Je, ulishawahi kulazimisha mpenzi au rafiki aendelee kubaki maishani mwako?

Je, ulishawahi kulazimisha mpenzi au rafiki aendelee kubaki maishani mwako?

Kosa kubwa ni kuweka mategemeo yako KWA mwanadamu, dunia inabadilika,watu wanabadilika tuko kwenye process Muda wote ni kama tunaevolve hivi,Tunaingia na kutoka kwenye mahusiano constantly,ukiingia ukakuta uhusiano haufullfill requirements zako unatoka,unaenda pengine na pengine,process nzima iko centered kwenye needs zako wewe unayeingia na kutoka,ambazo hizo needs unakuta tu ni ishu fulani fulani personal(self centered)
Na kibaya zaidi kila mmoja wetu anaevolve ,KWA kifupi ni kwamba HAKUNA BINADAMU ASIYE NA MIZINGUO including wewe mzee baba mleta post,unaweza kuwa rafiki mzuri sana KWA watu fulani na wewe huyohuyo ukawa worst friend KWA watu wengine, tuko kwenye web ya continuous PLEASURE na DISSAPOINTMENTS na hizi pleasure na dissapointment wakati mwingine sisi ndio vyanzo wakati mwingine wengine ni vyanzo,

Nazunguuuka ila point yangu ni hii MAISHA YAKO FAIR KWA KUWA HAYAKO FAIR KWA KILA MTU,kila mtu anaona anastahili vitu fulani na havipati,anastahili kuwa na watu fulani around na hawapati,life does that to everyone!, Everyone!

Nature ya binadamu huwa Ana tabia ya kulinda interest zake,Hizo interest zake zikitibuliwa na mtu wa karibu ndo BAD FRIENDSHIP zinaibuka hapo mambo ya MUACHE AENDE yanaingia,
Urafiki ukivunjika,mapenzi yakivunjika mtu anayetakiwa kukamatwa wa kwanza kabisa ni wewe uliyekuwa kwenye huo urafiki/mapenzi na ukikamatwa ukatoa maelezo waweza kuta kuna FAMBA kibao ulifanya unconcously ,and since you did without being conscious unajiona INNOCENT

Just celebrate your individualism without putting too much pressure on others, assume that this life is one big piece of cake, so big and enough for each one of us, everyone is taking his/her share, take your share quietly and leave.
Ujumbe mzito sana
 
mi nang'ang'aniaga ili akikubali nimkule ya mwisho tu alafu nisepe!! yaan kinachonifanya ning'ang'anie ni ili akikubali mi ndo nimuache sio aniache teh teh!

ongeleeni maumivu yote mnayoyajua ila maumivu ya "mko kikundi cha watu 8 harusini, wote wanapata sahani ya pilau na wewe unakosa" sio maumivu madogo ni makubwa sana, na kuzuia machozi ni kipaji kwenye mda huo.
Hahahahaha ni fala sana wewe chaliii anguu
 
Kosa kubwa ni kuweka mategemeo yako KWA mwanadamu, dunia inabadilika,watu wanabadilika tuko kwenye process Muda wote ni kama tunaevolve hivi,Tunaingia na kutoka kwenye mahusiano constantly,ukiingia ukakuta uhusiano haufullfill requirements zako unatoka,unaenda pengine na pengine,process nzima iko centered kwenye needs zako wewe unayeingia na kutoka,ambazo hizo needs unakuta tu ni ishu fulani fulani personal(self centered)
Na kibaya zaidi kila mmoja wetu anaevolve ,KWA kifupi ni kwamba HAKUNA BINADAMU ASIYE NA MIZINGUO including wewe mzee baba mleta post,unaweza kuwa rafiki mzuri sana KWA watu fulani na wewe huyohuyo ukawa worst friend KWA watu wengine, tuko kwenye web ya continuous PLEASURE na DISSAPOINTMENTS na hizi pleasure na dissapointment wakati mwingine sisi ndio vyanzo wakati mwingine wengine ni vyanzo,

Nazunguuuka ila point yangu ni hii MAISHA YAKO FAIR KWA KUWA HAYAKO FAIR KWA KILA MTU,kila mtu anaona anastahili vitu fulani na havipati,anastahili kuwa na watu fulani around na hawapati,life does that to everyone!, Everyone!

