du zamani dzm tuliwatania wale kule kusini wanaokula 'samaki nchanga' na ule mkoa ulojulikana kula mbwa... nilitahadhari kununua mishkaki mikoani humo nikisafiri ...
🤔sasa nahisi kula mishkaki safarini ni mtihani
manake, du sasa hii mada inaonesha hakuna mnyama ama mdudu asieliwa ... sijui tumeiga wachina ama kweli ni asili yetu???
ILA wanaJamii, tahadhari kuna wanyama wanaobeba magonjwa sugu yasiowadhuru ila yanatudhuru. Niliwahi soma kuhusu nguruwe kuwa na vidudu ambavo hata uchemshe nyama siku nzima havifi na vinaleta magonjwa hata saratani... tafiti kwanza kabla ya kubugia
Miiko ya kiasili na hata ya kidini ilikuwa na maana nzuri kiafya... tuache kulaumu dini. Ukila mnyama anaekula nyama mbichi ya mizoga ilozongwa na mainzi ... kweli unategemea nyama yake haitakuwa na madhara?
Hata haya makuku sijui yanaitwa chotara, paja kama mbuni .... sidhani ni bora kiafya kwa sababu yanakuzwa si kiasili bali kwa madawa