Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Nimekuwekea link inayoonyesha asili ya white people kupewa jina la wazungu. Wewe unaniletea origin ya neno "mizungu"
Niwekee link ulipotoa hiyo information kuwa wazungu walipewa hilo jina kwasababu wako kama miungu. Weka hiyo link nijisomee then nirudi hapa
Umeweka link ya mtu ambaye hajui hata Kiswahili, mimi nimekupa neno la Kiswahili linalounganisha neno "mizungu" na "Miungu/Mungu".

Inawezekana una hobby ya ubishi tu.

Tafsiri unayoisema imesemwa mwisho kabisa kama habari ya utani, baada ya watu kujadili tafsiri serious niliyoitaja mimi.

Mzungu - Wikipedia, kamusi elezo huru
Asili ya neno[hariri | hariri chanzo]
Asili ya neno haijulikani kikamilifu.

Inaonekana kuna uhusiano na neno mzungu / mizungu lisilo kawaida tena katika Kiswahili cha kisasa lakini limetunzwa katika kamusi za Kiswahili zilizokusanya maneno yake mnamo mwaka 1900. Lilimaanisha mambo mbalimbali kama vile: 1) kitu cha ajabu au cha kushangaza, 2) mbinu ya kujiondoa katika tatizo, 3) aina ya muhogo, 4) silika au akili ya wanyama.[2]

Waswahili waliwahi kutumia neno "mzungu" kwa "akili" na pia kwa mafundisho ya "unyago" yaliyoitwa "kufundishwa mizungu".[3]. Kama asili ya "Wazungu" iko hapa iliweza kumaanisha "watu wa ajabu, wasio kawaida, wenye mbinu nyingi" au "wageni walio tofauti sana".

Wengine wamehisi kwa utani ya kwamba kuna uhusiano na kitenzi "kuzunguka" na "mzungu" ilitaka kutaja tabia ya wapelelezi, wamisionari na wafanyabiashara wa kwanza kutoka Ulaya ambao hawakukaa mahalipamoja bali walizungukazunguka kote Afrika.
 
Hayo ndo maswali ambayo hata Mimi nilikuwa najiuliza,hivi inakuwaje mtu anadai nyoka kiumbe ambacho ni hatari kwa binadamu

critical thinker
natamani sana kufahamu,formula ama huo uwezo ambao watu wanao.kwamba wamepewa na Mungu au shetani,maana kubadili kiumbe hai kukifanya utakavyo sio rahisi ivo.nafahamu binadamu tunatengeneza na kubadilisha vitu visivyo na uhai.ila uchawi wa kumfanya nyoka amuue,binadamu au kutumika kwa kazi hizo ni ngumu kuamini.
 
Mazee, unaaminikwamba mbwa anawezakufundishwa kurukia mpira? Au tembo anaweza kufundishwa kucheza mpira?

Kuna videos You Tube wanyama wanafundishwa kucheza michezo ya ajabu ajabu. Wengine wanafundishwa mpakakufanya hesabu.

Ukipeleka shows kamazile vijijini huko,ukawaambia watumimi nina nguvu za kichawi za kuwasiliana na wanyama, wanakuamini.

Kuna m South Africa anacheza na Simba. Watu wa vijijini wakiona zile video watasema huyu mchawi.

Bibi wa watu pengine kwao wana utamaduni wa kucheza na nyoka miaka mingi, watu wanasema mchawi.

Ukiangalia movie ya majoka kwenye giza, mtu akija kwanyuma akakugusa mguuni tu unaruka kwa kufikiri umeguswa na nyoka.

Ndicho kinachotokea kwenye jamii zetu.

Tumesimuliwa sana stories za uchawi, kikitokea kitu kidogo tu chenye mazingira yanayoweza kuelezekakwa nadharia ya uchawi,tunasema uchawi.

Akitokea kibibi ana machomekundu anatembea uchi kwa magonjwa ya akili na ana decorations za kiasili, watu wanasema mchawi, wanamuua.

Hawataki kumchunguza.

