Boeing 747
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 3,515
- 9,415
- Thread starter
- #61
Tofauti na umbali kuna dalili unaweza kuziona kwenye gari lako...mfano gari kupunguza nguvu, gari kutokuchanganya haraha kama mwanzo, ulaji wa mafuta kuongezeka na sometimes kama zimechoka sana unaweza kupata misfiring...Mkuu aksante sana kwa elimu nzuri unayoitoa hapa na uzoefu wako kwenye magari...
Naomba unisaidie jambo...nitajuaje kuwa spark plugs zinatakiwa kubadilishwa tofauti na huo umbali ulioshauri???
Angalizo...
Kama fuel pump imechoka, air filter kama imeziba au ni chafu sana pia unaweza kuona hizo dalili hapo juu..
Kwa hiyo hizo dalili zinategemea sababu nyingi sometimes hata MAF iliyochafuka au kuharibika utaona dalili hizo na zaidi utapata check engine light