JE, UNAJUA UNAWEZA KUONDOA TAARIFA ZAKO BINAFSI KWENYE GOOGLE NDANI YA DAKIKA 1 TU?

its MalekoGJ

Senior Member
Joined
Aug 27, 2020
Posts
136
Reaction score
292
đź”’ JE, UNAJUA UNAWEZA KUONDOA TAARIFA ZAKO BINAFSI KWENYE GOOGLE NDANI YA DAKIKA 1 TU?
Watu wengi hawajui kuwa Google inatoa njia ya kujilinda dhidi ya watu wanaotafuta jina lako, namba yako ya simu, email au anwani ya nyumbani mtandaoni.
Kwa ulimwengu wa sasa ambapo taarifa zako zinaweza kutumika vibaya kwa urahisi, hii ni njia ya haraka ya kuhakikisha faragha yako inalindwa.
Fuatilia hatua hizi kwa kutumia simu yako (Google App):
• Fungua Google App kwenye simu yako
• Gusa profile icon (ile picha au herufi yako juu kulia)
• Chagua “Results about you” — hapa ndipo Google inakusaidia kudhibiti taarifa zinazokuhusu
• Gonga “Get Started”
• Weka jina lako kamili, anwani, namba ya simu na barua pepe
• Bonyeza “Continue” → “I Confirm” → “Save”
• Mwisho, bonyeza “Finish”
Mara tu unavyomaliza:
Utaanza kupokea email alerts kila taarifa zako zitakapotafutwa au kujitokeza Google. Hii inakupa fursa ya kujua nani anatafuta nini kuhusu wewe — na hatua za kuchukua.
BONUS TIP: Unataka kufuta matokeo maalum yaliyo tayari kwenye Google?
• Tafuta taarifa inayokuhusu kwenye Google
• Gonga alama ya dots ⋮ upande wa kulia wa result
• Chagua “Remove result”
• Chagua sababu (mfano: "ni ya binafsi", "ni ya zamani", nk.)
• Jaza maelezo na bonyeza “Send”
Google watapitia ombi lako na kukujibu kwa email kuhusu hatua watakazochukua.
Kwa nini hii ni muhimu?
• Inaweka taarifa zako binafsi salama
• Inazuia matumizi mabaya ya taarifa zako na matapeli
• Inakupa udhibiti juu ya kile ambacho dunia inakiona kuhusu wewe
Usikae kimya!
Drop something on my account
nisapoti.com/Maleko

kama umejifunza kitu leo.
Please share kwa ndugu na marafiki wanaojali usalama wao mtandaoni.

#FaraghaMtandaoni #TechTips #GoogleHack #DigitalPrivacy #OnlineSafety #DataProtection #MalekoStyle #KamaBure
 
Hii ni Elimu muhimu sana kwa Watu wote kabisa katika Jamii.

Cyber Security and Criminology.
 
Back
Top Bottom