Nature ya binadamu huwa Ana tabia ya kulinda interest zake,Hizo interest zake zikitibuliwa na mtu wa karibu ndo BAD FRIENDSHIP zinaibuka hapo mambo ya MUACHE AENDE yanaingia,
Urafiki ukivunjika,mapenzi yakivunjika mtu anayetakiwa kukamatwa wa kwanza kabisa ni wewe uliyekuwa kwenye huo urafiki/mapenzi na ukikamatwa ukatoa maelezo waweza kuta kuna FAMBA kibao ulifanya unconcously ,and since you did without being conscious unajiona INNOCENT

Just celebrate your individualism without putting too much pressure on others, assume that this life is one big piece of cake, so big and enough for each one of us, everyone is taking his/her share, take your share quietly and leave.
Ushauri wako na maneno yako ni kweli kabisa.. Tatizo mkuu moyo..Kwa mie ambae napenda kua na kitu kimoja tu always mbona kazi ninayo.
Mzee baba itakua either umeumizwa saa so umekua monster au hujaumizwa hujui ilivyo..😆
 
Ushauri wako na maneno yako ni kweli kabisa.. Tatizo mkuu moyo..Kwa mie ambae napenda kua na kitu kimoja tu always mbona kazi ninayo.
Mzee baba itakua either umeumizwa saa so umekua monster au hujaumizwa hujui ilivyo..[emoji38]
Waache waje maishani mwako,wakichoka waache wasepe kama walivokuja,na wewe huko unakoingia,ingia tu ukichoka sepa kimya kimya bila kelele,ndo cycle tuliyomo mzee baba ,hizi illusion za UNCONDITIONAL LOVE/FRIENDSHIP ukizifata utapata tabu Sana,UNCONDITIONAL LOVE ni highest expression ya Divinity,ni kitu Sacred, And humans aren't that sacred,they aren't even close to sacredness ,
Binadamu mostly tunaishi maisha mawili
1.maisha ya kwanza ni for Public display (highest form of hypocrisy) maisha yaliyopakwa rangi za uongo na kweli
2.maisha ya pili ni maisha yetu halisi,hii ni intrinsic feelings na Emotions,(hii part huwa inafichwa) huku ndo kuna makorokoro kibao,hii part ni sawa na mzazi aliyezaa mtoto mlemavu anamficha ndani ili watu wasijue,ila huyu mtoto kuna wakati anaforce kutoka nje,ndo Inakuwa AIBU,hata huyu amefanya hiviii?
Kumbe anafanya kila siku kimyakimya ni siri yake tu .

Hayo maelezo hapo juu yanatuhusu binadamu wengi mno.
 
Mizunguko yetu ya kimaisha inatuletea watu ambao wanaweza kuwa changamoto sana. Kuna mtu nimekutana nae 2016 tuko marafiki wazuri japo tunagombana mara nyingi. Ishu ni kwamba sitaki kumpoteza japo najua ninavyoendelea kumshikilia naendelea kumuumiza zaid😭😭😭
Nikupe pole sana..ukweli ni kwamba kuna wakati hata uwe gaidi kivipi.. there's a point of no turning back. Yaani lazima ushikike tu maana everyone need to belong to someone..who Love
Pole sana je una mpango wa kutafuta mbinu za kumpoteza
 
Habari wakuu.

Kwenye mizunguko yetu ya maisha kuna wakati unakua upo very attached na mtu Fulani either ni rafiki wa kawaida kama Man to man au Man to woman, pengine ni mpenzi wako umpendae sana sana. Yaani unakuta una mpenzi roho yako imetokea kumpenda sana husikii wala huoni juu yake, kila muda unatamani uwe nae karibu au kuwasiliana na nae. Au kama ni rafiki yako wa kiume unakua kila ukitaka kufanya kitu Fulani unamstua mshikaji wako, yaani kama kuna ishu unatka kufanya mshikaji wako bila kuwepo unaona unaifanya kimagumashi. Kiuhalisia unakua upo mentally attached to that person, unakua umempa nafasi kubwa sana mpenzi wako au mtu huyo kwenye akili yako na maisha yako kwa ujumla.

Je huo upendo na nafasi kubwa uliyompatia kwenye maisha yako ushachunguza kama naye anakupatia nafasi hiyo? Jibu ni No! na kama ni Yes basi nafasi hiyo amekupa kwa muda, kuna muda utamtext atakujibu kwa wakati wake, utatamani kuongea nae ila yeye ataona unaboa tu, utataka uonane nae yeye atakuona msumbufu.

Ikifika hatua unaona mtu yupo online unamtext pm ana like tu, unamtext wasap ana soma then anakaa kimya sana au unamtext kwa sms halafu yeye kaka kimya wakati unajua hiyo sio kawaida yake jua kwamba huna chako hapo, utakua unalazimisha mawasiliano, mapenzi au urafiki ambao mwenzako hautaki tena.

Kwanini ulazimishe mawasiliano au mapenzi ? Kila kitu chatokea kwa sababu. Unajua unapompenda na kumjali mtu sana kiasi asicho stahili utaishia kupata maumivu usiyo stahili..

