Je, umewahi kula mnyama ama wadudu gani Hadi ukajisemea nilikuwa wapi siku zote hizo? Nimekula wanyama wengi sana.

Je, umewahi kula mnyama ama wadudu gani Hadi ukajisemea nilikuwa wapi siku zote hizo? Nimekula wanyama wengi sana.

Kuna yale ma kenge makubwa nimetoka kula limoja juzi juzi lilikua linavizia mayai ya kuku wangu hapa nikapita nalo likawa kitoweo.
Asee mnanitamanisha sana nifundishe namna ya kumuandaa asee mambo yasiwe mengi huku wapo TU hata jioni hii nikidinda napata TU hapo bwawan
 
Hao nimewala Dar Kwa jina la dagaa kamba SI ndio?
Umeangalia hiyo video? ... ngisi sio dagaa kamba! ... anafanana, kwa mbali, na pweza!
Akikaangwa ...:
1784380398752.png
 
Asee mnanitamanisha sana nifundishe namna ya kumuandaa asee mambo yasiwe mengi huku wapo TU hata jioni hii nikidinda napata TU hapo bwawan
Huyo Hana mambo mengi unamkata kichwa unamlaza analalia mgongo unapitisha kisu kuanzia shingoni mpaka mkiani kisu kinaangalia juu kisha unaivua ngozi Kama kati tu.

Baada ya hapo toa matumbo unabaki na nyama safi unaweza kuitia viungo kidogo Kisha ukaipika au kuichoma pia ni nzuri zaidi ukikaanga na mafuta (dip fry)

Mboga tayari
 
Katika kuishi kwangu porini muda mrefu, nilijikuta nafakamia wadudu na wanyama wa kila aina.
Nimekula kobe, kenge, nguchiro, kima, mbega, ndezi, kuhe, nungunungu etc.
Kuna sehemu niliishi nikaamua kufuga kuku. Kuna hawa wanyama waharibifu wakaanzisha bifu na mimi kwa kunichukulia kuku wangu; kicheche, suzi na pakapori. Ilibidi nianze kusuka mipango ya kuwawinda kwa mitego na wote niliishia kuwanasa na sikuwa na ajizi zaidi ya kuwatengeneza ndafu na kaugali kwa mbaaali!

Katika nyama zote niliinjoi sana siku nilipokuwa nyama ya kiboko! Ni tamu balaa huyo kasongo na noa wakasome!
Aiseee 🙌🙌😄
 
Back
Top Bottom