuna class moja ivi mimi nikiwa na wahun wenzangu tuling'oa zile chuma za grill tukafanya ndo njia ya kuingia skul. Tukishaingia hiv class ile chuma tunaitegeshea, sasa kuna siku tukawa tumechelewa kama kawaida etu; tukaenda pale drishan ili tupenye tuingie ndan ...kumbe siku iyo kulikuwa na msala banaa, kuna uyo mwalimu flani hiv mnokooo alikuja gundua so siku iyo akatoa wanafunz ote wa ile class wataje ni akina nan wanapitaga drishan. ..ilikuwa ni msala balaa. .watu walikula fimbo ci kitoto. Sasa sisi bila kujua tukawa tunajijia zetu ili turuke tuingie clas, kumbe yule mwalim alikuwa nyuma etu akitufwatilia tu ...tulikuwa mtu kaa tano hiv kumbe wawili walimwona halafu hawajatusanua so wakasepa ...daaaaaah!! Kimbembe sasa tumefika pale drishan tuko watatu tu halafu mim ndo nilikuwa wa mwisho. Sasa tumefika pale drishan kuchek ndan clas hamna mtu. Ko tukamtuma mmoja aingie akachek wanafunz wameenda api. .si akaingia banaa; nje tukawa wawili na yule mwalim. Sasa mistake niliofanya, mim nilikuwa sigeuk nyuma kbs mawazo yang yote ilkuwa ni kuingia clas tuu ..na apo nilikuwa niko high kinyamaaa nilishatupia vitu kichwan. Sasa yule mwalim nyuma angu akawa ananiuliza "oyaaa ruken asii" me namjibu "vungaa" nikijua namjib mselaa ...sasa yule mwenzang ambay alikua mbele si akageuka ile kugeuka tu akakuta ni ticha yko nyuma angu. ...kilichofata apo ni bonge la tusii "wee mse**e unabonga na ticha mda ote huo na ujui!!" Ile na mim kugeuka ni ticha kwelii. Kilichofata apo ni kila mmoja alitafutana na njia akee hahahaha ...story ni ndefu sanaa acha niishie tu hapaa. Ila namshukuru Mungu nilitoka salama na three japo ya penati nkaenda advanc private. Daaaah noma sana iseee[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Huu uzi unafanana sana na ule wa [BOLD]mwenye stress pita hapa[/BOLD]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…