Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Siku moja natoka zangu bush naelekea town na tu kandambili twangu , sasa nilipofika centre ya Town yenyewe, kutokana na kushanga shanga midoli iliyo kaah kama watu bahati mbaya nikajikwa, ebwana wee kandambili moja ikakatika, ikawa hakuna namna, na tuhela twangu niliokuwa nimeuza kuku nikawa nimeweka M-pesa, bas ikabidi nianze kutembea Kandambili moja mkononi na moja mguuni mpaka nilipo ipata kituo cha kutolea na kuanza kutafuta fundi anishonee.

Yani ilikuwa igizo si igizo.
 
Rai don't you believe kuna hotel za bei hiyo bongo??
Oasis ya morogoro navyoongea now kahawa 1 cup ni 4500. Na ni hotel ya kawaida saana kwa wanaoifahamu...
hahahahah umenikumbusha tulienda sehem fulani kula piza na mchizi wangu,Pizza mbili.mishikikaki na juice zetu jioni ikawa imeisha tukaomba bili......tobaaaaa kitu kikasoma 49500. Hahahaha. Mkononi kuna hamsini likabaki jero,wacha tuukanyage kurudi majumbani.....hahahahaha........
 
Huu Uzi bwana! kila nikiupitia huwa nacheka mpaka machozi yananitoka .....lol
 
Yaan sitaki hata kukumbuka nilivyo aibika lol[emoji18]
 
ilikuwa primary darasa la sita sa kuna kademu kalikuwa kananielewa kinoma siku hyo kakaja kwetu mi mwoga mwoga sijui mambo ya kunjunjana. bro kakashawishi kakakubali tukapige mtungo. sa broo akaanza kaniambia mi nikae mlangoni nicheki so coz mshua alikuwepo home but anapenda kukaa njee sna kuingia ndani labda taarifa ya habari.. apo tumekubaliana kuwa mtu akitokea nipige mluzi sa ghafla nimesimama mlangoni nato shingo nje mshua hyu apa si nkashindwa kupiga mluzi nikasema kwa nguvu hyooooo. mshua kastaki then kanambia em sogea hapo kaingia ndani kawafuma broo na kidemu kakatiwa vibao kakasepa home kwao...hahah bro kashikwa dushelele mzee kaivuta huku anamwmbia naikata leo ndo inayo kuponza.................itaendelea
Ha haaa haaaaa aisee! ahsante kwa kuniongezea siku nimecheka sana aisee
 
Hehehe na hao masela wako wangekua ndo wanamuamkia huyo manzi basi usingeshindwa kumuamkia ukaitikia mwenyewe and i bet ulikua umekaa pale kwenye mapultable mengi mashine3

form1
😀😀😀😀😀😀😀😀😀......Dah,NOMA SANA AISEE!
 
.
Sometimes huwa tunafanya mambo kimazoea na kujitia ujuaji mwingi.
Najua mwana JF kuna siku uliaibika Aidha kwa ushamba ulionao, kujitia mjuaji ama kutokuwa na ufahamu juu ya Mambo fulani fulani.

Mimi: kipindi cha nyuma tulienda hotel moja kuogelea/swimming. Tulikuwa mobb ya watu kama 12(ke&me). Sasa kiubaridi cha saa 12 kikanipiga nikasema isiwe kesi ngoja nibugie hata tuvikombe tuwil twa kahawa nipunguze baridi. Washkaji waka ni alert ila nikasema liwalo na liwe walet ina 15000tsh bhana! haiwezi kuzidi hapo. Nikaitisha kahawa yangu... ile namalizia mhudumu/mama anakuja kukusanya vyombo vyake na sukari yake nyeupe( maana niliibakiza) nikapewa bill ya tsh 22500 [emoji23][emoji23][emoji23]. sheee tabala roi. Mimi nilijua mbalauni kama kwa mama clareee kumbe nauli ya chuga- moro kbs???

Na mmaza wa watu anataka kuondoka na pesa yake. Ikabidi washkji wajichange kimya kimya 6500 ikapatikana. Ila nilikiona cha moto kutembea kwa miguu kutoka hapo mpaka nyumbani. Na Nashukuru mamy u
siku hiyo sikuongozana naye.

