Je, unafanyaje ukiwa umepigiwa full light barabarani?

Je, unafanyaje ukiwa umepigiwa full light barabarani?

Una uzoefu wa kuendesha gari highway usiku?
Embu nipe experience yako pale unapokuwa na gari ndogo kisha ukapishana na Lori ambalo limewasha full light.

Kile kipande cha sekunde chache mnapopishana huwa unaona au unaenda kwa uwezo wa Mungu tu?

Kuna ule mchezo road unapishana na mtu unapigia pass apunguze mwanga wa lakini ha-respond Hadi mnapishana.

Hapunguzi nawapongeza madereva malori huwa ni wastaarabu Sana.. upande wangu huwa nafanya vitu hivi nikiona mwenzangu hapunguzi mwanga

1.Napunguza mwendo
2. Sitazami lori, naangalia mstari wa pembeni nje ya barabara, naweka tairi za kushoto kwenye line.
3. Kama mstari wa nje haupo, natumia wa katikati, nahakikisha sitembei

Mwendo nakuwa mdogo mdogo sizidi 50kmph

.View attachment 2420048

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
View attachment 2420096
View attachment 2420097
nakutanaga nao sana hao hasa njia hii ya morogoro road hasa kuanzia mida ya saa 5 usiku.

sema ukinipiga full nami nakupigia pass ukigoma na mimi nakuwashia full zote mixer na taa za juu na sizimi mpaka tupishane hata kama wewe utazima
 
Uko mahali Pako mwenyewe Rudi nyuma paki sehemu safe tulia liende laa sivyoo utapata ajali
 
Akipiga full punhuza wewe,au zima kabsa..maana kwa mbele yako Kuna mwanga wake unakupatia njia..all in all hata mm hiyo full siipendi..ikitua kwenye kioo mzee inavuruga mpk ubongo.
 
Hili swala Lina affect wengi Sana humu road wengine Wana matatizo ya macho na baadhi ya ajali zinasababishwa na hii kitu mkuuu so nivizuri kutoa elimu watu ambao huwa hawapunguzagi taa ni Hawa wenzetu wakina su,stk,STL mara nyingi nimekutana nao hawapunguzagi kabisa.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
Mkuu tabia ya mtu kurekebisha ni ngumu mno, but always Linda usalama wako, slow down,keep left, na dim taa zako, ukitaka kushindana naye unaweza poteza maisha, muda na utajiharibia safari yako, kupishana ni less than 4s!
 
Mfano ist au hivi baby Walker ukipima distance ya gari ndogo na kubwa gari kubwa inakuwa ipo juu kidogo so anapopiga full mwanga wote unamwagikia kwenye uso wako Hawa jamaa wa mabasi,STL,stk,su baadhi ni wababe road.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
I wish ni milik mandoline af miwekee ngao ya chuma still afu niwakomeshe kwa kupiga Taa zao
 
Unapunguza zako unawasha packing alafu unapaki pembeni kwa mda hadi mkubwa apite.ukijifanya unakomaa dereva kama mimi nina tone 32 nyuma nishaweka gari kati kati ya chaki niko gear ya 14 high kitu kina nesanesa eti nirudi kwangu ghafla ili tela ivute nichochore?hapana kwa kweli Mungu atanisamehe maana nikiangalia ushahidi hamna alafu ndio usiku wewe uko na ka ai esi tii kako watakuja kukutindua na tindo kukuokoa au kukupeleka kwenye kabati la mbeho
 
Hakuna madereva siwapendi kama waendesha malori....
Nilishapigwa full taa,zile zinakaa juu kabisa ya kibini aisee, aah wakuu mungu ni wakuabudiwa siku zote..

Nikikuwaahia sport lite za chini zile 2 ukakomaa nakuongezea zile nne pale juu ya kibin napiga full nikikuongezea hapo na bikon kidogo na hone kwanini usichochore mwenyewe[emoji13][emoji13][emoji13]
 
Hata magari makubwa mkuu ni wachache hasa madereva wa malori ya mizigo wana adabu kidogo usiombe ukutane na hawa wa malori ya mchanga ni shida.

Gari imewaka taa kama kituo cha kupozea umeme cha tanesco mbele huoni. Mimi huwa nikiflash taa zangu naona hapunguzi nawasha full na mimi huku nikijihami kwa kupunguza speed.

N:B sipendi kuendesha gari usiku sababu madereva wengi hawafuati sheria usku na walevi ndio mida yao hyo.
Mafuso na magari ya kokoto ndo wenye fujo.

Ila semis hawanaga noma. Ni wastaarabu sana.

Wanaoendesha vigari vidogo ndo pasua kichwa sasa. Hao anaweza asipunguze mwanga hata kama umemuomba apunguze.
 
Mtoa mada hapa sio Tu umeomba ushauri Bali ndivyo inavyotakiwa kufanya ukiwa unaendesha gari usiku yote ambayo umeorodhesha ndiyo njia sahihi ya kuepusha ajali Kwa kifupi wewe ni pia unajua kanuni ya uendeshaji usiku.

kwa kuongezea nyama ni hivi ukiwa unadrive usiku zingatia Sana mstari wa katikati hata kama utapigwa taa weka Akilini gari yako isivuke upande wa mwenzako.
pia soma eneo la mbele yako zaidi ya Mita 50 kujua jinsi palivyo hii itasaidia Sana kucheza na upande wako wa kushoto Tu bila kutoka nje zaidi.

na ukitaka kuwa master wa kuendesha usiku jaribu kipande cha DAR -MORO hapa kuna kila aina ya vituko kuanzia mabus,malori na magari madogo pamoja na ubovu wa barabara hapa kuna madereva wastaarabu,walevi na walio na mioyo ya plastic hawaogopi kifo wala KABURI
 
Mafuso na magari ya kokoto ndo wenye fujo.

Ila semis hawanaga noma. Ni wastaarabu sana.

Wanaoendesha vigari vidogo ndo pasua kichwa sasa. Hao anaweza asipunguze mwanga hata kama umemuomba apunguze.
Hakuna watu nawakubali kama madereva wa malori hawa jamaa Wanajitambua Sana mara nyingi usiku huwa ukiwaomba kupunguza taa wanapunguza tena unatakiwa uombe mapema ukiwa mbali ukiwasha taa zako mara 4 lazima atapunguza mwanga Tu na hata ukipunguza mwendo na kuwasha indicator ya kulia atabalnce gari yake asikugonge
 
Back
Top Bottom