Kumbe ukimpeleka Muhimbili kwa Profesa Kilonzo akampimaakili anakwambia huyu ana severe schizophrenia au magonjwa mengine ya akili, alitakiwa kwenda therapy na kupata dawa tangu mtoto,ilakwetu hamna hayo mambo. Ugonjwa wa kilinimpakauokote makopo.
hapo hapana shaka kabisa mkuu,sababu unaelezea kituambacho kipo au kinawezekana...shida ipo,kwenye misingi ya imani au hao watu wanaotumia wanyama kiuchawi hapo ndo kuna shida.utakuta mtu anakwambia amemkuta nyoka ndani au sehemu ambayo haiwezi kupitika kabisa,sasa huyo kaingiaje au hapo kafundishwa vp....hapo ndo nataka kufahamu uchawi unafanya kazi vp na kubadili vile vitu ambavyo physically tunaona haviwezekani.
 
uchawi upo tena upo saana tu wiki iliyopita rafiki wa mwanangu alikuwa akijisomea mida ya saa 2.45 usiku likatokea paka na kusumbua kwa kilio cha nyaaau! nyaaau mara kadhaa mtoto akamtimua paka likaondoka kisha likarudi tena ndio mtoto akalibutua teke na kuendelea na kujisomea.Siku ya pili mama mtoto akaitwa kwa.mwnyekiti wa mtaa kashakiwa na jirani kuwa alimpiga na kumvunja mguu,Mama wa mtoto alishauri wasubiri mtoto arudi shule ajae nae ajibu kwanini alimpiga mama huyo.Kijana aliporudi walinipitia tukajumuika kwenye mashauri hayo ndipo mtoto alieleza jinsi ilivyokua kuwa "ALIPIGA PAKA ALIYE MSUMBUA NA SI MTU TENA HAKUMBUKI PAKA HUYO ALIINGIAJE CHUMBANI NA ALIONDOKAJE BAADA YA KUMPIGA" mama aliendelea kudai kupigwa akaanza kulia kwa sauti na kugalala kisha akaondoka hakutaka suluhu ila kijana amekuwa kichaa hakufanikiwa kumaliza hata darasa la 7 ambaalo angetarajia kumaliza mwaka huu.na wamehama maeneo hayo.UCHAWI UPO !!!!
 
Story za kitoto hizi. Uchawi, ulozi, wanga ni story za kusadikika hazina uhalisia wowote. Wavivu wa kufikiri na watu wasio makini ndo wanaamini haya mambo. Hakuna uchawi
 
Nasikia wamemfanyia hiyo Magufuli Ikulu mpaka anataka kuhamia Dodoma.

Ila mimi siamini uchawi. Inawezekana ni sayansi isiyojulikana tu.

Nikupe mfano.

Ukimchukua mtu wa miaka ya 1600 huko, ukamuonyesha jinsi ndege inavyopaa, jinsi mawasiliano ya internet na redio yanavyofanya kazi,etc, halafu ukamwambia huu uchawi, most probably atakubali ni uchawi.

Kwa sababu kwake ni vitu vya ajabu.

Kumbe ni vitu vinavyoweza kuelezeka naturally tu,huhitaji supernatural powers kuvielezea.

Kuna muandishimmoja nampenda sana wa science fiction, anaitwa Arthur C. Clarke, alisema "Any sufficiently advanced technology is indistiguishable from magic".

Teknolojia yoyote iliyoendelea sana haitofautiani na uchawi.

Sasa mtajuaje mnachoita uchawi ni uchawi (i.e, supernatural powers) au ni kitu kinachotumia sayansi na teknolojia ambayo hamjajijua tu (i.e natural powers but unknown at the time) ?

How do you tell the difference?

Wale mababu zetu walioona wazungu wanajua kutabiri kupatwa kwa jua waliwaona wazungu wachawi (ndiyomaana wakawaita wazungu,wazungu maana yake ni miungu - ukichukua mzungu ukatoa z unapata mungu -).

