Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

yes amiri nondo nilimwona kawa meya! alikuwa na mshokaji wake madenge. nadhani nilisikia madenge amefariki. sijui kama ni kweli, dah!

yes hata mimi nlisikia madenge alifariki. hope utakua unajua co urio alifariki siku nyingi. nasikia hata akina nyundo na kibuyu walikwisha tangulia mbele ya haki. lkn sina hakika kwa hao wawili. hivi itakuaje kama kambi zitawaalika wote waliopita ktk hizo kambi kuzitembelea na kukutana na makamanda wao ambao bado wako hai hata kama watakua wameishastaafu?
 
Mmmh!

Namkumbuka afande Mlay wa Buhemba na dettach ya Lwamkoma . . .

Ilikuwa ni kupalilia miraba ya pamba kwenda mbele. Huoni mwanzo wala mwisho wa shamba.

A worthwhile experience.
Rwamkoma farming unit!!!....namkumbuka afande shekigenda na baiskeli yake imeandikwa "Let them say-Sheki"
bila kumsahau bah,na saa meja machachari saana muarusha nimesahau jina lake!
 
nakumbuka mgulani JKT, na kutoroka kwenye matundu ya senyeng'e, wee acha tu! asubuhi subuhi watu mko mtaani, giza likiingia you are back in the camp bila nomaa
 
DUH!.....nimemiss sana jeshi,naomba mtu mwenye picha ya combania D ya rwamkoma buhemba,tulienda butiama tukapiga picha na JKN.....please pm me,operesheni miaka 30 ya uhuru!!
ndolilo ndolilo,amba ndolilo!
Bogolosi...vanjoo...ha ha ha!
 
nakumbuka mgulani JKT, na kutoroka kwenye matundu ya senyeng'e, wee acha tu! asubuhi subuhi watu mko mtaani, giza likiingia you are back in the camp bila nomaa

Nilikuwa hapo wakati RSM Kitomali . ingawa mimi nilikuwa Shuleni kule kwa Lt Col Massawe.
 
yes hata mimi nlisikia madenge alifariki. hope utakua unajua co urio alifariki siku nyingi. nasikia hata akina nyundo na kibuyu walikwisha tangulia mbele ya haki. lkn sina hakika kwa hao wawili. hivi itakuaje kama kambi zitawaalika wote waliopita ktk hizo kambi kuzitembelea na kukutana na makamanda wao ambao bado wako hai hata kama watakua wameishastaafu?

Nimemkumbuka sana CO Ruvu Lt Col Urio, Meja Chota, Mkuu wa Hospital Meja Omar, Ndugu angu CI Capt Othman, capt Nakuchema, Capt Nyoni.

Vipi akina Sir meja Urassa, Basekana, Mazani.

Ruvu ilikuwa Ruvu kweli enzi zile ingawa nilikaa muda mfupi.
 
Maisha ya jeshi yana mvuto wake pindi ukutanapo na ulokuwa nao jeshini hukufanya ukumbuke vituko vya huko na siku huwa nzuri. mi nilikuwa makutupora miaka 30 ya uhuru, A coy. disco kwa sana, sisi hatukuwa tukiteswa kwani sir major wetu alikuwa anatukingia kifua, kimbembe B coy afande mwashamba alikuwa anawatesa vibaya. Nakumbuka siku moja tukiwa ktk kwata afande huyo akampa jamaa pushaps kisa mguu pande mguu sawa yake ni kama mbwa anakojelea kisiki, Walahi alipotamka hivyo tulishindwa kujizuia tukacheka.Mambo yalikuwa poa.
 
Dah! umenikumbusha mbali sana mkuu..1991/92 op. vyama vingi..Makutupora A-coy tulipangwa kumwagilia bustan.. Lakini baadae tukahamishiwa Bulombora, D-coy. Namkumbuka afande Mnzena, Mtekere, afande Sezero, coplo Ngoma, afande Mbewa na afande machachali mikwara mingii Stanslaus Makoba ''kadebra'' baiskeli yake iliandikwa ''sereuka mwana wa ndege..mnafiki hakosi sababu'' Kombania hii kulikuwa na vijana akina Robert Nyamhanga, Prudence Timanywa, Mongu Manumbu, Mpemba Francis, Safari Lucian, Redemtus Shoto, Privatus,Anterius Sostenes, Joe Kihampa (TBC1) na wengine. Akina dada kulikuwa na Kore Ally Sadick, Rose Manyama, Judith Schirima, na wengine wengi. Nakumbuka umoja, ushirikiano wa kusaidiana kuepuka visanga baina ya makuruta nk. Siku tukipokea ''kichele'' tulikuwa tunakwenda kijiji cha Kaseke kutumia. -J4 wa D-coy
 
