Je, Unaiamini hadithi ya mnara wa Babeli?

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Kwa hiyo unajipinga mwenyewe ama umebadili msimamo wako?

Angani mpaka wapi?

Anga ni kubwa sana. Kuna layers nyingi sana.

Kujenga mnara mrefu kwenda juu angani mpaka layer ya Exosphere Haiwezekani.
Nachukulia haya maelezo yako kwamba umekubali; upo uwezekano huo wa kujenga mnara hadi angani.

Kisayansi, hiyo ni hatua muhimu sana katika utafiti.
 
Brainwashed
Hoja mkataa (dismissive arguments) kama hizi hazisaidii kitu. Mara nyingi ni kauli za waishiwa-hoja.

Nashangaa kwa nini msomi kama wewe hujagundua hilo.

Kama huna hoja kinzani, ukimya ni jambo la busara sana.

Do you have any evidence kuwa Bible au quran ni kitabu cha Mungu?
^Hard evidence^? Define hard evidence.

Je, ni uthibitisho unaoweza kuuamini wewe, ama ni ule ambao upo kihalisia?

Kwa sababu uwepo wa vithibitisho na kuviamini, ni mambo mawili tofauti kabisa.

Usinipe story za Roho Mtakatifu, nipe hard evidence out of Bible kuwa ni kitabu cha Muumba!
Unahitaji ushahidi, wakati huohuo unachagua utoke au usitoke wapi?

Maana yake umejaa nahaba (bias) hata kabla ya kuuona ushahidi wenyewe?

Pili, unahitaji vithibitisho kutoka nje ya Biblia na wala siyo ndani yake.

Huoni kwamba tayari umeshajichagulia nini cha kuamini na nini usiamini?

Kwa nini uwaamini waandishi nje ya Biblia, ilhali walioiandika Biblia unawaona hawafai?

Kwa nini ushahidi wote usitathminiwe kwenye uwanja na mawanda sawia?

Simply put, you can never be a scientist; may be a nominal one.
 
Kwahio hii mipango ni ya kumfurahisha nani ? Wengine wateseke, Wengine wafe, Watu wanafanywa watumwa, Wanabakwa sababu Mungu alisema / amesema ndio ? For whose benefit ?

Au wale walioshika mpini ndio wanaku-convince wewe uendelee kupigika na kunyonywa sababu ni mpango wa Mungu ?

Unaongelea America hili Taifa Jipya wakati kuna Empires zilishapita hata USA hawezi kunusa (ila empires rise and fall) hio ni kawaida; Ingawa wewe unaona Mungu alipanga watu (Europeans) waende kuwauwa hao Red Indians na kuwasubjugate ili neno lake litimie ?
 
Nami nikuulize swali?

Biblia inaposema kwamba utawala fulani wa dunia utainuka na kufanya mambo kadha wa kadha bila kuutaja jina lake (rejea Ufunuo 13, kwa mfano), unadhani tunapaswa kuutambuaje???
Roman
Ottoman
British empire.
Germany under Nazi
Soviet union
Unasema marekani kwa sababu upo saa hivi waliosoma huo mstari zamani walidhani ni ottoman walidhani ni uingereza etc so bado huna hoja ya kuniconvince zaidi ya brah brah tu
 
Mkuu, namna yako ya kuisoma Biblia ni ya mashaka sana.

Hebu nukuu andiko lako ili watu wakusaidie kufafanua; vinginevyo utaendelea na ujinga wako katikati ya bahari ya maarifa.
Maarifa yapi kwenye biblia,

Kusoma kwa ufahamu nako unakutilia mashaka!?

Unadhani kunukuu kutabadilisha mchanganuo wa andiko nliokuandikia hapo!?

Unaelewa kitu kinaitwa kusoma kwa ufahamu!?
 
Kwani mbinguni ni wapi kama siyo hapo kwenye mawingu?
 
Hapa Kiranga anaweza kukupa maswali counter ukakimbia kabisa
 
Huwezi kutumia biblia ama quran kuthibitisha kuwa vimeandikwa na Mungu huyo!!

Kufanya hivyo utakuwa unafanya kosa kubwa la kimantinki.

Yaani unafanya circular argument, kwamba madai yanatumika kama uthibitisho.

