Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Unamkumbuka afande Sijali pale Masange Tabora na majaruba??Op Kizota Chale coy unaamka saa kumi kufagia giza hata kuona uoni nani anakumbuka uwanja wa embakassi bonge ya shamba??je alizeti??je kubeba mtulinga??mwisho pombe ya wanzuki na karanga duh mwenye op kizota ni pm tafadhali
 
Du hizi kali kweli:
Mie nakumbuka nilikuwa Ruvu JKT sikumoja tulikuwa tunatoka kule Phase 2 kwenye bustani tuaanza kuimba nyimbo kama kwaida;
sasa tukabadili mistari ya nyimbo tukiimba:
Sisi makuruta tunapenda mboo, mboo,... mboga za majaniiii!
Tunapenda ****,.. ****,... kumaliza jeshiiii!

Basi bwana afande akainyaka akatusimamisha- Siku hiyo siatisahau maana tulikula kwata mpaka bukta zikachanika. Wengine mpaka wakazimia ilikuwa balaa.:msela:
 
Namkumbuoka Commanding Officer Adam Mwakanjuki Makutupora 1976. Alikuwa akitupoza kwa pombe za kienyeji zilizopikwa hapo hapo kambini siku za sikukuu.
 
Wa Bulombora mpo?

Operesheni Kagera (Zamaani, 1979!). Nawakumbuka akina Sajenti Chwa wa kombania F(?) Huyu walikuwa wanatusimulia kuwa likuwa mkali sana na aliletwa hapo Bulommbora kwa kuwa alimhenyesha kuruta mmoja hadi akafariki dunia, kisha akataka kuficha kwa kumuweka kwenye gunia! (Ila naamini huenda huu ulikuwa ni uzushi - labda waliokuwa Oljoro watuambie).

Namkumbuka Koplo Kova na Koplo Ofinyo - Kwata kwa kwenda mbele. Na wale magreen kwanja nao walikuwa balaa.

Ila nakumbuka kwa masikitiko sana kifo cha kuruta mmoja ambaye aliumwa na koboko wakati wa kuokota kuni. Tulikaa usiku saa mbili, kamanda wa kombania (Luteni Albano Helandogo) akasema: haya! weka chenja!! Mana yake imbeni. Wakati huo ilikuwa ni kuimba nyimbo za kusifu CCM na kumlaani Nduli Iddi Amin na kusema kuwa tuko tayari kung'oa! Kisha akasema kuwa tusishangae sana kwani kufa si ajabu na ingekuwa ni kitu cha ajabu kama kuni alizoenda kuziokota zingemvunja jicho, lakini kufa si ajabu - haya! weka chenja! Na kesho kuni kama kawaida!!

Ila pia nakumbuka kwa furaha sana jinsi tulivyoweza kuishi kama kitu kimoja. Haikujalisha kama wewe ni Compulsory (form six, mwalimu, daktari, etc. ambaye umejiunga kwa mujibu wa sheria) au ni Volunteer (darasa la saba ambaye umejiunga kwa hiari). Wote tuliishi kama kitu kimoja na mwisho wa kujua kama unajua kusoma au kuandika ilikuwa ni kuhesabu "moja! mbili, tatu, moja!!!" Pia nakumbuka sana kutoroka (kujongomea) kwenda kwa chinova (mashamba ya mahindi mabichi), ziwani n.k.

Hivi kuna anayekumbuka matani ya JKT - kama kuruta aliyeulizwa "wewe kuruta, mbona huli?" akajibu, "sina appetite afande" afande akang'aka "hayo ndiyo matatizo ya kujongomea, wenzio tuliwagawia appetite juzi, wengine walipata mbilimbili, sasa wewe itabidi usubiri hadi tuagize makao makuu"!!!

Kwa wale dada zetu waliokuwa wana aibu ya kuonyensha miguu yao, kulikuwa hakuna kujifunika khanga - wote ni usawa wa bukta (ila zao zilikuwa na mpira mapajani!!

Jamani JKT iliuwa raha tupu!!!
 
Aaaaaaah Mkuu unatuumiza sisi tulioukosa huo uhondo ingawa wavivu watasema hakukuwa na lolote la maana lakini ukweli unabaki pale pale kwamba JKT ilikuwa ni sehemu moja nzuri sana ya kufundishia uzalendo kwa nchi yetu. Shetani hawa sijui kwa nini waliondoa kitu hii.

Sisi tuliomaliza shule miaka ya '90 tulikosa kabisa nakumbuka sisi wakati huo tulikuwa LITI Morogoro tukaishia kujaza fomu za kwenda Jeshini na tulikuwa tumekamilisha kila kitu na kupangiwa kabisa kambi za kwenda kuripoti mwezi Januari 1995. Aah! Ghafla bin Vuu jeshi likafutwa kwenye Bunge la 1994 sikumbuki mwezi wa ngapi vile.