Mafunzo mazuri ya ukakamavu lakini mbali ya hilo sioni zuri lilikuwepo JKT. Bullying, uonevu na raping in all but name. Kwa waliokuweko Mafinga (Nguvu Kazi - 1983/4) D-Coy watawakumbuka Commando, Mpogole Mpilano Nico Kimbunga na wengine. Yes, the disco bit and night time comical stories were enjoyable. Unaweza kuangalia nyuma ukasimulia kama entertainment - lakini if I had to do it again, I certainly would never want to. Pamoja na kilimo kilichoshamiri nilishangazwa nipilosikia kuwa JKT ilikuwa bado inahitaji msaada wa chakula toka serikali kuu. Hakika ulikuwa ni upotevu wa resources na muda wa watu wengi ambao ungaliweza kutumika kwa mengi mazuri.
 
Mdau wa 838KJ Maramba kanikumbusha..

Shamba la Ghuba ya Uajemi... mnaamshwa saa 10 usiku na kupangiwa miraba.. kutokana na giza mnalima tu na ku - guess msitari wa mahindi..ikifika asubuhi unakuja kugundua msitari ulioacha umenyoka ni majani na siyo mahindi...

Kila nikiona mabaharia nakumbuka wapishi wa kombania..walikuwa wanaitwa mabaharia kutokana na kubembea na mwiko mkubwa..ila ukiwa na rafiki Baharia ..basi lazima jioni utapata maharage yenye mafua..

Ukiwa na rafiki yako wa kike ..kila mtu anajua siku akienda period kwani.. mabinti wenye "B" za matron walikuwa wanaitwa mbele kila asubuhi..wanapigishwa kwata ya kiushikaji na kupewa light duty..sana sana kupika Sergeants' Mess..hivyo kwa wiki hiyo unapumzika kufanya nanihii lakini unafaidi maharage ya mafuta toka Sergeants' mess..

Mpaka sasa sijajua kwa nini maafande wakitaka msitari unyooke wanasema "Kabalov"

Siku za kulinda "Guard" unakuwa msafi kuliko Bwana Harusi..Kombati unalalia wiki nzima ili iweke inyooke..hakuna kupiga pasi..

Kwenye Platoon yangu nilikuwa nashindana na afande kufukuzia binti..hivyo platoon nzima ilikuwa inapata adhabu kila huyo afande anapokuwa zamu...push up za nguvu kila siku.... Extra drill na Guard toka kwa huyo afande nilishazizoea..hadi Ma MP wapigishao extra drill Main Gate ..walinizoea nikaanza kuwapa sigara wakawa washikazi ..

Kutoka ukuruta kwenda service man ni sikukuu ya nguvu..biashara ya kombani ya kuuza mihogo ilileta faida ambayo ilitumika kununua pipa moja la pombe ya Mnazi..

Ni hayo wadau ..toka Operesheni vyama vyingi...
 
:majani7:Jamani Mgambo Kabuku mnapakumbuka? Namisi sana mihogo ya Gendagenda. Siku ya mziki ilikuwa mwisho wa mwezi wakati tunapokea alawance kunakuwa na mauzo ya pombe ya kienyeji ndani ya holli (mradi wa kombania) oooh I miss Boha. nakumbuka mchakamchaka wimbo unaosema Iddi amini alifa mimi siwezi kulia, nitamtupa Kagera awe chakula cha Mamba:majani7:. JKT oyyeeee!! Hawa vijana wa sasa wa Dot Com wanahitaji kweli wapelekwe huko wakajifunze maish
 
yes hata mimi nlisikia madenge alifariki. hope utakua unajua co urio alifariki siku nyingi. nasikia hata akina nyundo na kibuyu walikwisha tangulia mbele ya haki. lkn sina hakika kwa hao wawili. hivi itakuaje kama kambi zitawaalika wote waliopita ktk hizo kambi kuzitembelea na kukutana na makamanda wao ambao bado wako hai hata kama watakua wameishastaafu?

