Boeing 747
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 3,515
- 9,415
- Thread starter
- #41
Hahaaa..[emoji851][emoji851] Jamaa ameweka ligi kweli..Mkuu unabishana na watu pengine hata hayo magari ya Nisan au Toyota hawana hivi plugs zipi ambazo ni imara na nzuri kati ya zilizoundwa kwa material ya copper, iridium au platinums?
Anyways...
Linapokuja suala la ubora wa plug, kuna mambo ya kuangalia.
1. Performance (Utendaji wa kazi)
Plugs zilizoundwa kwa madini ya shaba au copper ndizo plug bora kabisa kwa performance kwa sababu kitaalam copper ina lower resistivity kuliko iridium na platinum...Waliosoma masuala ya umeme kama mimi wanafahamu mambo ya resistance of a conductor..
Hivyo copper inaruhusu umeme kutiririka vizuri kuliko iridium na platinum. In this case, most of performance cars kama Toyota Supra, Nissan skyline GT na mengine ya namna hiyo utakuta wanapendelea zaidi copper plugs kuliko iridium na platinum..
2. Longevity ( Kudumu kwa muda mrefu)
Linapokuja suala la plugs zinazodumu kwa muda mrefu basi platinum inashika Namba 1, iridium namba 2 na copper namba 3.
Iridium na platinum ni madini magumu kuliko copper hivyo yanadumu muda mrefu bila kuathiri performance yake kwa haraka ukilinganisha na copper..japokuwa iridium na platinum zina resistivity kubwa kuliko copper ila zinadumu ndiyo maana ukifunga unasahau kabisaa.
Linapokuja suala la bei, platinum ina bei ya juu ikifuatiwa na Iridium kisha copper ni ya mwisho..
Sasa kuna hizi plugs za kichina unakuta plag inauzwa 3500/, 4000/ yaani bei zake hazivuki 10,000/..hizi zina mashaka....wanaweza wakaandikia iridium kumbe siyo, wanaweza wakaandika copper kumbe ni aluminium au madini mengine ya bei rahisi....ndiyo maana unakuta mtu kafunga plug miezi miwili tu tayari zinaaza kuleta misfiring.
Conclusion
**Kama unahitaji plugs zenye high performance zinazoishi muda mfupi, go for copper.
**kama unahitaji plugs za standard required performance and recommended by the most of car manufacturers na kudumu muda mrefu sana, just opt for iridium or platinum kama wallet ina mbavu nene..
Nawasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app