Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,583
Umeweka link ya mtu ambaye hajui hata Kiswahili, mimi nimekupa neno la Kiswahili linalounganisha neno "mizungu" na "Miungu/Mungu".Nimekuwekea link inayoonyesha asili ya white people kupewa jina la wazungu. Wewe unaniletea origin ya neno "mizungu"
Niwekee link ulipotoa hiyo information kuwa wazungu walipewa hilo jina kwasababu wako kama miungu. Weka hiyo link nijisomee then nirudi hapa
Inawezekana una hobby ya ubishi tu.
Tafsiri unayoisema imesemwa mwisho kabisa kama habari ya utani, baada ya watu kujadili tafsiri serious niliyoitaja mimi.
Mzungu - Wikipedia, kamusi elezo huru
Asili ya neno[hariri | hariri chanzo]
Asili ya neno haijulikani kikamilifu.
Inaonekana kuna uhusiano na neno mzungu / mizungu lisilo kawaida tena katika Kiswahili cha kisasa lakini limetunzwa katika kamusi za Kiswahili zilizokusanya maneno yake mnamo mwaka 1900. Lilimaanisha mambo mbalimbali kama vile: 1) kitu cha ajabu au cha kushangaza, 2) mbinu ya kujiondoa katika tatizo, 3) aina ya muhogo, 4) silika au akili ya wanyama.[2]
Waswahili waliwahi kutumia neno "mzungu" kwa "akili" na pia kwa mafundisho ya "unyago" yaliyoitwa "kufundishwa mizungu".[3]. Kama asili ya "Wazungu" iko hapa iliweza kumaanisha "watu wa ajabu, wasio kawaida, wenye mbinu nyingi" au "wageni walio tofauti sana".
Wengine wamehisi kwa utani ya kwamba kuna uhusiano na kitenzi "kuzunguka" na "mzungu" ilitaka kutaja tabia ya wapelelezi, wamisionari na wafanyabiashara wa kwanza kutoka Ulaya ambao hawakukaa mahalipamoja bali walizungukazunguka kote Afrika.