Miaka ya sabini wahasibu na watu binafsi walikuwa wakiporwa fedha walipokuwa wakienda au kutoka benki. Na matukio mengine yalikuwa fake. Kwa wakati huo Sh.20,000 ilikuwa ni mishahara ya taasisi nzima au mauzo ya wiki na zaidi. kuona hivyo serikali ikatunga sheria hiyo kwamba mtu yeyote akiwa anaenda au anatoka benki lazima asindikizwe na polisi. Na benki walikuwa hawalipi cheki ni lazima polisi asaini nyuma ya cheki kuthibitisha escort yake. Kuna wahasibu wajanja walikuwa wakiandika cheki ya 19,900 au cheki mbili za sh. 10,000 kukwepa adha ya kufuata escort. kwa bahati mbaya sheria hii imepitwa na wakati na haijarekebishwa.