Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Daah nyengine hii..
Yaani kuna sku nimekuja na demu wangu geto kumgegeda
Mara simu yangu ikaita daah fasta kaipokea si alikua mchepuko wangu balaa likaanza hapo yaani demu haelew lugha bas isiwe tabu demu akatoka nikamfata kumsindikiza home kwao

Nikajikuta nimepanda daladala huko nimesahau kila kitu yaan sina wallet sina smu na mfukon sina hata mia na demu kanuna ajabu hata hatak nimsemeshe


Hahaha siku hio ndo niligindua mademu wana imani sna

Konda kuja anadai nauli sina kitu bas demu kuona konda anaanza kuongea akanitolea

Yaani nilishkuru sna kuniepusha na aibu

Ila kuanzia hapo mm na yy ikawa basi hadi hii leo naandika hii commet
 
Niko darasa la pili, miaka hiyo ya 90. Ni muda wa mapumziko, tupo na mpira wa chandimu, tunacheza mbele ya darasa na wenzangu!!

Nimebanwa ushuzi, nikaona isiwe tabu kwenda nje, nikajisemea kimoyomoyo, ngoja niwakomoe ntajamba kwa nguvu na kwa sauti !!

Shetani akawa upande wangu!! SIKUJAMBA.

Nilikunya mbele ya darasa, kilichosaidia nilikuwa na pensi ndani, nikakimbia toilet nikasaula pensi nikatupa ndani ya choo kilichojengwa kwa msaada wa HESAWA.

sorry! it was surposed to be a secret!
Duh noma sana aisee
 
Me niliwah kugombania daladala yan ule mbanano na mvutano wa mlangoni mpaka nafika kwenye siti vifungo vya blauzi vyote vimetatuka brazia hii hapa
hahahahhahahha daah pole sana
 
Ahahaha...mkuu mimi kuna hii niliisahau
Wakati ATM ndiyo zinakuwa mashuhuri hapa tauni mzee alikuwa anamwagiza bro akachomoe mkwanja. Sasa mimi si nikawa naenda nae nasimama mbali maana kwenda wawili si hairuhusiwi may be unasaidiwa.

Siku moja nikapata emergency mzee hayupo then natakiwa nimfuate Tanga. Akaniambia nichukue ATM nikachukue angalau nauli kidogo.

Ishu Ikaja nina kadi ya NMB then nikaenda machine ya DTB..[emoji23][emoji23][emoji23]. Nimezuia foleni ya watu huko kila nikiingiza kadi inaleta mapicha picha. Hadi Askari akaja akaniambia tatizo nini? Nikamwambia haisomi akanipeleka ndani. Ile officer wa DTB anaangalia anakuta nina kadi ya nmb alikasirikaaa akataka kunizabaaa nilichomooka ndukiiii [emoji23][emoji23][emoji23] watu wote benki wakawa wananiangalia navyopotea
Niliaibikaaa saana siku hiyo aseeh
hahahhhahahaaa hiii kiboko
 
Nilikua napenda kuingia vyumba vya wazazi kila nyumba nnayotembelea,sasa nikiwa form2 likizo nikatumiwa nauli niende kwa Mjomba aliyekua ameoa na mkewe ni mjamzito nikasaidie kidogo,kesho yake wakaenda kazini asubuh mi sikujua kumbe shangaz kwa hali yake anatoka mapema sa nmeingia kuoga nikatoka vuuup hadi chumban kwao, kunyonga kitasa kikaitika nikaingia mzima mzima heee!.shangazi huyu hapa kakaa kitandani afu akaniuliza kwa upole vp shangazi vyumba vimekuchanganya??...mi huku machoz yanalenga nikaitika kwa kichwa afu nkatoka taratibu,....yani aibu ile sitaisahau
 
Form 4 hyooo.mwana kaniambia twende tukamsalimie maza ake kariakoo.tukaenda.kivumbi ilikuwa mlangoni.kuvua viatu sitaki.maana vinanuka balaa.yaani sijavua lakini harufu naisikia.nikaingia navyo sebuleni kiubishi ubishi.bahati nzuri kulikuwa na tiles tu.ila shuhuli waliipata.
Hahahahaa

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
 
Me nakumbuka nilimtembelea mamdogo town so nkawa nmebanwa kiu nikakasogelea kafriji nikafungua nkaona mzinga.wa chupa wa vineger nkaufananisha na maji poa wacha nijimiminie kwa raha zangu kilichokuja kunistua ni ile.ladha ya ndimundimu
hahahaha
 
Nilikua napenda kuingia vyumba vya wazazi kila nyumba nnayotembelea,sasa nikiwa form2 likizo nikatumiwa nauli niende kwa Mjomba aliyekua ameoa na mkewe ni mjamzito nikasaidie kidogo,kesho yake wakaenda kazini asubuh mi sikujua kumbe shangaz kwa hali yake anatoka mapema sa nmeingia kuoga nikatoka vuuup hadi chumban kwao, kunyonga kitasa kikaitika nikaingia mzima mzima heee!.shangazi huyu hapa kakaa kitandani afu akaniuliza kwa upole vp shangazi vyumba vimekuchanganya??...mi huku machoz yanalenga nikaitika kwa kichwa afu nkatoka taratibu,....yani aibu ile sitaisahau
hahaha
 
siku moja nikiwa china tumeenda shopping nikawakimbia masela , nikaingia kwenye mall moja kubwa sana nikapanda lift huyo hadi maduka ya ghorofani... nimemaliza shopping nikapotea na nisijue pa kutokea na huku nje jamaa wananitafuta kuona hawanipati wakatoa taarifa polisi then wale polisi wakawataarifu wenzao waliomo ndani ya ile mall kuwa wakiona black man wam'escort to the exit. Kimbembe kimekuja hapa sasa, askari alivoniona akawa anakuja na mm nikaanza kumkimbia aisee tulitimuana mle ndani sitakaa nisahau. Mpaka nimechoka jamaa akanipeleka kwa masela huku nimepata aibu ya karne
hahaha
 
Sometimes huwa tunafanya mambo kimazoea na kujitia ujuaji mwingi.
Najua mwana JF kuna siku uliaibika Aidha kwa ushamba ulionao, kujitia mjuaji ama kutokuwa na ufahamu juu ya Mambo fulani fulani.

Mimi: kipindi cha nyuma tulienda hotel moja kuogelea/swimming. Tulikuwa mobb ya watu kama 12(ke&me). Sasa kiubaridi cha saa 12 kikanipiga nikasema isiwe kesi ngoja nibugie hata tuvikombe tuwil twa kahawa nipunguze baridi. Washkaji waka ni alert ila nikasema liwalo na liwe walet ina 15000tsh bhana! haiwezi kuzidi hapo. Nikaitisha kahawa yangu... ile namalizia mhudumu/mama anakuja kukusanya vyombo vyake na sukari yake nyeupe( maana niliibakiza) nikapewa bill ya tsh 22500 [emoji23][emoji23][emoji23]. sheee tabala roi. Mimi nilijua mbalauni kama kwa mama clareee kumbe nauli ya chuga- moro kbs???

Na mmaza wa watu anataka kuondoka na pesa yake. Ikabidi washkji wajichange kimya kimya 6500 ikapatikana. Ila nilikiona cha moto kutembea kwa miguu kutoka hapo mpaka nyumbani. Na Nashukuru mamy siku hiyo sikuongozana naye.

Msinicheke wengi yametukuta. Je na wewe yalikukuta yapi???

[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Back
Top Bottom