Mkuu timbilimu, tulikua kombania moja F ya afande Mnyomole, Sanga,
Rajab, mahingu,kaumbu na volvo ROCKY, tafadhali ni PM tufahamiane zaidi.
Hssan Mdenge(RIP) nilikutana naye mara ya mwisho nakumbuka 2000 akiwa
Mhasibu pale wizara ya sayansi na elimu ya juu.
Mpo wapi Athmani Juma Mlinga, Alfayo Ngoma,Bahati Nyamwesa,, Minza msengi,
Emson Malick, Safina Maloya Kombo(mama),Nunu Hamisi, Ali Mwankenja,
Lucas Mwaipyana, Adili Sheusi,Manyama Matoke,Tedy Lyamuya,na wengine wote?
 
MtemiwaWandamba ntaku PM! Umenikumbusha akina dada Minza Msengi na Nunu. Sijui wako wako wapi? Tedy Lyamuya yupo NSSF dar,lakini sijui tawi gani. Sheusi aliendaga Marekani.
 
Kweli kifo cha Abrahamu Maji kilisikitisha sana. Wengine nawakumbuka ktk kombania yenu ni akina John Mongela na Evarist Mashiba! Kuna mshikaji tulikua nae hapo F coy akiitwa Amir Nondo siku hizi ni Meya wa Manispaa ya Morogoro!

Mkuu hao kina Mongela na Mashiba walikuwa Eagle Coy nafikiri.
 
Nilikuwa nachukia sana mchakamchaka hivyo nilikuwa naukacha sana. Jamaa wakiwa huko kwenye mchakamchaka kila mmoja anapewa namba ili kuwanasa wasiokimbia. Sasa wakisharudi sisi ambao hatukukimbia tunajipachika kwenye foleni halafu afande anawaita watu kwa namba, unafunga mguu (una-hot) na kusonga mbele. Mara nyingi nilikuwa na-hot kwenye namba ya mtu mwingine aliyekimbia mchakamchaka na kumponza, kwani wote mnapigishwa push-up za nguvu. Lakini maudhi yalikuwa siku ambayo umekimbia mchakamchaka halafu jamaa mwingine ambaye hakukimbia ana-hot kwenye namba yako.
 
:majani7:Jamani Mgambo Kabuku mnapakumbuka? Namisi sana mihogo ya Gendagenda. Siku ya mziki ilikuwa mwisho wa mwezi wakati tunapokea alawance kunakuwa na mauzo ya pombe ya kienyeji ndani ya holli (mradi wa kombania) oooh I miss Boha. nakumbuka mchakamchaka wimbo unaosema Iddi amini alifa mimi siwezi kulia, nitamtupa Kagera awe chakula cha Mamba:majani7:. JKT oyyeeee!! Hawa vijana wa sasa wa Dot Com wanahitaji kweli wapelekwe huko wakajifunze maish

............... Mafinga kwa TN MLAY, mfupi kama DANNY DE VITO ! shughuli yake ............ wee acha tu ! tuligoma kombania nzima ! ............... ebanaeeh ! .......... tukaambiwa wanajeshi wameasi !! hiyo shughuli yake sipati kukukambia MP gari MBILI adhabu siku nzima ! kumbe kugoma jeshini ni KUASI !? ................. daaaaah wee acha tuu !
 
duh ... pale Makutupora 1993 operesheni vyama vingi ..... tuliiba zabibu nyeupe nakwenda kuzila mitunduruni ....

very interesting and uncovered now .....rais wa DRC Hon. Joseph kabila alikuwa Combania D....... wala hatukuwahi kujua yeye ni nani ..alikuwa mpole and very social
1993 ........ sio mafuriko lushoto?
 
Nimemkumbuka sana CO Ruvu Lt Col Urio, Meja Chota, Mkuu wa Hospital Meja Omar, Ndugu angu CI Capt Othman, capt Nakuchema, Capt Nyoni.

Vipi akina Sir meja Urassa, Basekana, Mazani.

Ruvu ilikuwa Ruvu kweli enzi zile ingawa nilikaa muda mfupi.

..... Nguvu ya Nyani, Afande Fred Mwakyosi "MzanzibarI" ..................... Kapteni Wazir na Mahakama yake (Mzigua ana Roho Mbaya kaa nini !!) Mafinga hiyo ..................... Mvua si mvua bali Nyahenge !!
 
Back
Top Bottom