Sasa tutajuaje kwamba tunachofikiri ni uchawi si sayansi tofauti tu ambayo hatujaijua?

If at all the suspicion is authentic.
Mkuu walimfanyia nini Magu hapo ikulu? hebu tupe uhondo kidogo.
 
Kuna watu wanaamini mitini miungu yao, wanaomba kwenye miti.

Walikuwa wanaheshimumazingira,na leo tunajuakwamba mitiinasaidia kutunza mazingira na kuleta mvua.Wao waliiabudu mitina kukataza isikatwe. Wakiomba mitiiwatunze. Na kwaaina fulani ya kufikiri, walikuwa sawa, kwa sababu mitiilisaidia kuwatunza.

Sasa ule uanamazingira wa asili nao utaitwa uchawi nao?
Maswali yako yanafikirisha mkuu...
 
...

Wale mababu zetu walioona wazungu wanajua kutabiri kupatwa kwa jua waliwaona wazungu wachawi (ndiyomaana wakawaita wazungu,wazungu maana yake ni miungu - ukichukua mzungu ukatoa z unapata mungu -).
....

Kwenye "mzungu" upo tayari itolewe "z" ili iwe "mungu" ila kwenye "zunguka" unaulizia "ka" imeenda wapi.

Kuna maneno yanabadilika kadri muda unavyoenda na wakati mwingine hata maudhui ya neno husika huweza kuhama kabisa.

Wazunguka kubaki wazungu ni inawezekana. Ni kama neno mwanamume kuwa mwanaume.
 
Hahaaaaa umeniwahi!

Nami nilitaka kuhoji hivyo hivyo.

Binafsi naikubali zaidi nadharia ya 'mzungu' - mzungukaji na 'wazungu' - wazungukaji.

Naamini hivyo ndivyo ilivyokuwa [yaani kuzunguka zunguka kwao] hadi kupelekea wao kuitwa hivyo.
 
Hakuna kitu kinachoitwa uchawi.

Hizi ni imani tu ambazo hazina ukweli wala uhalisia wowote.

Nilishaomba kurogwa toka miaka mingi lakini hakuna kitu kama hicho.
 
Jamani tuwaache wazungu, karne zilizopita wazungu walikuwa wanajua wachawi kama sisi tunavyoua Leo. Na criteria walizozitumia ni kama sisi tunazozitumia Leo.wao walikuwa wanasema Mzee mwenye macho mekundu na ambayo ana uzito mdogo below sikumbuki kana ni 50 au 60 kg which means atakuwa mwepesi kupaa na fagio waliuwawa. Uzuri wao wametengeneza mpk museums kwa ajili ya kumbukumbu kwa vizazi vijavyo. Tunavyovipitia Leo wao walishavipitia may be tumechelewa kimaendeleo lakini naamini tutafika haya mambo ya uchawi wa kulogana hatutayasikia tena

Kwa hiyo unakubali kuwa tuwaue mama zetu au baba zetu wembamba (ambao hatuwatunzi vizuri) na hii ni kutokana na matoto ya siku hizi yakifika mjini yanawasahau wazee wa kule kolomije?? Tuwaue kwa sababu wanaruka kwa fagio?? Haya nayaita mawazo mgando man.
Sio kila mwenye macho mekundu ni mchawi wala sio kila mwembamba ni mchawi. Kulogana kupo na kutaendelea kuwepo. Hakuna mchawi mkubwa kama anayekuchongea kwa boss wenu kila kakosa kadogo huku akiutumia mwili wake kumpumbaza boss. Nimewahi kufukuzwa kazi kwa kosa ambalo sikulitenda kumbe kisa ni mwanamke alimtaka boss amwandike kazi mdogo wake.
Kuna mchawi mbaya kama huyo?? Mama yangu alikufa na zaidi ya miaka 100 tuseme alikuwa mchawi?
 
Hakuna kitu kinachoitwa uchawi.

Hizi ni imani tu ambazo hazina ukweli wala uhalisia wowote.

