Eti Mungu anatumia USA kukamilisha maneno yake, hizi ni chai, kikubwa ni kuamini tu ilimradi siku zisonge.
Ngoja nikuweke sawa ewe mwana wa uasi.
Iko hivi: watu wote, kila mtu, na hata kila kitu (Yesu alisema hadi mawe pia) hutimiza makusudi ya Mungu.
Lakini kuhusu makusudi makuu ya utawala wa dunia, Marekani ndiye ameshikilia fimbo hiyo.
Tangu zamani, hata wakati wa nabii Danieli na kuendelea zilikuwepo falme zenye nguvu zilizoitawala dunia ya wakati huo, kama Asiria, Babeli, Umedi & Uajemi, Misri, Rumi, nk.
Hizo zote ziliinuka na hatimaye zikasambaratika na kutoweka kwa mujibu wa maandiko.
Waliojaribu kuinuka kinyume na unabii hawakuweza. Kwa mfano akina Musolini na Hitler.
Wasovieti walijaribu, wakashindwa. Urusi na China sasa zinainuka, lakini hazitashinda.
Kwa nini? Kwa sababu
haziko kwenye nafasi nzuri ya kuutimiza mpango mkuu wa Mungu kama ilivyo Marekani.
Hizi supapawa zingine ziko tu kubalansi nguvu ya Marekani na kulizuia wimbi la uovu kwa muda, lakini kamwe haziwezi kuipiku Marekani!
Siyo kwamba hazina uwezo huo. Hapana!
Sababu pekee ni kwamba hilo liko kinyume kabisa na mpango wa Mungu.
Watajaribu lakini hawataweza katu.