Je, una imani na jeshi la polisi kuomba escort unapokuwa na fedha au madini?

Ujinga tu wa watu.
Escort humparamii askari kwenye daladala kisha umuombe,au huzoi askari wanaokaa mataa na kuzurula na piki piki kisha uwaambie una madini.haiko hivyo.

Ingekuwa ni rahisi kuiba kwa mtindo huo,za kwanza kuibiwa zingekua banki zinazofanya kazi ya kuhamisha pesa tawi moja kwenda jingine kwa kiasi kikubwa,mpaka 2bln wakati mwingine.

Mwenye shida ya kupewa escort,ataripoti kituoni kwa kutoa taarifa zote muhimu,atapewa askari kimandishi wakiwa na silaha,kisha atalipia gharama zao atakazo ainishiwa. Kisha kwenda kufanya zoezi lake kwa usalama kabisa.

Utaigiza tu kutowamini polisi,lakini kuhamisha madini yenye thamani kubwa bila ulinzi imara ni uamuzi wa mfanyabiashara kiazi,sio kampuni inayojitambua.
 
Huuu mtego siungiii kwamweeeee
 
Kama fisi ana uwezo wa kutumwa nyama na aifikishe bila kuoinja au kuila yote basi na polisi nao wataweza kusindikiza pesa ya mtu binafsi.
Ile pesa ya banki au makampuni inayosindikizwa na mapolisi haiporwi kwa sababu tu ya network ya ulinzi iliyo nyuma ya safari.
Ikitokea tu opportunity ya hakikisho la kupoteza ushahidi wa wasindikizaji hiyo nayo inapigwa mchana kweupe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Police na Mke hawatakiwi kujua harakati zako za hela nyingi, msiseme hamkuambiwa.
 
Nenda mwenyewe we!
Ukikabwa yakakukuta basiiiiii au kodi ulinzi kutoka nchi za wenzetu huko
 
Polisi kabisa tena wa Tz uwahusishe kwenye pesa,,zikiwa 10M haina shida ila kuanzia 200M usijaribu
 
Eatakufksh salam ila after apo jiandae [emoji16]🟤
 
Tatizo Imani ya Raia Kwa jeshi la polisi imeshuka mno,kuna chuki kubwa sana baina ya Raia na police........
 
Kaka,hapa sio swala la kulishwa sumu ya chuki dhidi ya polisi.....kama polisi wanatenda hayo wanayotuumiwa nayo na raia wanaona unadhani wataacha kuwachukia polisi?.Kwahyo usikomae sana kwamba watanzania wamelishwa sumu ya chuki dhidi ya polisi.....No.....kuna watu wameumizwa sana na wameumiziwa wapendwa wao na Mali zao n.k.na hao ambao wewe unasema watu wamelishwa sumu kuwachukia.Polisi ni watu kama sisi...kwahyo hata maovu pia wanaweza kutenda kama raia wengine tu.......Kwahyo sio wote wanaochukia polisi ni kwamba wamelishwa sumu ya chuki.....Lazima watakuwa na sababu zao za msingi...tena nyingi tu.Chunguza utagundua Hilo.Nadhani Kwa mahusiano mabovu yaliyoko baina ya Police na raia ni vyema wakajirekebisha sana....picha sio nzuri,hata Police wenyewe wanajua kuwa Raia wengi hawawapendi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…