Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Aisee, jeshini tulijifunza mengi. Mimi operesheni OKOA, nilikuwa kambi ya Oljoro. Nakumbuka mambo ya kutoroka asubuhi subuhi mkienda bustanini kumwagia, basi unakuwa umeshafungasha kamzigo kako, unakitoa unakatisha msituni hadi barabarani njia panda (mwendo wa mbali), then unadandia magari ya mchanga yanayokwenda Arusha mjini, ukibanana na wamasai.
Shida ya kutoroka jeshini (kuondoka bila pasi kutoka kwa CO), ni wakati wa kurudi, inabidi kufoji vyeti vya hospitali au vya kuitwa for interviews za college, kidogo hii ilisaidia.
Jeshi lilirudi bwana, lina raha na karaha zake LOL
 
Nimekumbuka mbaali kweli hadi machozi yanatoka duh, MIE Nilikuwa "OLJORO JKT"-arusha. Miaka ya 1994, OPARESHENI "OLJORO" mkuu wa kambi alikuwa "col NANDONDE[RIP] nimekumbuka yale mashamba makuuubwa ya "DUNIA NA EMBAKASSY" pia kule shimo la mungu kwenda kutafuta kuni bila hata panga. Lile shimo lina maajabu kwelikweli. Bila kusahau kule Mirongo minne kutafuta kuni na ku-chat na watoto wa kimasai. Mie nalikuwa "chale coy" tulikuwa na saa meja MADUMA mkali kwa kwata tukiamshwa saa 9 usiku kupiga kwata. Yapo mengi saana ila namalizia kwa "mwendo wa kunyakua usawa wa gudulia la ugali" up...up...up...up...up....up....[akikosea mmoja mnaanza upya] kweli zamani hairudi tena. Miaka ile hapakuwa na simu hivyo marafiki wote tulipotezana ...
 
Umenikumbusha mbali sana mie niliudhuria ile miaka ya mwishoni ya themanini (1989/90) Pale kambi ya Ruvu kombania ya B kuna afande alikuwa anaitwa Nyundo. Huyu afande hatukubahatika kumuona akiwa amefurahi kila siku sura yake ili kuwa ya kazi kazi. Mwenyewe alikuwa anajiita ndio handsome wa kwao.
Nakumbuka moja ya wimbo ambao alitufundisha muda wa disco ulikuwa wa Malela.... na mwingine ulikuwa nadhani wa kishona kama sijakosea unaitwa Kule kule kwa chinoma....
Kitu kingine nakumbuka ni ufugaji wa kuku kule phase 2 pamoja na kusimamisha minazi serengeti muda wa jioni.

Mimi nilkuwa hapo kombania D kuna mtu alikuwa anaitwa afande Mazani huyu bwana kwa toos alikuwa nia hatari nadhani historia yake unakumbuka ilikuwa inavuma kambi nzima.
Alafu nakumbuka tulikuwa tuaamka usiku kula kiporo cha wali maarufu kama "Kijogoo" pila jeshini tuliwaza hata kula mayai mabichi bila wasiwasi kitu ambacho huwezi kufanya hivyo leo hii.

hayo ndio nayakumbuka
 
Hivi jamani zile kambi za Bulombora, Masange, Mlale, n.k. bado zipo?

Labda tujadili wazo la kufufua tena JKT, kuna yeyote ambaye ana habari za uhakika juu ya programu hii? Mimi naona itakuwa ngumu sana kwa sababu ya itikadi za vyama. Isije ikatumika kueneza ideology badala ya "nation building"
 
Mmmh!

Namkumbuka afande Mlay wa Buhemba na dettach ya Lwamkoma . . .

Ilikuwa ni kupalilia miraba ya pamba kwenda mbele. Huoni mwanzo wala mwisho wa shamba.