Nakumbuka mie nilikuwa nimepangwa kwenda kuripoti Mlale JKT Songea!! Na nilikuwa nimejiandaa kikamilifu kwenda kupambana kwenye shamba lao walilokuwa wanaliita DUNIA. MUNGU wangu kwa nini nilikosa hii bahati? Na mipango yangu yote ikavurugika maana nilikuwa nimepanga mara nimalizapo JKT ningebaki huko huko Jeshini (yaani JWTZ) sijui ningekuwa wapi sasa hivi!!

Any way yote ni maisha!! Hongera yenu mliobahatika kuhudhuria hayo mafunzo!!
 
Na vile vinyimbo navyo???

"Upatapo dishi lako, usawa wa kombania, ole wako ukifumwa usawa wa gudulia!!!! Viongozi wa siasa, imarisheni chama, watakaochaguliwa, imarisheni chama!!!

Mnakumbuka kunyakua kwenda usawa wa gudulia? Ilikuwa ni juhudi zako. Halfu sasa wagawaji wa dishi walikuwa na nyodo - anaweza akakuangalia akakupiga (akapakua) kwa angle ya mustini!

Ila baada ya hapo, kuna renew au basti!!!
 
Bubu Msemaovyo,

Hivi Rwekaza hakuwa kwetu Danger Coy?

Huyo afande aliyemuuwa tulikaa naye jela kwa siku zaidi ya ishrini. Nakumbuka wakati anaingia jela alitutishia tukatoka mkuku. Alipotupa story ya tukio zima tulimuonea huruma. Nasikia siku ya kutoa heshima za mwisho afande Mlay aliilaumu maiti na kusema amekufa kifo cha aibu sana.

One leg unamkumbuka?

Nasikia marehemu alikuwa anakula makuruta kwa njia ya kipopo bawa.
 
Mmenipeleka RUVU JKT,(program ya chama) 1988/1989 EAGLE COY, jamani mpo? nakumbuka nilijongo kwa muda kama wa miezi mitatu hivi, niliamua niache kabisa kwani maisha yalielekea kunishinda, lakini kila nilipokuwa nakutana na watu mitaani walikuwa wananiuliza vipi si ulikuwa jeshini wewe?

umeshamaliza mara hii! hali hiyo ilikuwa inaniumiza sana hasa nikiona kuna baadhi ya kina dada ambao walishapitia na kumaliza mimi mwanaume mzima nikimbie? nikaamua kurudi kambini lakini kasheshe sijui jamaa watanipokeaje, kama kawaida nikapanda basi toka Dar hadi Mlandizi jioni ili niingie usiku kambini, kumbuka huwezi tumia njia ya kawaida kama ulijongo, kwa usalama wako ni lazima utumie njia za panya, na tayari giza liliisha ingia na kumbuka RUVU kuna historia ya SIMBA,

nimekwenda vizuri mpaka nakaribia kambi ghafla nasikia mshindo mkubwa upande wangu wa pembeni, yaani nilikimbia kama sina akili nzuri, kumbe walikuwa ni nguruwe mwitu nao wananikimbia, bahati nzuri nilifika salama kambini, kasheshe ikawa nitaingiaje na jamaa wakiniona watanipokeaje! nilikuta wenzangu wako kwenye disco,

nikanyemelea mpaka nikaingia kwenye hanga, nikamkuta rafiki yangu mmoja ile kuniona tu hakuamini kama ni mimi kwani alisema jamaa walikuwa wananitafuta kama mwizi nikataka kutoroka tena lakini nikikumbuka ile njia niliyotumia nikaishiwa nguvu nikaamua kubaki, habari ikawafikia kuwa nimerudi basi walishindwa wanirarue vipi,

walichofanya ni kumwita MP KAMANDA aje kunibeba nikahenyeshwe mahabusu, watu walijua nimekwisha! lakini cha ajabu huko ndiko niliko pata shushu ambayo sikuitarajia, nikaona ni bora nisirudi tena kombania!
 
Hakuna Mjasiliamali moja akusanye stories hizi kuziedit na kutoa kitabu?

Zinafurahisha sana.
 
Story nzuri nimezisoma zote, though in a way kwa sisi mabinti naona ingekuwa tabu kidogo, kwahiyo tabia ya ufuska ya hao maafande, hivyo though I didn't go thru that..am glad I can read about it, compile stories mzalendo Mtsimbe

Kisa cha mhindi kimeniacha hoi, ;d
 
Duuh! Hii kali sana.

LOL.

Respect.

