Je, umewahi kula mnyama ama wadudu gani Hadi ukajisemea nilikuwa wapi siku zote hizo? Nimekula wanyama wengi sana.

Nakubali mkuu makonde Wana mitego wanweza kunasa Hadi bindamu maana wanamitego huwezi kuuona Kwa macho Abadan ila yeye mtegaji TU. Nimeisha na mmakonde porini alikuwa akipotea kama masaa2-3 ana kuja na nyama kashamaliza na kuichoma anakula kauli yake ni Moja jamani anayetka kula aje tule...habari za mnyama Gani huyu hakuambi😹😹
 
Niliwahi kuzila nikiwa India (pumbu za mbuzi) ni tamu sana.
Wenyewe wanaita KALEJI.
Huwa zinauzwa mitaani kama mishikaki.
Sisi hii ni mara nyingi TU haihesabiki hata wiki hii tunaenda kuhasi Kwa mfugaji ameniomba nikamfanyie hivyo na sharti nibebe au nile hapohapo matamu sana full steki
 
Wale panzi sio tondogoso kweli?
 
Yule ndezi hana tofauti na panya kimuonekano. Ndiyo maana Kizungu anaitwa cane rat, au grass-cutter. Africa magharibi wanafunga na kuuza.
Nyama yake tamu sana. Nimekuja kumla Mara ya kwanza mkoa wa Pwani miaka miwili iliyopita.
 
Yule ndezi hana tofauti na panya kimuonekano. Ndiyo maana Kizungu anaitwa cane rat, au cane cutter. Africa magharibi wanafunga na kuuza.
Nyama yake tamu sana. Nimekuja kumla Mara ya kwanza mkoa wa Pwani miaka miwili iliyopita.
Huku kiangazi hiki wanaliwa vizuri TU hawana baya kabisa.
 
Nimejifunza kaka 😊
 
Kobe wa majini anakunya funza kabisa mkuu mliwezaje
Hahahaaa!
Wanaokunya funza ni wale kobe jamii ya wadogo wadogo.
Wapo wale wakubwa wanafikia size ya kalai weusi hivi, hawa wapo safi kabisa kwa mlo!
Nakumbuka siku madogo wanamchangua yule kobe alikuwa jike so akawa na mayai kibao makubwa kwa madogo. Mi nikaanza nayo kwanza yale kwa kuyakaanga kisha nikala!

Najua inastaajabisha!
Ila ndo hivyo kuna wengine sie tumezoea adventure na kuexperience mambo ya ajabu ajabu basi tu yaani!
 
Ewaaa! Swadakta wanaitwa tondogoso huko usukumani!
Sasa mkuu imagine mtu anakula yale makitu!
Na unaambiwa uandaaji wake unatakiwa upasue kifua utoe kuna utando flani wa majimaji ni sumu na mchungu balaa!
Usipo utoa utahara hadi utumbo utoke nje!
Wale wananuka mbaya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…