Msinicheke wengi yametukuta. Je na wewe yalikukuta yapi???
Naufufua tena huu uzi
 
Me niliwah kugombania daladala yan ule mbanano na mvutano wa mlangoni mpaka nafika kwenye siti vifungo vya blauzi vyote vimetatuka brazia hii hapa
Daaar Maskin pole ,hapa nmevuta taswira nkaona kabsa ulivyokua ,pole sana mpendwa
 
hahahaha, sijui kama hii inastahili kuitwa ushamba, ila ni aibu iliyotokana na ukauzu.

likizo moja ya advance tulirudi home na tukajikuta classmates wa o level tuko mtaani. basi matembezi ya mida kama saa 8 mchana, mob kama ya watu wa4 tukasema tupite kwa classmate wetu pia aitwa clara(sio jina lake halisi). bahati nzuri au mbaya na mama clara pia alikuwepo. haya yalikuwa mazungumzo yetu.

mama clara: karibuni wanangu, hamjambo?
sisi: hatujambo mama shikamoo?
mama clara; marhaba, mmekuta tumemaliza kula ngojeni niwaandalie.
baadhi yetu; Usijari mama tumeshakula.

basi zikaendelea mazungumzo ya hapa na pale, sisi na clara, baadae mama clara nae katujoin ili kuzisikia habari za boarding na advance (maana tuliosoma advance na kuishi wilayani 'nyakati hizo' ilikuwa ni respect of some kind mtaani na kwenye familia).

Ghafla katika hali isiyotarajiwa mwenzetu mmoja aitwaye Patrick akasonya na kusema, 'Mama mimi nikuambie tu ukweli, mchana hatujala na tunanjaa mno'. hahahha. tulipigwa butwaa ila msela kakaza sura, nakisha kutuuliza kwani nyie mmekula.

kwakweli kwao clara palikua 'ushuani' sana na mama clara alikua na 'ulokole fulani'. pale pale mama akasema ngojeni niwaandalie chakula wanangu. ilibidi mama achambue mchele atupikie lunch.. msosi tulikula lakini hali ya kichwani haikua sawa kutokana na fedheha niliyoifeel.. ila 'msela' Patrick kigumu yeye akapiga sahani mbili kabisa. tumetoka hapo njiani sikutaka hata kumsemesha. 😀😀😀😀
 
Me niliwah kugombania daladala yan ule mbanano na mvutano wa mlangoni mpaka nafika kwenye siti vifungo vya blauzi vyote vimetatuka brazia hii hapa
Nimecheka kwa sauti[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hahaha aisee unanikumbusha mbali sna

Nilienda town one day na jinsi yangu nyeupe yaani Nimefunga pamba fresh

Si nije kuteleza ktk mtaro wa maji taka yaani jinsi yote na flana full maji taka na mfkoni sna ata hela ya kununua nguo zengine na home sio karibu

Daah ilinibidi nipige boda to boda la mitaa kwa mitaa yaan nilizunguka ili nijifiche wachizi na watoto wakali wanaonijua wasije kuniona

Ilikua balaa hadi nafika home
 
ilikua form3 majira ya asubuhi nimegonga chai na kiporo cha makukuru then tumeingia kupiga test, basi tumejipanga fresh kilamtu na kiti chake, mm npo katikati ss ile tumegaiwa karatasi za maswali tumbo likavuruga kidogo afu nkaskia kama kigesi chembamba kimegonga hodi, kuangalia kulia na kushoto raia wakobize wanaperuzi maswali, nikawaza kwan nani atajua bhana pasipo iyana nikapumua kibingwa[yusuphhh], duh sikujua nilichofanya kilikua na maajabu gani mpakapale nilipoona darasa zima wakiongozwa na msimamizi wakitokanje speed huku wakipiga kelele na mm nikafuata mwisho sikumbuki walichosema lkn nlisikiawakitaja jinalangu huku wakicheka sana, duh huwezi amini nlijikuta natabasam maskini mm
NB:fikiri mara mbili kabla hujaachia shuzi la kimya kmya
Noma sana aisee
 
Back
Top Bottom