hearly
JF-Expert Member
- Jun 19, 2014
- 54,381
- 80,393
😄Wewe china huwezi ishi abadani. Unaambiwa china kisicholiwa ni sauti tu vingine vyote kama kawaida
😄Wewe china huwezi ishi abadani. Unaambiwa china kisicholiwa ni sauti tu vingine vyote kama kawaida
😄😄🙌🙌Paka ni mtamu ila ukutane na wanaojua kumuuandaa bila hivyo utaoshia kusema nyama ni chungu
SioHao nimewala Dar Kwa jina la dagaa kamba SI ndio?
Eti na fisi..!!🤣🤣🤣Chui!!! Are you serious
Mtu yeyote anayekula vitu wanyama au wadudu waliotajwa kwenye hii thread binaadamu anamla pia ni vile tu hajapata hiyo fursaMtu anayekula nyani na jamii zake basi hashindwi kula binadamu
Ni kweli mkuu. Nakumbuka hata siku tunakula kenge, jamaa mmoja akatutisha kwamba tusitafune mifupa yake ikikuchoma mwili unatutumuka!Kuna wanyama ukila nyama yake ni sumu..
Unazungumziaje hilo
Nswa, loh utakua ntu ya tabora shehe...Senene na nswa
Utakuwa na harufu ya mwili ya asili mbaya sana. Unakula vitu vya ajabuKuishi kwingi kuona mengi wakuu.
Habari za Leo ninyi nyote wakuu!
Ninaudhoefu kadhaa wa kuishi porini kulingana na kupenda Nature ama kuwa na Hobby ya kilimo na kufuga.
Nimeishi maporini Kwa nyakati tofauti tofauti na kukuta jamii zikila wanyama ambao kikwetu ni mwiko na hawaliwi ila jamii hiyo ndo unakuta chakula chao au ni mboga Yao pendwa!
Kanda ya ziwa ni ngumu kukuta watu wanakula.
Panya
Bundi
Mwewe
Kipanga
Fisi
Chui
Nyani
Ndezi
Funza wa kwenye magogo ya miti nk.
Hao ni ngumu na sikuwahi kuona tangu kukua kwangu.
Lakini Kwa mara ya kwanza nikiwa pwani nilishuhudia Nyani analika vizuri TU na watu jamii ya malila kutoka mbeya huko na waluguru kama sio wapogoro
Ni nusura TU nile nyani Kwa mpogoro kama sio mluguru bahati yangu nilikuwa na msukuma akanikataza Kwa kisuma Kisha nikaona kiganja Cha nyani wao walikuwa wanamuita abdalah kapotea.
Hapo alikuwa amebanikwa vizuri kwenye moto wa nje uroho ukaniingia na vile Kwa mtani wetu nikataka kujipimia kumbe nyani bana.
Nikiwa huko nilishuhudia panya wakubwa wanaliwa vyema TU wengine waliitwa ndezi hii ni mto Ruvu kulikuwa na makabila tofauti wakiwamo na wazaramo wenyeji wetu.
Pamoja na yote hayo sikula hao wanyama.
Sasa nimeenda mahali pengine tena nikakutana na wafipa na wabende nk asee wanafukia vitu vya ajabu sana na ikanifanya sasa nami nitest mitambo wanyama niliokula na kuona ni watamu TU na hawana shida labda shida uwe nayo wewe mwenyewe ni
Ndezi
Mwewe wakubwa kabisa wale wenye uwezo wa kubeba hata mtoto wa mbuzi
Chui
Mbawala
Nungunungu
Kasogo yeye
Nguruwe pori
Kuna mnyama fln jina limenitoka wale huchimba mashimo Kwa Kasi sana .
Hawa wanyama watamu sana.
Ajabu ni bawala hana mafuta hata Tone Moja yaani ni mnyama asiyechosha kumla lakini ndo hivyo hana mafuta kabisa kabisa pamoja na kuwa amenawili vyema!
Naangalia namna nipate mtu wa kumuandaa chatu vizuri naye ni mle TU kesi iishe.
Hao ni baadhi TU ya wanyama niliokula ambao kwetu hawaliwi
Labda Hawa ndo Kwa uchache huliwa huko kwetu
Nguruwe pori(kwanza hawako)
Ngiri hawapo pia
Nungunungu wapi wakubahatisha walaji ni wachache mno
Mbawala wapi ila SI Kwa wingi ..hasa shida kubwa ni koo mfano ukoo wetu ni mwiko kumla pasina sababu yoyote ya maana Mimi nimemla na Niko vizuri TU.
Wewe umewahi kula nini ambachi kwenu ama jamii yenu haili kabisa?View attachment 3631650
Matini hayakai kichuguuni, hua yanakua sehemu ya kawaida kabisa mkuuKuna wale wanaitwa MATINI unawafahamu wanakaa kwenye vichuguu wanan'gata sana
Watamu hao niliwalaga Tabora
Niliwahi kuzila nikiwa India (pumbu za mbuzi) ni tamu sana.Ni meupe mkuu damu kidogo mno unaweza Kuta hata mils10 haifikiView attachment 3631824hata mboo nayo huliwa vilevile
Watu ni walafi aiseeee!Kuna hii nyingine sijui ni uroho au kutaka kuingia kwenye kitabu cha guiness!
Wajita wanakula wadudu flani wadogo wadogo jamii ya mbu. Wenyewe wanaita masami.
Ukamataji wake ni kipengele. Wanachukua kalai wanalilowanisha maji kisha wanaanza kupunga hewani kipindi hao wadudu wanapaa!
Na kuna kabila moja wanaitwa Wanguu-Wajumbi, wao wanakula wadudu flani jamii ya "dudu washa" ila shariti wapatikane kwenye miti ya mikarati.
Funga kazi ni Waluguru, wao hula panzi flani wazubaifu/mazoba wanaitwa ngeda au mbulumundu. Wanakuwa wa kijani. Hupatikana kwa wingi kipindi cha masika wanapenda kutembea kundi au wawili wawili. Hawawezi kupaa na mara zote utawakuta njiani wamezubaa.
Usukumani wanaitwa "kafula"
Wamakonde salute kwenu. Mnakula konokono wale wenye utelezi. Wenyewe hujisifia eti wana nyama nzuri kama firigisi ya kuku!
Matunda gani hayo mkuuNimekutana na matunda ambayo sikuwahi fikiria yapo duniani na yanaliwa!
Nimekaa porini kuanzia mwezi wa2 Hadi huu wa saba bila kuona mtu anaumwa Wala kusikia fln anaumwa labda usikie kachomwa kisiki.
Mimi mwenyewe nimeugua kuharisha baada kunywa maziwa yaliyochacha😂😂