Huyo jamaa anafaa sana kuishi na mimi. Kuna siku moja night kali sana around nane kuelekea tisa nilishtuka usingizini kwa makelele ya paka nahisi walikua zaidi ya wanne. Sauti ingine nikawa naisikia inatoka ndani sebuleni, nikanyata mdogo mdogo nikawasha taa pap!!
Mara naona paka kubwa jeusi linanikodolea macho moyoni nikasema usintanie hunijui nikarudi room nikachukua rungu huku nawaza hili paka limepitia wapi mbona madirisha yote yamefungwa (ni haya ya aluminium) aisee nimerudi nakuta paka anahangaika dirishani atoke nikasema leo nakuua. Kwanza nirusha lile rungu likatua mgongoni.
Paka likatoa mlio flani kama linafoka hivi likahamia dirisha lingine mie nnalo tu sasa safari hii nlipiga sikurusha rungu.. paka likawa kama limezimia basi nikalishika nikafungua dirisha nikalitupa nje kwa kulirusha likaenda jipigiza kwenye uzio nikasema nishau paka la watu. Asubuhi naenda pale nilipolirusha, hata dalili ya paka sikuona nikasema duh! Hii hatari
Ni hivi mie hua siogopi mauza uza binadamu ninaweza kumuogopa akinijia hiyo Mida ya wanga ila sjui paka sjui bundi ndo siogopi kabisaaa. Ila mpaka kesho sijajua yule paka aliingia vipi ilihali hakukua na sehemu ya kuingilia