Je, una kiwango cha kuridhika kwenye maisha yako au you just want it all?

Kila mtu ako na test yake kwenye mafanikio kwa maana jinsi Mimi nnavyoyatafsiri mafanikio inawezekana ikawa tofauti sana na jinsi wewe unavyoyatafsiri.

Kuna watu hawahitaji mambo mengi, kwa maana unakuta akimiliki gari la kutembelea akiwa na nyumba yake ya kuishi na familia yake na kufanya investment za hapa na pale ambazo zitamfanya awe comfortable kwenye kula na kulipa bills nyinginezo hana shida ya kuhangaika tena bali akatulia na kuishi maisha yake.

Ila kuna wengine wanaweza wakawa na vitu vyote hivyo lakini bado wakawa wanaona kama wako na safari ndefu sana ya kufanikiwa, na utakuta ni aina ya watu ambao kila ukikaa nao utaona wanalalamika kwamba maisha magumu and vitu kama hivyo.

Kwamfano Mimi sina mambo mengi, nahitaji vitu nnavyohitaji kuvifanya nivifanye kila ninapojiskia na pesa isiwe sababu ya kuwa kikwazo cha kutokufanya mambo hayo, huu ndio watu huwa wanaita uhuru wa kifedha.

Nikiamka zangu asubuhi niko na mood zangu za kwenda somewhere for no reason, nivute laptop yangu nikate ticket niweke nguo mbili tatu kwenye kibegi changu shwaaaaa nisepe.

Just to be free and to explore the world bila kikwazo chochote kinachotokea upande huo wa kitu kinachoitwa pesa.

Kuhusu kiasi cha namba ambacho nahitaji hakisemekani ila ni any number ambayo itanifanya niwe huru bila stress yoyote.
 
Nadhani mimi na wewe hatuna tofauti kubwa kwenye hili, mimi pia I just wanna be free bro.

Nilale, niamke, nisafiri kwa style niitakayo au niipendayo.

Beside nili ifanya hii 2023, I went here and there just to explore na kufurahi.
Ila kwa basi na gari private mzee๐Ÿ˜‚.
 
Kuna aina fulani ya maisha ukiipitia (maisha ya ukata) unakuja kugundua wale waliosema basic needs ya human ni food, shelter and clothes waliona mbali sana.

Kwa mtu ambaye hana uwezo wa kumudu hizo basic needs siku akija kumudu nadhani kwake ndio itakuwa mafanikio makubwa sana.

After all mafanikio ni suala ambalo ni subjective and personal, kila mtu anatafasiri kwa angle yake.Kitu ambacho wewe kwako unadhani ni mafanikio kwa mwingine ni kinyume chake and vice versa
 
Ni kweli kabisa, but we all wish for the best circumstance.

Hiyo ya basic needs ni sahihi, nili enda sehemu wao kula milo 3 ni ndoto.
 
Dunia haina cha zaidi ya hilo mkuu๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…... Usiache kuendelea kuexplore maana ni kitu kinachotuliza sana akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