Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa JF katika maisha ya uhalisia (Jamii)?

Wa kwanza nilikuwa naye kwenye mahusiano baadae tukaja juana wote ni members wa Jf mpaka leo tunazoomiana kwa mbali tuu.

Wa pili ndugu mmoja alikuwa anapangisha chumba chake na kuuza vitu ya ndani alikuwa anaenda nchi za nje nikaenda kuangalia nyumba nadhani yupo nje ni kitambo sasa.
 
nitakutana nao soon ndipo nitapata fursa nzuri zaidi ya kueleza walivyo na tumezungumza nini 🐒
 
Mtu kuijua ID yako wakati unaperuzi siyo rahisi kwa sababu unakuwa una-scroll randomly ataijua pale ume-reply au ume-post kwenye uzi au jukwaa husika na awe makini kweli kweli kukufuatilia.

Mimi simu yangu hashiki mtu zaidi ya wife maana najijua mzito ku-log out kwenye mitandao Jamiiforums ikiwemo.
 
Nimekutana wa watu wawili wote ni watu wa maana kabisa Mungu azidi kuwabariki nyie watu.
Wengine tulipanga kuonana ila ikifika siku ya kuonana anasema Kuna kijana wangu nimemuagiza utaonana naye..na kweli naona naye Sasa sijui ni spin au vipi.!! Ila ni watu wa maana sana
 
Nilikutana mwaka 2008 au na 2009 hivi na yule bingwa wa it alikuwa memba wa jf aliyekuja kujiua baadaye. Sijui baadae nae alianzisha forum yake. Id yake kidogo imenitoka. Nilijitambulisha kwake kuwa ni mtumiaji pia wa jf na tulikuwa na maongezi mazuri. Ilikuwa ni kwa bahati tu aliona nikibrowse mada za jf kwenye simu akawa wa kwanza yeye kujitambulisha.
 
Alijiua kwa sababu gani mkuu
 
Alijiua kwa sababu gani mkuu
Mambo ya ndoa, mkewe alikuwa nyanda za juu kusini huko sijui ndio kisa kilianzia huko. Uzi wake wa msiba umo humu jf ila siukumbuki title yake, unaweza utafuta unaelezea mkasa wake. Nilisikitika sana kwa kifo chake ukizingatia ni mtu niliyekwisha muona ana kwa ana. I think id yake ilikuwa shayo ama shio, sina uhakika bado jina limenitoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…