Historia naijua kwa kiasi chake na bado najifunza ila umeandika kwa mahaba zaidi ya hali halisi, labda kama una maana nyingine na si historia.
Utawala Otoman ambao ndio ulikuwa ukiitawala Palestine ulianguka baada ya vita ya kwanza ya dunia Uingereza ilichukua udhibiti wa Palestine chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa (League of Nations). Mwaka 1917, serikali ya Uingereza ilitoa Azimio la Balfour, ambapo ilitangaza uungwaji mkono kwa kuundwa kwa “makazi ya kitaifa kwa Wayahudi” ndani ya Palestina. Zingatia hili ndugu
kuundwa kwa “makazi ya kitaifa kwa Wayahudi” ndani ya Palestina!
Kufuatia mauaji ya kimbari (holocaust) kwa wayahudi na kufukuzwa fukuzwa maeneo mengi Ulaya wengi kupitia fursa hii walihamia Palestine kama wakimbizi.
View attachment 3264474
Hii ilisababisha mivutano kati ya Wapalestina na wahamiaji wa Kizayuni waliokuwa na lengo la kuanzisha taifa lao wenyewe. Hata ingekuwa ni sisi Tanzania tusingekubali kirahisi.
Baada ya mizozo ya hapa na pale mwaka
1947, Umoja wa Mataifa ulipitisha
Azimio, ambalo lilipendekeza Palestine igawanywe katika sehemu mbili:
56% ya ardhi iwe ya Wayahudi (ingawa walikuwa wachache kwa idadi wakati huo),
43% ya ardhi iwe ya Wapalestina na
1% (Jerusalem) iwe chini ya utawala wa kimataifa. Wapalestina walikataa mpango huo kwa sababu waliamini ulikuwa
hauna haki, kwani wao walikuwa wengi lakini walipewa sehemu ndogo ya ardhi yao ya asili. Kwahiyo walikuwa na sababu ya msingi kukataa ni kama ilivyotutokea sisi pale Iddi Amini aliposema kipande cha Kagera ni chake!
1948 Wayahudi walitangaza kuundwa kwa taifa lao, unadhani nguvu waliitoa wapi wakati mwanzo walikuwa hawana kitu? Jibu unalo. Nchi za Kiarabu zilikataa mpango huu zikaamua kuisaidia Palestine (walikuwa na haki ya kufanya hivi) lakini bahati mbaya walishindwa vibaya vita hii na kuifanya Israel kuchukua maeneo zaidi (78% ya ardhi ya Palestine). Kipindi hiki zaidi ya wapalestina 700,000 walihamishwa kwenye miji na vijiji vyao kwa nguvu na hawakuruhusiwa kurudi hata vita ilipoisha.
Na usidhani hawa mashetani Waisrael walijiongezea maeneo baada ya Wapalestina kuanzisha vita la hasha! Jamaa waliendelea kumega maeneo mengi zaidi kila siku hata baada ya vita na kusababisha Palestine kubaki na maeneo madogo zaidi. Mwaka 1967 Waarabu wakaamua kujitutumua tena kwa vita (6 days war) lakini pia walichemka na Muisrael akaendelea kumega maeneo zaidi wakati huu akiimega na Syria (Gollan Heights) na Misri (Sinai).
Hadi leo Israel bado anaishikilia Gollan heights lakini Sinai aliirudisha baada ya makubaliano ya kidiplomasia, unafikiri ni kwanini Myahudi hakuendelea kuishikilia Sinai kama lengo ni buffer zone!
- Misri ni moja ya nchi za kiarabu zenye nguvu kijeshi
- Misri ni mshirika wa Marekani.
- Shinikizo la kimataifa kwasababu mfereji wa suez unategemewa sana na nchi nyingi.
Unapoongelea buffer zone usisahau kuna nchi nyingi zimewahi kupigana lakini si kwa kuchukua maeneo kiasi hiki eti kisingizio buffer zone. Mfano south Korea na North Korea zilikubaliana
Demilitarized Zone baada ya vita na si kushikilia miji ya nchi nyingine na kuifanya kuwa yako!
View attachment 3264481
Inawezekana kuna mengi hujui kuhusu huu mzozo kwababu ya biased information ama kuchagua upande mmoja, mimi mwenyewe nilikuwa nawashangaa sana Waarabu miaka hiyo eti wanajilipua ili kuuwa Waisrael. Hizi harakati za Hamas unazoziona sasa ni kwasababu wamechoka kutawaliwa na kuendelea kuchuliwa maeneo kila kukicha. Wapalestina wanaishi kama wafungwa si Gaza wala West Bank. Israel inaamua nini kiingie nini kitoke Palestine, hawaruhusiwi kuwa na uwanja wa ndege, mashirika ya umeme hata maji kwasababu Israel anataka kucontrol kila kitu kwa kifupi Muisrael ni mtawala na Mpalestina ni mtawaliwa. Leo anaweza kuamua anaingia eneo fulani West Bank na kufukuza wanakijiji, kuvunja nyumba zao na kuweka makazi ya wahamiaji haramu, kumbuka West Bank hakuna Hamas! Kama Waafrika pamoja na ujinga wetu hatukukubali ujinga huu miaka hiyo iweje Waarabu wakubali kirahisi leo hii?
- Wakulaumiwa ni Wayahudi ambao waliombewa hifadhi wao wakajimilikisha na kutangaza taifa lao.
- Wakulaumiwa ni UN kwa kukosa nguvu ya kuchukua hatua na kuishia kutoa matamko tu.
- Wakulaumiwa ni Uingereza na USA kwa sasa kwa kuwa upande wa Waisrael kwasababu tu Zionist organizations and pro-Israel groups lobbying is one of the most powerful in the world.
Nakushauri rudi ukasome historia vizuri, kama hautakuwa na ushabiki na mahaba utajifunza mengi na utakuwa wazi hapa.