Je, ulishawahi kushuka na begi/mzigo wa abiria mwenzio kwa bahati mbaya? Mtu aliyeshuka na box langu la samaki mwaka 2012 sasa ni family friend

Je, ulishawahi kushuka na begi/mzigo wa abiria mwenzio kwa bahati mbaya? Mtu aliyeshuka na box langu la samaki mwaka 2012 sasa ni family friend

Kuna siku Songea tumekesha bar Planet sijui bado ipo! asubuhi nikaunganisha na superfeo hadi Njombe. Wakati natoa bag nikachukua ambalo sio langu, nikapanda bus za kwenda Ludewa.
Kufika milima ya gangitoroli nikapokea simu kuwa tumechanganyana mabag, mwenye langu kaliweka ofisi za superfeo kwa hiyo nitalikuta pale.
Mkuu, hivi hawa superfeo na zile buses za BM za Morogoro ni za mtu mmoja?...
 
Ndio. Nilikua nimetulia kuona mwisho wao. Tulikua tunapata habari mbalimbali za wizi na utapeli wa bongo. Kwahiyo mimi nilikua tayari kujipanga mapema. Wangeondoka na begi langu. Na mimi ningeondoka nao. Bila kupiga kelele. Kwanza nilijiona kazi yangu ingekua nyepesi....
Bila shaka upo njema sana katika judo na karate boss
 
Niliingia kanisani kusali nikaweka baskeli nje ila nilisahau kuifunga baada ya sala kumaliza kutoka nje naiona baiskeli ipo na nikashangaa sana haikuibiwa maana ni nilisahau kuifunga ,basi nikaamua kurrudi kanisani kwenda kushukuru kwa mungu kwa kuikuta basikeli yangu ipo salama, wandugu kutoka baiskeli haipo, ,.
 
Daaah noma sana mkuu...
 
Kuna siku Songea tumekesha bar Planet sijui bado ipo! Asubuhi nikaunganisha na superfeo hadi Njombe. Wakati natoa bag nikachukua ambalo sio langu, nikapanda bus za kwenda Ludewa.
Kufika milima ya gangitoroli nikapokea simu kuwa tumechanganyana mabag, mwenye langu kaliweka ofisi za superfeo kwa hiyo nitalikuta pale.
Nilivyofika kituo cha nyumbani nikaliacha tu stand kwa jamaa then nyumbani nikaenda kama le baharia yaani sina kitu mkononi hata peni.
Siku ya pili nikalipitia na kwenda kubadilishana Njombe.
Planet ipo mkuu na boss ni yule yule mchaga mzee msalanga ila yule mama wa counter maarufu mama dave mungu kampenda zaidi
 
Planet ipo mkuu na boss ni yule yule mchaga mzee msalanga ila yule mama wa counter maarufu mama dave mungu kampenda zaidi
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
Bambu uvii kuperemihu ndee penyeapo? Wangoni wamenishinda tabia
 
Mwaka 2016 haraka haraka na furaha ya kufika home salama,nikabeba begi la mdosi pale Jnia,nafika home nafungua nakutana na tambuu na zagazaga zingine za kidosi Duu nikapagawa mbaya,begi langu lilikuwa na mazaga yangu kibao na zawadi za madogo!....fasta nikarudi airport nikalikuta begi langu pale lost and found kwa Swissport....kumbe mdosi alivyoona begi sio lake akaliacha pale....kwa mazaga yale ingekuwa mbongo mhh sijui....
 
Mimi katika harakati zangu. Nilitoka Unguja kufika bara. Kushuka kwenye boti pale bandarini. Vijana wa Azam wameniambia mizigo yote unayifwata mbele ya mlango wa kuelekea Custama. Mie nimetii naelekea sehemu iliomwaga mizigo ya abiria... Vijana wa pale bandarini wanachagamkia kugombania mizigo ya kubeba. Vijana wawili wamejitokeza wamechagua begi langu. Moja kati yao amesema ndo hilo livute. Na mimi nimenyamaza nawangalia kwa jicho la huruma ila aliekuja kuharibu shoo yote ndo ule niliefwatana nae.

Kusema kusema Sheikh begi lako si ndo hilo vijana yanaolinyanyua? Nilimwambia ndio ila ananiletea hapa. Ghafla abiria yote wameshangaa. Kwa upole nilionyesha na bila kubishana nao wale vijana. Niliwambia nimenyamaza kusudi ili nijue mwisho wa mchezo wenu? Ili mkichezecha begi langu rafu. Na mimi niwapoteze kimya kimya huko baharini.

Kwamba Ulitaka kufanya umafia kimya kimya hahahahah!
 
Niliingia kanisani kusali nikaweka baskeli nje ila nilisahau kuifunga baada ya sala kumaliza kutoka nje naiona baiskeli ipo na nikashangaa sana haikuibiwa maana ni nilisahau kuifunga ,basi nikaamua kurrudi kanisani kwenda kushukuru kwa mungu kwa kuikuta basikeli yangu ipo salama, wandugu kutoka baiskeli haipo, ,.
Ilienda wap mkuu
 
Kumbe wewe jamaa ni mjaluo, kabila lenu nalikubali kinouma pia inanikumbusha maisha ya uvuvi miaka hiyo sota na shirati
 
Huko mbeya miaka ya nyuma kabla Bujibuji hajazaliwa kuna abiria alitamani box lilikuwa kwenye carrier ya ndani gari imetoka swanga linaenda tukuyu.

Jamaa akashuka mwanjelwa na box alililitamani.

Mbele kidogo mwenye box ana note kuwa mzigo umeshashuka. Kuuliza akaambiwa box limeshuka mwanjelwa. Akasema ndani mna mwili wa mtoto mchanga, alitumia mbinu tu ili kurahisisha usafirishaji.

Kilichotokea mbeba box alifika huko vichochoroni kufungua ohooo, ikabidi arudi stend ,

Mwisho walikuja kukutana na kumkabidhi mwenye mwili wake.

Be careful siyo kila zigo la kubeba mingine siyo.
 
Huko mbeya miaka ya nyuma kabla @Bujibuji hajazaliwa kuna abiria alitamani box lilikuwa kwenye carrier ya ndani gari imetoka swanga linaenda tukuyu.

Jamaa akashuka mwanjelwa na box alililitamani.

Mbele kidogo mwenye box ana note kuwa mzigo umeshashuka. Kuuliza akaambiwa box limeshuka mwanjelwa. Akasema ndani mna mwili wa mtoto mchanga
Mwili wa mtoto mchanga ndani ya box? Doooh sio mchezo hata kidogo...
 
Back
Top Bottom