A worthwhile experience.
 
very interesting story....JKT...BUt i wonder kama uzalendo ulifundishwa....UADILIFU KATIKA KUJENGA TAIFA NOW NI ZERO..Y???????????
bora wameifuta
Story nzuri nimezisoma zote, though in a way kwa sisi mabinti naona ingekuwa tabu kidogo, kwahiyo tabia ya ufuska ya hao maafande, hivyo though I didn't go thru that..am glad I can read about it, compile stories mzalendo Mtsimbe
Kisa cha mhindi kimeniacha hoi, ;d
ni kweli dada yangu, na sasa hivi magonjwa yalivyoshamiri ili hali tabia za watu zinazidi kuwa mbaya
Je wadau? Kulikuwa na sababu yoyote ya msingi ya kufuta huu utaratibu wa JKT, eti magreatthinkers?
ni bora wameufuta na wanaonganganiza urudishwe ni vichaaa
 
Kule Kisimani mama sitakwenda tena
Matumbili na Manyani yanaogelea . . .
Embeee, embe mamaeee,
Eeembee embeee mama eeee!
 
It was good, really. Miezi 3 ya mwanzo migumu, baada ya hapo mnaishi kifamilia zaidi, mnawazoea na maafande, muda wa kuondoka ukifika mnafurahi kuondoka lakini mnasikitika kuondoka. Huwa natamani ingetokea tena tutangaziwe kurudi japo mwezi mmoja mmoja kila operesheni kwenye makambi yetu.... Mliokosa jeshi hilo mlikosa mengi mazuri, mateso yalikuwepo lakini mwanzoni ambayo sehemu yoyote unapoanza kitu ugumu huwa upo.
 
JKT ilikuwa safi sana hasa nakumbuka vituko vya wale form 7(maafande wa kwata) na mwendo wa kunyakua hasa wakati wa kwnda kula.

Ninachokumbuka zaidi ni afande mmoja alimtokea binti na wakakubaliana, walipofika faragha binti akakuta afande an "fore skin", akamwambia afande wasifanye chochote la sivyo angepiga kelele. Akamwomba afande akaondoe hiyo kitu na kidonda kitakapopona atampa bila shida. Afande akakubali akaenda kukata, akazembea kufanya dressing, akawa anatoa harufu mbaya. Akaniomba nimsaidie ili apone, maana nilikuwa pale kama tabibu, kwenye zahanati ya Kikosini. Nikamsaidia kwa dressing mpaka kidonda kikakauka vizuri. Bahati mbaya wakati afande anapona na muda wetu ukawa umekwisha na binti akaondoka,afande akawa amemkosa ila alifaidika na kutahiri akiwa na miaka 40!
 
Afande Justo wa OLJORO na mkwara wake wa KWATA....Pia shamba almaarufu DUNIA...unaangalia mraba wa kupalilia huoni mwisho........Kuchonga matofali toka mwamba laini kwa Mzee Shabaan.....Hakika ulikuwa mwaka wa aina yake...Pamoja na ukakamavu nilijifunza kuwaza haraka sana hasa katika kutengeneza UONGO kujiokoa kwenye mikono ya maafande pale ukutwapo usipotakiwa kuwa🙂
 
Nakumbuka nilikuwa Makutupora JKT, Operation Kambarage.
Nilikuwa Kombania B (B-Coy) Chini ya Koplo Mwashamba.
Kipindi hicho Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi alikuwa ni Dr. Salim Ahmed Salim.
Pale tulikuwa na mtoto wa Mh. Rashid Mfaume Kawawa (RIP) aliyekuwa akiitwa Mariamu, pia tulikuwa na mdogo wake Dr. SAS aliyekuwa akiitwa Abbas.

Ile mwanzo mwanzo tu huyu Mariam, alikuwa akinata nata loooh kwahakika aliipata fresh na baada ya wiki 2 akanyookaaaaaa! Ila Abbas alikuwa bingwa wa kazi alikuwa anakata Kuni za Mitunduru, zigo la kufa mtu na Maafande wakampenda mno japo umbile lake lilikuwa ni legelege.

Baadaye nilikatwa Bogi kwenda Chita, ambako nilitumika hadi Juni Kumi na Tano mwaka ulofuata nika-passout. Nakumbuka tarehe 3 ya Januari mwaka niliopass-out tulienda Uchaka, na nikapangwa na mabinti 2 ili kuchimba handaki na kulala 2 ndani yake na mmoja akiwa mlinzi nje. Nawakumbuka mabinti hao ni; Zena Amiri (Dip ya Ualimu) na Tabu Manyirizu ( Toto la Kisukuma).......

Ama kwa hakika hii imenikumbusha mbaaliiiiiii.
 
Mlale JKT, nawamiss sana afande undunduundundu, huyu alikuwa RSM, alikuwa akipenda kutoa adhabu ya kibatabata, kuna pia afande mmoja akiitwa Mange K, huyu alikuwa bingwa wa kwata ya Singe, sauti yake ilikuwa kali utadhani chiriku.

Kuna matukio kama ya kuzima moto, hakika haya yalikuwa yanaudhi kweli kweli, mnaamshwa saa tisa usiku, mnazima moto upande huu, mkirudi wakati usingizi ndo unaanza kushika kasi, mnaamshwa kwenda kuzima moto upande mwingine, sometimes umbali wa zaidi ya km 2.

Kuna jamaa alianzisha wimbo wenye utata akapigwa dosodoso ile mbaya, wimbo wenyewe ulikuwa kama hivi, 'TUNAPENDA KUMAKUMA, KUMALIZA JESHI x2'halafu wengine mnatitikia hivyo hivyo, mwanzoni afande alikuwa hakuelewa lakini ilipokuja beti ya pili ndiyo akashtuka.
Beti ya pili, 'TUNAPENDA MBOOMBOO MBOGA ZA MAJANI x2' hapo kila mtu akaangua kicheko, afande akamwambia jamaa hebu rudia mbona wenzako wanacheka, ile kurudia wimbo ilikuwa balaa

Du vituko vilikuwa vingi unaweza maliza mwezi kwa kuviandika.

Enzi hizo CO alikuwa Kanali Mtono (Marehemu), huyu bwana alikuwa mjeshi kweli kweli, sio hawa wa siku hizi na kuku wa kisasa.
 
Mafinga JKT Operation Miaka 25 (1988/89) i realy miss you. Danger coy mko wapi wakuu? Kayange, Double P, Chalamila, Nyaulingo where are you guys? Namkumbuka Sir Major Mulembo akimfokea Kayange:
Afande Mulembo: We Kuruta unajifanya mjanja sana eeh?
Kayange : Kimya
Afande : mimi ninakuuliza wewe unanyamaza Kimya?Afande akikuuliza "unajibu ndiyo afande"
Kayange: ndiyo afande
Afande : unajifanya mjanja sana?
Kayange : Ndiyo Afande
Afande: pumbafu zako
Kayange: ndiyo afande
Afande: Unatuona sisi ni wajinga sana?
Kayange: Ndiyo afande
Afande: ( akiwa amekasirika) Unatuona sisi wapumbavu sana?
Kayange: Ndiyo afande

kombania tukashindwa kuvumilia tuaanza kucheka tukala push ups wote kwa kucheka huku bado akiwa hajui kuwa amem-limit Kayange kujibu 'Ndiyo afande' hata kwa negative statements.
 
baadhi yetu pale Ruvu tuliona bora twende kwenye timu ya mpira kwani huko kuna shusi kidogo. tukawa kuruta kibao wote tunataka kuwa wachezaji. siku ya siku akaitwa afande mwihava na kesi wakaambiwa waongoze mazoezi ya viungo, kukimbia uwanja. tukaanza kuzunguka uwanja kuanzia saa 10 jioni. wengine tukawa tunahesabu round. mimi niliacha kuhesabu ulipofika raundi ya 40! nilishachoka hoi. na jamaa atakayeshindwa kwenye kukimbia anafukuzwa hakuna kurudi tena kwenye mpira. tulikimbia mpaka saa 12.30 byugwa lilipokuwa linapulizwa! tulikuwa hoi bin taaban. kuna jamaa mmoja adolph alipotoka uwanjani akakuta bomba la maji pale karibu na hospitali. akainama kulowesha kichwa. hakusimama. alianguka chini na kuzirai pale pale. bahati nzuri ilikuwa ni hospitalini wakamwingiza na kulazwa! iliuwa shughuli pevu. kesho yake tuliorudi mpirani tulikuwa wa kuhesabu, tumeshajichuja wenyewe!
 
Naomba hii thread musiiondoe kwani inafurahisha na kukumbusha mambo ambayo leo hayapo. Pili najiuliza jkt ingekuwepo bado na huu ukimwi uliopo sijui ingekuwaje kwa wasomiwetu hawa.
 
Back
Top Bottom