Hoja mkataa (dismissive arguments) kama hizi hazisaidii kitu. Mara nyingi ni kauli za waishiwa-hoja.
Nashangaa kwa nini msomi kama wewe hujagundua hilo.
Kama huna hoja kinzani, ukimya ni jambo la busara sana.
Do you have any evidence kuwa Bible au quran ni kitabu cha Mungu?
^Hard evidence^? Define hard evidence.
Je, ni uthibitisho unaoweza kuuamini wewe, ama ni ule ambao upo kihalisia?
Kwa sababu uwepo wa vithibitisho na kuviamini, ni mambo mawili tofauti kabisa.
Usinipe story za Roho Mtakatifu, nipe hard evidence out of Bible kuwa ni kitabu cha Muumba!
Unahitaji ushahidi, wakati huohuo unachagua utoke au usitoke wapi?
Maana yake umejaa nahaba (bias) hata kabla ya kuuona ushahidi wenyewe?
Pili, unahitaji vithibitisho kutoka nje ya Biblia na wala siyo ndani yake.
Huoni kwamba tayari umeshajichagulia nini cha kuamini na nini usiamini?
Kwa nini uwaamini waandishi nje ya Biblia, ilhali walioiandika Biblia unawaona hawafai?
Kwa nini ushahidi wote usitathminiwe kwenye uwanja na mawanda sawia?
Simply put, you can never be a scientist; may be a nominal one.