Huyo afande Mlay alikuwa ana vituko! Ukisimuliwa habari zake jasho litakutoka. Mimi ndiye aliyenifundisha kujitwika gunia la mahindi begani kwa mara ya kwanza. Nakumbuka tulikuwa jela ya kijeshi tukapelekwa Mufindi kwenda kupakia mahindi ya afande Mlay. Mimi walivyotaka kuniwekea gunia begani nikajitetea kwamba sijawahi kubeba. Akanifokea na kunitaka niweke mgongo sawa wanipachike gunia. Wakanipachika nikastukia naweza na kuendelea kupakia
 
Mzalendo Yoyo, share with us . . . Ni nini hasa unakumbuka tufurahi wote?

Nilipata kusikia kwa walioenda JKT walikuwa wakitoroka na wanawake kisha wanalala pamoja bila hata kufanya MAVITUZI ni kweli?

Hivi kwa hali ya sasa, inawezekana kweli?
 
Nilipata kusikia kwa walioenda JKT walikuwa wakitoroka na wanawake kisha wanalala pamoja bila hata kufanya MAVITUZI ni kweli?

Hivi kwa hali ya sasa, inawezekana kweli?

Mkuu Jeshini tulikuwa tunavaa Pitshort, Unapopewa Hiyo kitu ikiwa mpya inakuwa ndefundefu ukishafua mara moja inaruka kama nini, sasa siku za kuvaa hiyo kitu wadada huwa nusu kuvazi. Siku moja nakumbuka tilikuwa na wadada marafiki, tukaenda kwemye kazi kama kawaida, kazi yenyewe ilikuwa ni kufyatua Tofali, Tofali 500 kwa siku, sasa ukiwa na Familia unafanya kazi mara mbili, manake tofali 500, Zakwako na Za mwenzako 500, Unajua ilikuwaje siku hiyo, Baada ya kumaliza hizo Tofali 1000,Ilikuwa Hoi, kwenda kulala maporini chakali, Kwenye kuoga?Mnaoga kama wote wanaume tu, Hoi.
 
Mkuu Jeshini tulikuwa tunavaa Pitshort, Unapopewa Hiyo kitu ikiwa mpya inakuwa ndefundefu ukishafua mara moja inaruka kama nini, sasa siku za kuvaa hiyo kitu wadada huwa nusu kuvazi. Siku moja nakumbuka tilikuwa na wadada marafiki, tukaenda kwemye kazi kama kawaida, kazi yenyewe ilikuwa ni kufyatua Tofali, Tofali 500 kwa siku, sasa ukiwa na Familia unafanya kazi mara mbili, manake tofali 500, Zakwako na Za mwenzako 500, Unajua ilikuwaje siku hiyo, Baada ya kumaliza hizo Tofali 1000,Ilikuwa Hoi, kwenda kulala maporini chakali, Kwenye kuoga?Mnaoga kama wote wanaume tu, Hoi.
Duu mkuu umenifurahisha hapo kwenye bold & red. kumbe ulikuwa unanyung'unywa mara mbilimbili kwa sababu ya kuwa na familia - wadadamarafiki?!!!!
 
Ah inimekumbuka mbali! Mie nilikuwa Bulombola operation miaka 30 ya uhuru! Nakumbuka kisa kimoja nilivyo danganywa na wavuvi wa dagaa pale kijiji cha jirani. Tulikuwa na kazi ya kukata magogo ya kuchomea chokaa! Basi tunaamka alfajiri tunawahi porini. Siku moja wakanitokea wanakijiji wakaniambia kuwa huwa wananunua magodoro toka kwa makuruta kwa bei ya shs 800. Duh kuona hivyo tamaa ikaniingia, kichele wakati huo ni 300 au 400 sikumbuki vizuri. Nikawaambia nitawaletea kesho yake. Basi usiku huo nikafanya mpango na storeman wa kombania yangu ya C akiitwa Samiza Samizi, jamaa kanipatia godoro moja kwamba tutagawana pesa.

Nakumbuka niliamka alfajiri sana yapata saa kumi ili jamaa wasinistukie. Nikabeba godoro mwendo wa kama km 4 kupitia porini ili nisikutane na maafande waliokuwa wamelala vijiji kwenye pombe. hatimae mzigo nikaufikisha salama nikauficha mahali. Yapata saa nne mteja wangu kaja. Nilipomuonyesha kasma godoro limezeeka sana hawezi kuchukua. Kumbe alijua sina pa kulipeleka. Mwishoni kabisa tukafika bei. Akanipa sh 50/-! Yaani nilikoma. MAtumaini yangu yoyr ya kupata shs 800 nikaambulia shs 50/-! Siwezi kusahau!
 
Back
Top Bottom