Je, uliwahi kuwa maarufu shuleni?

Je, uliwahi kuwa maarufu shuleni?

mi nakumbuka shuleni nilikuwa bright mno alafu mi ndo nilikuwa navaa viatu peke yangu 1992 PRIMARY. hahaha dah, sasa pia nilikuwa mtu wa kusikiliza sana redio hasa dunia yetu leo mchana na DW, BBC SWAHILI NA SAUTI YA AMERIKA, habari zote muhimu wanafunzi walizipata kwangu hata baadhi ya walimu kwenye mikutano mbali mbali nikawa naitwa kuelezea kwa fact nini kinaendelea Huko duniani,
Nilipata umaarufu sana nilipoanza kuchambua masuala ya vita ya kimataifa YEMEN, YUGOSLAVIA, na wengine wengi,
Mzee wangu alikuwa na library moja balaa magazeti yoote yapo, hata yale ya Scientific america na National Geographic yanayotoka kila mwaka alikuwa nayo ya mwaka 1961 hadi 1998 humo kumesheheni nondo, mambo ya sayansi , geography , magalaxy ma big bang, na kila kitu niliyasoma na kuwaeleza wengine kama story,

Nilikuwa najua sana hesabu hiyo mpaka chuo kikuu nilikuwa kipanga mnoooo,

ISHU MOJA AMBAYO INANISHANGAZA ILIKUWA NIKIANZISHA KUONGELEA JAMBO MPAKA WATU WOTE WAKUSANYIKE KUNISIKILIZA MBAYA ZAID NA NINAO WAZIDI UMRI, NIKAPATA JINA LA ENCYCLOPEDIA BRITANNICA
 
Primary : nilikuwa nawakimbiza, kuanzia darasa la tano hadi la saba ni moja tu.

O level nilikuwa niponipo tu, nikakutana na vipanga zaidi ndo nikajua kuwa nilikuwa nakuwa wa kwanza kwa wajinga. ila nilikuwa napendwa sana na totoz. Nyota yangu kwa totoz iling'aa sana o level.

A level, nilikuwa nipo kama sipo

Chuoni ndo kabisaaaaaa kila mtu na maishs yake.
 
Nakumbuka nilikuwa najulikana kwasababu ya muonekano wangu unique, mrefu mweupe etc.
Kingine darasani nilikuwa nafaulu alafu general knowledge yangu ni kubwa kwahiyo vitu karibia vyote nilikuwa navijua.
Pia nilikuwa najua kingereza balaa na hizi speech sijui madebate nilikuwa sikosekani.
 
Kusema kweli wakati niko shule was the best days of my life, kwanza nlikua niko vzr darasani, nlikua sijui namba mbili ikoje mm moja tu hadi namaliza, cha pili nlikua maarufu kwa ajili ya mpira, nlikua nakichafua kweli kweli, nlinusurika kwenda zile academy za mpira but mzee wangu akasema ntolee ujinga hapa soma.
Cha tatu Walimu na wanafunzi walikua wananikubali sana yaani I was a Typical superstar back then, and kiukweli I really appreciated that.
Baada ya hapo sasa yakaja maisha yenyewe, haya kila mtu anayajua the hustle ni kila siku ukizubaa tu u going down. By the way ahsante kwa uzi umenkumbusha mbali. #onelove.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom