Je, uliwahi kuwa maarufu shuleni?

Je, uliwahi kuwa maarufu shuleni?

hahahaha..! nilikuwa mpiga kelele maarufu, kila mkiitwa hata kama nililala utasikia teacher "panya mabaka, njoo hapa, lala chini" yani nakula za maana alaf wengine wanaachwa! dah, shule hizi..

Kuna maticha walikuja BTP tuko Std 5, wiki ya kwanza tu nikajulikana ndo mpiga kelele, nikapelekwa staff nikalambishwa fimbo. Wakati hiyo batch inaondoka wanakabidhiana na wanaokuja eti wanasema mimi ndo mpiga kelele, mpaka batch nne zinaisha walikuwa wanapokezana kunitaja na kila batch ilikuwa ni lazima nidakwe kwa kelele.

Ikaja kwenye pepa, maana walitunga pamoja, tukafanya nikawa wa kwanza wakakataa kunipa zawadi, mpaka mwalimu wa darasa anawaambia mpeni tu, ndivyo alivyo.
 
Primary nlikuwa mkali wa soccer, kuna mechi moja ilinipa umaarufu sanaaa,, walimu wote walinijulia hapo. Niliweka kambani goli mbili, mpira ukaisha kwa ushindi, mambo ya ujirani mwema,, hadi shule jiran nikawa maarufu,,

Secondary ivo ivo ila nikakutana na wenye kuujua mpia wenzangu ivo sikubamba sanaa,, "K" ndo zilinilostisha aiseeeh,, ila nlitoboa

High school, nlitundika daruga, nikawa bize na book,,

Chuo mahaba niue yakanishika na mtoto mmoja matata dahhh,



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Actually siwezi sema maarufu sana ili nisipokuwepo watu wanajua sipo.Primary nilikua very smart na naongoza lakwanza hadi la tano.Kuendelea hapo mambo yakawa meng mda mchache.Pili nilikua naletwa na gari na kuja kuchukuliwa kila siku enzi hizo mzee anamiliki pijoti na suzuki.Nilikua ka handsome flani hivi videm vinanikubali laana.kuna mtoto mkali sana enzi hizo wa kikenya ananizimia balaa na yeye kwao wako vizuri sana kifedha.Cha kushangaza sijui kutongoza na nawaogopa wanawake vibaya mno.Nikawa maarufu zaidi kwa skendo ya udomo zege.

Olevel hapo ndio nilivurugika zaid.mzee kafilisika na nimeshazoea pesa.Hapo ndio nilikua maarufu sana sana kwa uvaaji wangu na manukato.Pili kipanga wa madem balaa.Kwa utoro ndo usiseme kwa week naingia darasani mara 2 ama 3 na sikai mpaka mwisho wa vipindi.Pia nilikua mchezaj mzuri wa mpira wa kikapu.Pia nilikua mchezaji mzuri wa muziki staili ya kuvunjikavunjika.Namiliki simu utaniambia nini.
Mwandaaji wà safari za pikiniki.wacheza kareti ndio sisi,ugomvi ndio sisi,bangi na mimi.Enzi hizo tuna rap rap yaani ni balaa tu la ujana.
Ulizia sasa matokeo yangu.....
Edmund rice 2002++++ watakua wananikumbuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wale wa ENABOISHU SEC sidhani kama kuna mwl. hamjui Freemason mimi,maskini ya mungu wazazi wetu walitudekeza unapewa pocket money kila wiki,Huko shule n mwendo wa Kufanya FUJO tu.

Namimi kuona naitwa FREEMASON ndio nikakoleza na kuvaa mikanda yenye bacon za mafuvu japo haikua ikiruhusiwa ila hamna mwalimu alithubutu niambia niutoe wakiamini eti kweli mimi FREEMASON.

Yule freemason saiv wakinikuta na kandambili zangu na jasho la mwendo kasi hawaelewi elewi..wengine bado wanahisi naigiza.

wakat mwingine natamanigi kurudi enzi zile...Unanunulia SODA wanafunzi DOM zima...asubuhi uji unanunulia BOYS wote half cake shenz type DON nani zaidi yangu banaaaaa.

Hilo tranka langu sasa...bwana eeeeh hatari mnoooo
 
Darasani masomo yote hunioni ila chemistry O level walikua wananielewa...walikua wananiita mwalimu WAO ... ntafute saivi niulize what is chemistry?
 
Tunapita kimya. Kuna vitu vingine unaweza kukosa,mchumba bure..bora tu upige kimya
Humu kila mtu alikua namba moja (john kisomo)?
Ina mana wale tuliokuwa tunakamata mkia kama mimi humu hawamo?

Kila mtu kaenda chuo?wa la saba na form four hapa hawapo ehee??

Wale wa di nne za kuunga unga hawapo???

Wale wa ziro kama mimi hawapo???

Wale wa veta na setifiketi hawapo????

Duuuh!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Humu kila mtu alikua namba moja (john kisomo)?
Ina mana wale tuliokuwa tunakamata mkia kama mimi humu hawamo?

Kila mtu kaenda chuo?wa la saba na form four hapa hawapo ehee??

Wale wa di nne za kuunga unga hawapo???

Wale wa ziro kama mimi hawapo???

Wale wa veta na setifiketi hawapo????

Duuuh!!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Winners write history...!

Kila mmoja anaandika kile anachoona ni cha kukumbuka, kwa nini niweke habari ambazo hata mimi nikizikumbuka nafadhaika?
 
Back
Top Bottom