Nilishaomba kurogwa toka miaka mingi lakini hakuna kitu kama hicho.
Kurogwa hakuombwi bali kuna sababu zake hadi kufikia hatuya ya kutogwa.Hivi we unadhani wale walio act movie za kichawi walibuni tu or there are something behind

critical thinker
 
Kwa hiyo unakubali kuwa tuwaue mama zetu au baba zetu wembamba (ambao hatuwatunzi vizuri) na hii ni kutokana na matoto ya siku hizi yakifika mjini yanawasahau wazee wa kule kolomije?? Tuwaue kwa sababu wanaruka kwa fagio?? Haya nayaita mawazo mgando man.
Sio kila mwenye macho mekundu ni mchawi wala sio kila mwembamba ni mchawi. Kulogana kupo na kutaendelea kuwepo. Hakuna mchawi mkubwa kama anayekuchongea kwa boss wenu kila kakosa kadogo huku akiutumia mwili wake kumpumbaza boss. Nimewahi kufukuzwa kazi kwa kosa ambalo sikulitenda kumbe kisa ni mwanamke alimtaka boss amwandike kazi mdogo wake.
Kuna mchawi mbaya kama huyo?? Mama yangu alikufa na zaidi ya miaka 100 tuseme alikuwa mchawi?
Nadhani hukumwelewa vizuri ila alichokwambia kuwa hizi imani hazikuwa Africa tu hata Ulaya pia zilikuwepo lakini baada ya kuingia kwa ustaraabu wa middle East ndo wakaziacha

critical thinker
 
Kwa hiyo unakubali kuwa tuwaue mama zetu au baba zetu wembamba (ambao hatuwatunzi vizuri) na hii ni kutokana na matoto ya siku hizi yakifika mjini yanawasahau wazee wa kule kolomije?? Tuwaue kwa sababu wanaruka kwa fagio?? Haya nayaita mawazo mgando man.
Sio kila mwenye macho mekundu ni mchawi wala sio kila mwembamba ni mchawi. Kulogana kupo na kutaendelea kuwepo. Hakuna mchawi mkubwa kama anayekuchongea kwa boss wenu kila kakosa kadogo huku akiutumia mwili wake kumpumbaza boss. Nimewahi kufukuzwa kazi kwa kosa ambalo sikulitenda kumbe kisa ni mwanamke alimtaka boss amwandike kazi mdogo wake.
Kuna mchawi mbaya kama huyo?? Mama yangu alikufa na zaidi ya miaka 100 tuseme alikuwa mchawi?

Mi sijasema tuwaue wachawi nimemjibu huyo aliyesema wazungu wametuaminisha uchawi ni mbaya ndio nikamjibu hata hao wazungu wenyewe walikuwa wanajua wachawi so kila kitu tusiwe tunawasingizia hao wazungu na wao walikipitia hiki na sisi tutapita. Walikuja kujiina ni wajinga wakaacha so sisi badala tuache ujinga tuna kazi ya kulalamikia wazungu
 
Nyumbi hii bombi hii, hawa jamaa nyoka huko ndio vitendea kazi umesahau yule jamaaa aliyeuliwa nyoka yake na yeye akafa hapo hapo? Afadhali huyu nakumbuka mafinga niliona kijiti kinageuka mtu ndani ya coaster, mzee kadaiwa nauli katika kutoa pesa kile kijiti kikadondoka akaanza kuweweseka abiri fumbeni macho nawaaomba chonde chonde fungeni macho, mara harufu ikaanza kubadilika ndani ya gari ukizingatia kule ni baridi na ilikuwa saa kumi na mbili asubui abiria wengi walikuwa wamefunga vioo, kile kijiti kilianza kubadilika mle ndani huku kila mwenye macho akitazama...
 
Mkuu una undugu na mshana?,kutembea kwako na sura ni kama mshana jr isipokuwa wewe ukitembea hugeukigeuki nyuma kama mshana nadhani hugeukigeuki unaogopa kuwa nguzo ya sukari kama kama mrs rutu
 
Back
Top Bottom