Sakwe
Member
- Jul 31, 2022
- 46
- 300
Mimi nilikutana na matangazo haya ya ajira kwenye nguzo za umeme bhn mshahara 410k. Nikapiga simu, wakaniambia niende kwenye interview kesho yake pale Chang'ombe Junction saa 12 asubuhi na niwe smart sana, wakaniasa.
Kesho yake, kama kawaida, nikaenda kutimba pale Chang'ombe. Nikampigia jamaa, akanipa maelekezo hadi nikafika pale. Mmmh, nikaanza kupata wasiwasi tu kwa muonekano wa ofisi ile. Kuangalia kushoto, naona watu wamejipanga mstarini—yaani ni kama parade hivi! Daah!
Nikakaza moyo, nikaulizia alipo huyo jamaa maana aliniambia nikimuulizia tu nitaelekezwa alipo. Basi, kufika kule, jamaa akaniambia nitafanya interview kwa njia tatu tofauti: Oral (maswali ya mdomo), darasani kwa maandishi, na kwa vitendo. Nikajibu, "Sawa, hamna shida kiongozi."
Oral tukaanza. Mara wakaitwa wengine watano na mimi, tukawa sita. Anauliza swali, unanyoosha mkono ukiwa unajua jibu, anayejibu anapewa maksi.
Swali la kwanza likawa: "Unatakiwa kufika kazini saa ngapi?"
Nikajiuliza, "Mtu ndo nimekuja, wananiuliza muda wa kuja kazini kweli?" Kusikia sauti, "Saa 2! Saa 2!" Nikageuka, kuna mdada nilimuona ananinong’oneza kimoyomoyo. Nikasema, "Kama anajua, si anyooshe mkono ajibu jamaa?" Ila hakuna aliyejaribu kufanya hivyo kati ya wale ili tusionekane wote viazi.
Mimi nikanyoosha mkono, nikajibu, "Saa 2, kiongozi." Akasema, "Safi safi!" Wale wenzangu wakaanza...
Itaendelea: 2