Je, Umewahi Kuvunjia Kichwa cha Plug kwenye Cylinder Head?

Mkuu unabishana na watu pengine hata hayo magari ya Nisan au Toyota hawana hivi plugs zipi ambazo ni imara na nzuri kati ya zilizoundwa kwa material ya copper, iridium au platinums?
Hahaaa..[emoji851][emoji851] Jamaa ameweka ligi kweli..
Anyways...
Linapokuja suala la ubora wa plug, kuna mambo ya kuangalia.

1. Performance (Utendaji wa kazi)
Plugs zilizoundwa kwa madini ya shaba au copper ndizo plug bora kabisa kwa performance kwa sababu kitaalam copper ina lower resistivity kuliko iridium na platinum...Waliosoma masuala ya umeme kama mimi wanafahamu mambo ya resistance of a conductor..
Hivyo copper inaruhusu umeme kutiririka vizuri kuliko iridium na platinum. In this case, most of performance cars kama Toyota Supra, Nissan skyline GT na mengine ya namna hiyo utakuta wanapendelea zaidi copper plugs kuliko iridium na platinum..

2. Longevity ( Kudumu kwa muda mrefu)
Linapokuja suala la plugs zinazodumu kwa muda mrefu basi platinum inashika Namba 1, iridium namba 2 na copper namba 3.
Iridium na platinum ni madini magumu kuliko copper hivyo yanadumu muda mrefu bila kuathiri performance yake kwa haraka ukilinganisha na copper..japokuwa iridium na platinum zina resistivity kubwa kuliko copper ila zinadumu ndiyo maana ukifunga unasahau kabisaa.

Linapokuja suala la bei, platinum ina bei ya juu ikifuatiwa na Iridium kisha copper ni ya mwisho..

Sasa kuna hizi plugs za kichina unakuta plag inauzwa 3500/, 4000/ yaani bei zake hazivuki 10,000/..hizi zina mashaka....wanaweza wakaandikia iridium kumbe siyo, wanaweza wakaandika copper kumbe ni aluminium au madini mengine ya bei rahisi....ndiyo maana unakuta mtu kafunga plug miezi miwili tu tayari zinaaza kuleta misfiring.

Conclusion
**Kama unahitaji plugs zenye high performance zinazoishi muda mfupi, go for copper.

**kama unahitaji plugs za standard required performance and recommended by the most of car manufacturers na kudumu muda mrefu sana, just opt for iridium or platinum kama wallet ina mbavu nene..

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo...
Lakini kwa sababu nyingi tunazofunga ni after market, na tunanunua kwa bei isiyoumiza sana. ni vyema kubadili angalau km 16000/...
Kwa mfano plugs umezinunua 100k, ukizitumia kwa muda wa mwaka na miezi sita naona ni fair kabisa...pesa yako itakuwa imerudi na change juu.
Genuine zinaweza enda zaidi ya 70,000kms

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwa kufanya DIY maintenance mkuu. Hii naiunga mkono saana. Soon nitaleta uzi wa Oil na ATF Change ili watu wajifunze.
 
Sio kwenye engine ila niliwahi kutumia drill kutoboa katundu kadogo kwenye screw. Alafu nikatumia alan key kuifungua
 
Kwa namna nilivyokaza lazima tu ikatike...
Uko sahihi, ubora wa plug sio ugumu wa plug Bali ni uwezo wa kutoa spark (mlipuko) na kudumu muda mrefu ambao kwa kawaida hutegemea madini yaliyotumika.

The best ni iridium unatembea zaidi ya kilomita 100,000. Nina mpango wa kubadilisha spark plug hivi karibuni na nitakubali kutoboka mfuko ili kununua za iridium. Nitafunga mwenyewe, japo sio fundi lakini ni mtundu sana yanapokuja masuala ya magari

Sent from my Nokia 6.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Gauge ya temperature ulikuwa huioni mkuu?

Sent from my Nokia 6.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Ukitumia denso Iridium Spark plugs Kwa Toyota ni km laki moja, hiyo ni warant kabisa mkuu.

Sent from my Nokia 6.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Hongera kwa kufanya DIY maintenance mkuu. Hii naiunga mkono saana. Soon nitaleta uzi wa Oil na ATF Change ili watu wajifunze.
Hizo mimi siku hizi nafanya DIY. Nataka ni advance kwenye DIY hadi nianze kuwa fundi kidogo kidogo maana mafundi wa mtaani ni wengi na hawana weledi kabisa

Sent from my Nokia 6.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Hizo mimi siku hizi nafanya DIY. Nataka ni advance kwenye DIY hadi nianze kuwa fundi kidogo kidogo maana mafundi wa mtaani ni wengi na hawana weledi kabisa

Sent from my Nokia 6.1 Plus using JamiiForums mobile app
Ni wazo zuri saana. Na utaepusha makosa mengi kwenye maintenance. Maana utakuwa unafanya research kwanza ndio unajua the right thing to do. Sio mafundi wetu wa kujifunzia kwenye gari lako. Mpaka anagundua tatizo moja, ameshatengeneza mengine kama tisa hivi.
 
Ni kweli mkuu. Huwezi kufanya DIY bila kusoma manual. Pia Mimi najifunza kwa video za you tube kuna jamaa anaitwa Peter Finn the Car Doctor anafundisha kwa vitendo, pia kuna Scotty Kilmer. Ukifanya kitu mwenyewe unakuwa extra careful na Kwa uhakika.

Nilipoteza mzuka na mafundi nilipouliza niweke oil gani kwa gari yangu wanasema SAE 40 wakati najua gari yangu inatumia 5W30. Ni heri kusema sijui kuliko kumpa mteja kitu ambacho si sahihi

Sent from my Nokia 6.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Hehehee! Aseme hajui akose soko? Yaani wanakosea saana. Tena hapo kwenye oil ndio usiseme. Kuna tatizo balaa. Usipokuwa makini utawekewa oil ya tractor kwenye saloon car.
 
Mkuu aksante sana kwa elimu nzuri unayoitoa hapa na uzoefu wako kwenye magari. Naomba unisaidie jambo...nitajuaje kuwa spark plugs zinatakiwa kubadilishwa tofauti na huo umbali ulioshauri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…