A woman is just a woman, yaan hata kama ana jinsia tatu as long as ni mwanamke nafasi yake hua anaicheza vizuri.
Growing up nilikua na rafiki ambae alikua na hormone nyingi ya kiume, sisi tulikua family friend kwao. Nguo za kike alikua havai hata umwambie utamuua, Shuleni ilibidi avae bukta, alikua anapenda michezo ya kiume haswa Kupigana.. tuko std 4 alikua anatembea kifua wazi vifungo kachaniwa kwenye ngumi wakishona anatafuna, primary alivaa hijab siku ya Necta.. tulivyo fika sec aliendelea kuvaa hijab ila muda mwingi ushungi anavua anabaki na shati la mikono mirefu na suruali.
Form 3 alikutana na kamwamba flani ivi kako feminine kiasi, sura ya Mama.. sijui urafiki wao ulianzia wapi ila they ended up dating.. Sikuwahi kumsikia akinukia hata lotion ila baada ya kukutana na kale ka mwamba akaanza kuiba Casablanca za mamaake.. mwanzoni bimkubwa alishtuka ila baadae akaanza kununua vipodozi viwili viwili ili akibeba kimoja kingine kinabaki,mamake alikua anampa stori maza nikiwa around.. ulikua muujiza
Alikua na kifua flat, sura ya kawaida ila haiba ya kiume kiasi, aloo! Siku puberty ilivyokuja kumtembelea tulijilaumu mazee.. she had feminine masculine body, tumbo six packz zinaonekana ila hipsi zimetunza mafuta, kifua flat kikawa na vifuu vya nazi. Uso wa kike ukachomoza ngozi ikanawiri ikiwa na vinyweleo vya kiume laini alafu vingi kiasi.. ukichanganya na vipodozi vya bei vya mama ake hadi walimu walianza kumsumbua. Form four then six, mpka sasa Ye na mume wake wako wizara ya Afya ila Mwamba Ana karama ya Uinjilisti pia.. watoto ndo hawajafanikiwa mpaka sasa nahisi ni ile ishu ya hormone kwa Dada angu yule!!