Memtata
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 587
- 1,863
Ni kweli wapo Waarabu wengi wanaishi ndani ya Israel na wana uraia wa israel kani si kweli kwamba wanaishi kwa amani na haki sawa, ila sio rahisi serikali ya Israel kuliweka wazi hili.Unaposema "... (Wayahudi) kujifanya wenye haki ya kuishi hapo peke yao"
Unamaanisha nini ukizingatia kwamba ndani ya Israel kuna Waarabu zaidi ya 2m wanaishi kwa amani pamoja na Wayahudi?!
Tatizo ni hao Hamas na washirika wao waliojipa kandarasi ya kuwafuta kabisa Wayahudi, kazi ambayo kamwe hawatafanikiwa na inawakula wao wenyewe
Tuanze na Waarabu ndani ya Israel; Inakadiriwa Waarabu wapo kama 20% na ni asilimia 8 tu ndio wanaishi kwenye miji mchanganyiko na Wayahudi lakini wengi waliobaki wako kwenye miji iliyotengwa na Wayahudi na miji masikini sana. Waarabu wanabaguliwa kwenye mikopo ya elimu za juu, miradi ya maendeleo na hata baadhi ya shria haziwapi uhuru kama Wayahudi mfano: Nakba law hii inawazuwia Waarabu kufundisha historia yao ama kuelezea namna taifa la Israel lilivyopatikana, ikitokea taasisi imefanya hivi basi waziri wa fedha ameruhusiwa kuinyima fund taasisi hiyo ama watu hao. Hivi unajua hata IDs zao ni tofauti na zile za Wayahudi? Sasa unasemaje wanaishi kwa amani?!! Kwani hii inatofauti gani na ilivyokuwa kwa South Afrika kipindi cha apartheid?
Kwa wapalestina wa Gaza na West Bank; Huku ndio hata usiulize maana habari ziko wazi hadi zile media ambazo huwa biased kwa Israel kuna wakati mambo mabaya yanafanyika hadi inabidi wayaripoti wazi wazi, kama hujui uchafu anaoufanya Israel ndani ya maeneo haya aidha itakuwa umeamua kuchagua upande wako (hasa kwasababu za kidini) bila kujali nani mwenye haki ama ni unapata habari zenye upendeleo.
View: https://www.youtube.com/watch?v=Wxm2dTWANm0
Mara nyingi watu wamekuwa wakiitaja Hamas au juzi kilichotokea Oct. 7.... ndugu haya mambo unayajadili baada ya kuona Hamas kafanya tukio lakini hujiulizi kwanini wamefanya hivyo? Nini chanzo? Muisrael ameshachukua maeneo mengi lakini bado hajaridhika hadi leo West Bank inamegwa, Wapalestina wanaishi kama wafungwa kila kitu anaamua Israel. Nani atakubali kuishi maisha haya milele?
Israel akiuwa mnasema ni self defence ila Hamas wakijihami mnawaita magaidi! Wakati Israel ndio mvamizi. UN chapter 1514 (XV) – 1960: Inatamka kuwa ukoloni ni kinyume cha haki za binadamu na linahimiza uhuru wa haraka kwa mataifa yaliyotawaliwa na chapter 2625 (XXV) – 1970: Inatoa haki kwa mataifa yanayotawaliwa kupambana kwa njia zote zinazowezekana, ikiwemo vita vya ukombozi, dhidi ya utawala wa kikoloni na wa kibaguzi. So Wapalestina wako sawa na Hamas ni wapigania uhuru na si magaidi1