Imagine biblia iwe kweli tu kuwa ni kitabu cha Mungu kwasababu ndani yake imeandikwa kuwa ni kitabu cha mungu!!

That is illogical.

Unaweza thibitisha Mungu yupo kweli na kwamba hizo hadithi za kwenye biblia na qurani si hadithi za uongo tu zilizotungwa na watu wajinga wajinga tu wasioelewa hata jua linaenda wapi usiku!?
 
Je? Unaamini pyramid zilijengwa na wanadamu?
 
Kwa hiyo unajipinga mwenyewe ama umebadili msimamo wako?
Hakuna sehemu nilisema hivyo.
Nachukulia haya maelezo yako kwamba umekubali; upo uwezekano huo wa kujenga mnara hadi angani.

Kisayansi, hiyo ni hatua muhimu sana katika utafiti.
Nakwambia hivi Haiwezekani kujenga mnara mrefu kwenda juu angani mpaka layer ya Exosphere.
 
Sijui ni mimi tuu, ila habari za kwenye biblia haziniingii kabisa akilini achilia mbali kwenda kanisani
Mkuu, ni kwa vile hujatulia ukaisoma Biblia vizuri.

Tafuta likizo moja tulivu hivi, jitafute peke yako na Biblia, utakuja kunishukuru baadaye.
 
Natamani nikwambie mambo ya Yale ma pyramids pale misri kua ndo mnara wenyewe Ila kwa sababu najua utabisha ngoja tu kikae kimya
 
Maarifa yapi kwenye biblia,

Kusoma kwa ufahamu nako unakutilia mashaka!?

Unadhani kunukuu kutabadilisha mchanganuo wa andiko nliokuandikia hapo!?

Unaelewa kitu kinaitwa kusoma kwa ufahamu!?
Awali uliuliza swali la Biblia, nikakutaka unukuu andiko ulikotoa swali lako, ili ujibiwe.

Mbona tena maelezo mareefu babu!?
 
Hujajibu hoja ya mleta uzi
 
Kwani mbinguni ni wapi kama siyo hapo kwenye mawingu?
Ni kweli.

Katika Biblia mawinguni nako ni mbinguni, japo siyo kwenye makao halidi ya Mungu kwa mujibu wa maandiko.

Lakini hebu nikupe faida ya mashaka kwamba uko sahihi.

Je, kufika tu hapo angani ndipo kuthibitisha kwamba hamna mbingu halisi?

Unajua pakoje hasa? Panaonekana kwa macho haya ya nyama?

Nadhani tufike hatua kama wanadamu tukiri tu kwamba kuna mambo yako nje kabisa ya upeo wetu.

Kukiri hivyo siyo udhaifu bali ni hekima. Kushupalia tusichokiweza ni sawa na kupiga ngumu ukutani.
 
Hakuna sehemu nilisema hivyo.
Je, unanithibitishia kwamba kuna hoja halisi ya uwepo (argument of existence)?

Namaanisha kwamba uwepo wa viumbe ni nadharia tu ama ni halisi?

Au tu akili zetu zinaota, na kwamba hakuna chochote kilicho yakinifu/halisi (kama wadaivyo wengine -- jambo ambalo wala halihitaji kufikiri ili kubaini kwamba haliwezekani)?

Nakwambia hivi Haiwezekani kujenga mnara mrefu kwenda juu angani mpaka layer ya Exosphere.
Majibu yako yameshathibitisha kwamba umekubali kuna uwezekano huo (rejea maelezo ya awali).

Huenda hujaelewa swali (japo umejibu kwa usahihi).

Nimeuliza (mfano): Unaweza kuruka?

Umejibu: Siwezi kuruka zaidi ya mita 2.

Hitimisho ni kwamba naam, unaweza kuruka!
 
Hujajibu hoja ya mleta uzi
Mkuu, sijui kama umegundua kwamba mleta-mada hajauliza swali lolote wala kuomba msaada?

Nimeona maelezo tu, nikajua anatualika kuingia uwanjani freestyle, ndiyo maana mie nikaamua kumswalisha.

Nasimama ili nirekebishwe! 🙂
(Niko radhi ku...)
 
Dini zimewajaza hofu na uongo mwingi Mungu yupo juu tukifa tunazikwa chini kwa nini Mungu asiwavurugie lugha watengeneza Rockets na setilites
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…