Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Nakumbuka mashamba ya Idetelo, detach ya mifugo,kina afande Kingu, john's corner, c ya matron, smart area...
Mi nilikuwa intake ya miaka 20 ya azimio la Arusha.
Tukipewa hotuba siku ya kugawiwa combania,
Nikiwa A-coy.
Hapa tutakufundisha kula mboga ya aina moja kwa mwaka; kushindia kikombe kimoja cha chai.
Nakumbuka tukiwa kitengo cha kupasua kuni jinsi tulivyoweza kuchoma bisi bila moshi kuonekana, na kila mmoja alikuwa na uwezo wa kula mahindi manane ya bisi kwa siku.
Nilimalizia Mlalakua makao makuu ya JKT, enzi za marehemu colonel Msonge aliyekuwa CPNS.
 
Tukiwa na ujenzi wa ghala la kijiji eneo la Kitelewasi,mvua ilikuwa inanyesha kuzunguka eneo la kazi ilhali sehemu ya kazi ikibaki kavu.
 
Duh mwenzenu siku za mwanzo nusu nife njaa chakula cha moto maharage yana wadudu sijamaliza tonge mbili filimbi
 
Duh mwenzenu siku za mwanzo nusu nife njaa chakula cha moto maharage yana wadudu sijamaliza tonge mbili filimbi

Hiyo kwa siku za kwanza mbona ni kawaida! Mestin ya moto, haragwe lina wadudu, umenyoa para dume jike hajulikani wote kuruta tu. Kwanza kuruta sio mtu hatakiwi kusaidiwa, weee! Haya endeleeni na mambo ya huko!
 
Duh mwenzenu siku za mwanzo nusu nife njaa chakula cha moto maharage yana wadudu sijamaliza tonge mbili filimbi

Hiyo kwa siku za kwanza mbona ni kawaida! Mestin ya moto, haragwe lina wadudu, umenyoa para dume jike hajulikani wote kuruta tu. Kwanza kuruta sio mtu hatakiwi kusaidiwa, weee! Haya endeleeni na mambo ya huko!
We ndo yule foxy? Ukiacha hilo jina la kwanza?
 
Tumo mozambique tumo, maputo tisa tisa moja bila ya buti tumo mozambique tumo!
Aisee!
 
Mama jeni! Mama jeni, we mama jeni.
Nyimbo zenu hizo na ile ya
Iddi Amin akifa, mie siwezi kulia, nitamtupa kageqa, awe chakula cha mamba!
Lol. Hapo wote weusi kudadadeki dume ,jike hajulikani.
 
Oh sorry ni majina tu yamefanana na ni jina langu la kweli simjui huyo ulonitajia
 
Nimekumbuka mbali wakuu! Op. Vyama Vingi- 91/92; Kikosi 836KJ, OLJORO JKT, MAKUYUNI subdetach Arusha, Force No XXXX. Mashamba makubwa ya Mahindi Oljoro, Dunia na Embakasi. Sehemu ya kujongo: korongoni.
 
Matangazo yalitolewa kama ORDER
 
Hii kweli imeamusha hisia zangu mwanzo mwisho. Wale wa Hanga La Mawe Butuku, 822 KJ Operasheni vyama vingi, 1993 mpaka 1994. Hebu tuwasiliane wakuu. Maana nikimkumbuka Afande Mazole, Chale,mashenene, WII Chacha,Luteni Richonjo ........................................................orodha ni ndefu CO Akiwa Colnel Ng'umbi. Wajeshi Bwana anaitisha kikao anawambia Kuruta hastahili kuonewa. Akitoka hapo anawa anaitisha kikao cha wakufunzi wakitoka huko moto mtauona bwana. WOII Chacha alikuwa naweza kuamurisha kikosi kizima mkurya yule bwana we acha tu...................... Siku yangu imekumbuka mbali hadi raha
 
Wengine tulikosa jeshi kwasababu ya sheria kuwa ilishafutwa lakini hapo Same Secondary napo ilikuwa kama jeshi tu.
Wengi sana tunatamani hy nafasi ila mfumo mgeuzo ndio umetutesa...Lakini mazingira 2liyopitia JKT tosha...Wale waliosoma Pomerini Sekondari(Iringa) ilikuwa ni JKT namba 2 baada ya Mafinga.
 
Nimekumbuka mbali wakuu! Op. Vyama Vingi- 91/92; Kikosi 836KJ, OLJORO JKT, MAKUYUNI subdetach Arusha, Force No XXXX. Mashamba makubwa ya Mahindi Oljoro, Dunia na Embakasi. Sehemu ya kujongo: korongoni.
Cha ajabu number yangu ya sim naweza isahau lakini si force number, mpaka leo naikumbuka !
 
Nilianzia Masange Tabora Danger COY ya Wella na Busongo, Busongo akisema wewe kama Ni form six yeye ni form seven, Degree normal vidato nothing, Tall water. Nikakatwa Bog kwenda Bulombora nikijua nimemkwepa Wella huko nikamkuta affande Chacha na JD aliyemtengua kiuno kuruta akafukuzwa jeshi. Baadae Wella akahamishiwa Bulombora akanikuta huko. Sitasahau Migebuka na mawesse. Tulikuwa tunakata magogo ya kuni kuchoma chokaa kwa jembe likitumika kama panga. Operation Miaka 30 ya Uhuru tulijenga nyumba za askari mwaka huo hadi Makame Rashid akafurahi Tukapunguziwa muda wa kukaa JKT. Ni mengi ila umenikumbusha Mbali Ubalikiwe. wasiopitia jeshi wana hasara. tuwape pole!
 

Dunia na Embakasi, haya mashamba ni makubwa balaa.
 
Ila pamoja na mikwala yote hiyo ya JKT nilistahimili kwani nilikuwa nimetoka Chuo Cha maafisa wa jeshi nimeiva yaani NYAKATO SEC. Bukoba hii nayo ilikuwa zaidi ya Jeshi, Koma ya msosi, Karakana kila siku usiku, kujificha Nyamushongoma, Mchakamchaka hadi Nyanga we acha tu. Waliosoma nyakato enzi hizo wanalijua hilo na wengi walioingia jeshi walikuwa maafisa ndio maana naiita Nyakato chuo cha maafisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…