Je, Umewahi Kuvunjia Kichwa cha Plug kwenye Cylinder Head?

Je, Umewahi Kuvunjia Kichwa cha Plug kwenye Cylinder Head?

Mkuu aksante sana kwa elimu nzuri unayoitoa hapa na uzoefu wako kwenye magari...
Naomba unisaidie jambo...nitajuaje kuwa spark plugs zinatakiwa kubadilishwa tofauti na huo umbali ulioshauri???
Tofauti na umbali kuna dalili unaweza kuziona kwenye gari lako...mfano gari kupunguza nguvu, gari kutokuchanganya haraha kama mwanzo, ulaji wa mafuta kuongezeka na sometimes kama zimechoka sana unaweza kupata misfiring...

Angalizo...
Kama fuel pump imechoka, air filter kama imeziba au ni chafu sana pia unaweza kuona hizo dalili hapo juu..

Kwa hiyo hizo dalili zinategemea sababu nyingi sometimes hata MAF iliyochafuka au kuharibika utaona dalili hizo na zaidi utapata check engine light
 
Aksante Mkuu kwa maelezo mujarabu...
 
Za nickel vp mdau???
Nickel/copper spark plugs...
Hizi ni spark plugs ambazo ni standard kwa pesa yako...bei nafuu kulinganisha na iridium au platinum.

Structure yake huwa wana coat nickel alloy kwenye electrode lakini sehwmu ya ndani inayopitisha umeme huwa ni shaba/copper..

Plugs hizi hazishauriwi sana kwenye magari yenye COIL ON PLUG au modern cars, japo baadhi ya magari ya high performance yanaruhusu kutumia plugs hizi ili kupata spark yenye nguvu./mlipuko mkubwa ndani ya combustion chamber.

Faida ya plugs hizi za nickel/copper ni kuwa zina uwezo wa kutoa spark kubwa zaidi kuliko iridium au platinum lakini hazina maisha marefu kulinganisha na iridium au platinum.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, plugs za nickel ni nzuri zaidi kwa magari ya miaka ya 1970s huko kwa sababu technology yake ya mfumo wa ignition ilikuwa ni duni kulinganisha na magari ya miaka hii....hivyo spark plugs hizi zilikuwa msaana mkubwa sana kwa mifumo hiyo ya zamani kuhakikisha inafanya kazi ipasavyo.

Kwa technolojia ya leo, iridium na platinum ndiyo zinakuwa recommended kwa sababu mifumo ya ignition imeboreshwa na coil zinaweza kuzalisha umeme mkubwa sana wenye nguvu tofauti na mifumo ya zile distributer za zamani.

Wengine wataongezea.
 
Leo tarehe 9/3/2020 nilikuwa nina ratiba ya kubadili Spark plugs kwenye kausafiri kangu..

Niliponunua nikarejea nyumbani, nikachukua vifaa vyangu nikaanza zoezi la kutoa plugs za zamani na kuweka mpya.
kufungua cylinder head ingechukua mda gani?
 
Leo tarehe 9/3/2020 nilikuwa nina ratiba ya kubadili Spark plugs kwenye kausafiri kangu..

Niliponunua nikarejea nyumbani, nikachukua vifaa vyangu nikaanza zoezi la kutoa plugs za zamani na kuweka mpya.
Plug zingine ni fake.

Mimi huwa nanunua plug pale palipokuwa ofisi za tigo zamani kabla kuhama ..pale kamata panaitwa GATHANI..karibia na kituo cha basi GOLDSTAR.

wao wanauza original plugs. Na ni viuri uende na kadi yako ya gari huwa kuna namba za engine wanazichukua kwenye gari na kukupatia plugs zinazoendana na gari yako.

Ukipata plugs zinazoendana na gari yako zinasaidia unywaji wa mafuta unakuwa mzuri kwenye gari na pia gari inakuwa haina miss miss za kipuuzi au gari kukosa nguvu.

Kila gari ina plugs zake.

Nenda hapo watakuelekeza.
 
Plug zingine ni fake.

Mimi huwa nanunua plug pale palipokuwa ofisi za tigo zamani kabla kuhama ..pale kamata panaitwa GATHANI..karibia na kituo cha basi GOLDSTAR...
Shukrani kwa ushauri mkuu
 
Back
Top Bottom