Subconscious mind hutenda kazi ikishirikiana sambamba na Nature, kuna hali Fulani unawez kua nayo katika maisha labda ni upweke,huzuni,kukosa faraja kiufupi unakua huna furaha au amani ya maisha. So kinachotokea ni kwamba
Subconcious mind inawasiliana na Nature kua mwanadamu huyu (yaani wewe) una matatizo Fulani maishani inaiamuru nature kutafuta mtu wa kuja maishani mwako ambae ataendana na hali ile uliyonayo.

Baada ya muda mfupi utajikuta umepata rafiki ukawa nae anakuliwaza kweli hadi ile hali ikawa imeisha..Mind ikishaona mentally ya huyu mtu iko stable inamuamuru nature kuruhusu yule mtu kuondoka au akaendelea kubaki. Hapo sasa ndio utaona umepata rafiki labda ni mwanamke au mwanaume akawa anakupa company sana kwa hali uliyonayo kwa muda Fulani (hata mwaka mzima. Unajikuta umekua attached sana na mtu huyo then inafika muda bila sababu yoyote ile ya msingi unaona mawasiliano na urafiki unapungua taratibu then unaisha kabisa. Hapo nature inakua ishafanya yake..

Nachotaka kusema ni kwamba watu ambao mpo kwenye mahusiano jifunzeni kusoa alama za nyakati, so unaona hapa mapenzi au urafiki unaanza kuisha ila wewe ndio bado unazidi kuongeza kupiga simu na kumfuata ili aendelee kubaki…Kijana kila kitu kinakuja kwa muda na sababu Fulani, hutakiwi kutumia nguvu kubwa kumfanya mtu aendelee kubaki kwenye maisha yako. Mtu kama ni muhimu kwenye maisha yako atakuja mwenyewe na kukaa nawe daima, huna haja ya kulazimisha.

Kwanini ulazimishe mahusiano? Watu wote hawa waliojaa duniani au unadhani yeye ndio bora pekee kuliko wote, mwache aende labda alikua sio riziki ya maisha yako! Utapata mwingine. Kikubwa zaidi ambacho hutakiwi kukifanya maishani mwako ni kupuuzia ubaya wa mtu anaokufanyia kwakua unahitaji mtu huyo aendelee kubaki maishani mwako, train your mind to be stronger than your feelings.

Kingine maishani mwako usionyeshe wema au uzuri wako ili uwafanye wavutiwe nawe, waonyeshe ule upande wako ambao ni mbaya uone kama watakuvumilia au wataondoka. Wakiondoka usijali jua ni watu fake. Be real that’s beautiful enogh kijana.
Mwaka mpya,misimamo mipya..Uliumbwa mwenyewe! Huyo mpenzi au rafiki yako umpendae sana ambae unaona huwezi fanya kitu bila yeye ni wa kupita tu.

Hamishia nguvu zote kwa mama yako ndio the best one ambae hatakuja kukusaliti. Jiamini katika uwezowako, unaweza kufanya makubwa bila mpenzi wako huyo ambae unaona huwezi fanya kitu kikafanikiwa bila yeye.If you Doubt your power, you power your doubt.

Binafsi hua sijali wala kujutia chochote maishani mwangu, ukinipenda Ahsante na karibu, ukiondoka hamna shida pia.. you weren't meant to stay in my life, if you were! You will stay in my life forever
A guy has said, It’s up to you To choose me or to loose coz I’m not a second choice
With or Without you, I shine!

Vers
Safi sana [emoji870]
 
Nikupe pole sana..ukweli ni kwamba kuna wakati hata uwe gaidi kivipi.. there's a point of no turning back. Yaani lazima ushikike tu maana everyone need to belong to someone..who Love
Pole sana je una mpango wa kutafuta mbinu za kumpoteza
Nshajaribu several times lakin hataki kuondoka na i feel guilt kumfukuza kwa force maana we have beeen close kwa kwel hata ushauri wa kimaisha ananipea sana, sijui hata nifanyeje ( hajui kama nawaza juu ya haya mahusiano yetu, anaona tu namchukulia poa, namdharau etc
 
Kwanini unataka mtengane
 
Maisha haya we acha tu!nilidumu nae kwa muda wa mwaka mmoja kwenye mahusiano,nikagundua hana sifa ya kuwa mke!anakunywa pombe wakati mimi sijawahi ,anapenda kutoka lkn mimi ni mtu wa home tu,muongeaji sana wakati mimi mkimya,lkn alijaribu kuendana na lifestyle yangu lkn haikuwa ndani yake ilikuwa just kufake tu!niliamua kumuacha ila kila niki move on nashindwa kufurahia mahusiano mapya!japo ni tabia zake mbaya natamani nirudi tena!yaani moto unauona ule pale!lkn moyo unakwambia nenda tu hivyo hivyo [emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom