Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

[FONT="Century
Gothic"]Hapo nitapenda kuwakumbusha wale tuliokuwa wote pale Mafinga JKT Kombania F chini ya OC Rweikaza na yule afande invisible aliye julikana kwa jina la Master Follow-up. Tutamkumbuka afande kijana aliyeitwa Mwakyosi. Nakumbuka siku moja tuliamshwa saa kumi alfajiri kama ilivyokuwa kawaida kukata mifagio wakati tukielekea huko porini kukata mifagio kwa mchaka mchaka tuliambiwa twende tukiimba, nikaanzisha wimbo "...Siasa yetu hapana mbaya. Isipokuwa maafande ndiyo wabaya..." Jamaa kusikia mistari ile akaamuru wote kuchuchumaa chini na kuruka kichura chura.

Upande wa Afande Master Follow-up au Afande Mlimbila ambaye sasa ni marehemu, nakumbuka siku moja alimuuliza kuruta mmoja kwamba alipataje kovu lililo katika paja karibu na nyonga. Tamko lile lilizua kilio kwa binti yule na binti alikwenda moja kwa moja kwa CO T N Mlay kutoa taarifa kuhusu mauza uza aliyoyaona usiku ambapo alisema alikuwa akiota kuna mtu amevinjari naye usiku kucha na iweje afande atamke kuhusu kovu wakati ni kweli analo na alijuaje wakati hajawahi kuwa naye kwa makubaliano.

Kifo cha Master Follow-up: Siku hiyo kulikuwa na mkutano mkuu wa wakuu wa vikosi Ma-CO nchini wakati huo Mlimbila alipangiwa kulinda kituo kidogo cha JKT kilichoitwa Sao Hill ambako kulikuwa na mradi wa kuchoma mkaa. Jamaa akakaimu kazi hii kwa mtu mwingine yeye akabaki kikosini. Pale kikosini kulikuwa na afande mmoja Mngoni aliyekuwa na mkewe dogo dogo aliyeishi karibu kabisa na apartment au hanga la Mlimbila. Na afande huyu Mngoni alipangiwa kulinda geti dogo karibu kabisa na nyumbani kwake na inaelekea alishapata fununu za mtoto (Mkewe) kuvinjari na Mlimbila. Muda wa saa mbili usiku bwaloni kukiwa na dance la kumalizika kwa mkutano afande Mngoni akaaga kwenda nyumani kwake "kukagu". Inasemekana alifika akagonga mlangoni bila kufunguliwa, kisha akaenda kuchungulia dirishani na kumuona Mlimbila akiwa ameketi kitandani akiwa mtupu na mke wake afande Mngoni. Alilenga SMG kupitia upenyo wa dirisha na kumkuta Mlimbila katikati ya paji la uso kuona vile binti alikimblia sebuleni na kufungua mlango na kukimbia. Mngoni aliingia na kuuchakaza mwili kila sehemu kwa risasi. Alibakiwa na risasi kama tisa tu. Mwili wake ulipelekwa Mafinga Hospital kujazwa pamba ili angalau uso wake uweze kutambulika. Haya ndiyo nayakumbuka sana ninawakumbuka kuruta wenzangu akina Tarama Mamkwe, Ndubula Msaki, Rachel Mapande, na wengineo.[/FONT]
Nakumbuka mashamba ya Idetelo, detach ya mifugo,kina afande Kingu, john's corner, c ya matron, smart area...
Mi nilikuwa intake ya miaka 20 ya azimio la Arusha.
Tukipewa hotuba siku ya kugawiwa combania,
Nikiwa A-coy.
Hapa tutakufundisha kula mboga ya aina moja kwa mwaka; kushindia kikombe kimoja cha chai.
Nakumbuka tukiwa kitengo cha kupasua kuni jinsi tulivyoweza kuchoma bisi bila moshi kuonekana, na kila mmoja alikuwa na uwezo wa kula mahindi manane ya bisi kwa siku.
Nilimalizia Mlalakua makao makuu ya JKT, enzi za marehemu colonel Msonge aliyekuwa CPNS.
 
Taarifa yako hapo yawezekana ni kweli kwasababu huko huko Ruvu JKT kulikuwa na afande mmoja aliyekuwa katoka JKT Mafinga akiwa na cheo cha Staff Sgt jina lake Afande Stuke. Huyu afande alikuwa na sauti kali sana akitoa amri mfano pale JKT Mafinga sauti yake ilisikika hadi Mafinga Seminari kiasi cha kilometa kama tano au sita hivi. Kutokana na umahili huu alihamishiwa JKT Ruvu. Na kama kawaida wakaona huyu Afande apandishwe cheo kuwa Afisa Mteule Daraja la Kwanza. Ndipo hapo wivu wa wenzake ulipojitokeza. Inasemekana siku moja akiwa tayari na cheo chake alikuwa akikagua mahanga toka A Coy hadi mwisho sijui ni Coy gani pale Ruvu ni ya mwisho. Inasemekana alipotokea mlango wa pili ikawa moja kwa moja hadi msituni na baada ya hapo moja kwa moja kwenye magofu ya kaole akafichwa huko. Order ya kutoweka kwake ikatoka, kisha wakaona kimya Jeshi likaanza kumtafuta bila mafanikio. Baada ya miezi kama sita hivi ndugu zake wakahangaika wakapata taarifa kwamba wakienda magofu ya kaole watamkuta afande Stuke. Wakapewa dawa wakaenda na bila ajizi wakamkuta Afande Stuke akiwa kakonda ile mbaya. Walimchukua hadi Tanga kwa mganga wao akatibiwa na kuhamishiwa kambi ya Maramba Tanga ama Mgambo JKT sina uhakika ni kambi ipi alihamishiwa kwa usalama wake. Uchawi upo sana huko majeshini. Hata huyo Malela wangekazana ndugu zake wanaweza kumuona.
Tukiwa na ujenzi wa ghala la kijiji eneo la Kitelewasi,mvua ilikuwa inanyesha kuzunguka eneo la kazi ilhali sehemu ya kazi ikibaki kavu.
 
Duh mwenzenu siku za mwanzo nusu nife njaa chakula cha moto maharage yana wadudu sijamaliza tonge mbili filimbi
 
Duh mwenzenu siku za mwanzo nusu nife njaa chakula cha moto maharage yana wadudu sijamaliza tonge mbili filimbi

Hiyo kwa siku za kwanza mbona ni kawaida! Mestin ya moto, haragwe lina wadudu, umenyoa para dume jike hajulikani wote kuruta tu. Kwanza kuruta sio mtu hatakiwi kusaidiwa, weee! Haya endeleeni na mambo ya huko!
 
Duh mwenzenu siku za mwanzo nusu nife njaa chakula cha moto maharage yana wadudu sijamaliza tonge mbili filimbi

Hiyo kwa siku za kwanza mbona ni kawaida! Mestin ya moto, haragwe lina wadudu, umenyoa para dume jike hajulikani wote kuruta tu. Kwanza kuruta sio mtu hatakiwi kusaidiwa, weee! Haya endeleeni na mambo ya huko!
We ndo yule foxy? Ukiacha hilo jina la kwanza?
 
Tumo mozambique tumo, maputo tisa tisa moja bila ya buti tumo mozambique tumo!
Aisee!
 
Mama jeni! Mama jeni, we mama jeni.
Nyimbo zenu hizo na ile ya
Iddi Amin akifa, mie siwezi kulia, nitamtupa kageqa, awe chakula cha mamba!
Lol. Hapo wote weusi kudadadeki dume ,jike hajulikani.
 
Oh sorry ni majina tu yamefanana na ni jina langu la kweli simjui huyo ulonitajia
Hiyo kwa siku za kwanza mbohmona ni kawaida! Mestin ya moto, haragwe lina wadudu, umenyoa para dume jike hajulikani wote kuruta tu. Kwanza kuruta sio mtu hatakiwi kusaidiwa, weee! Haya endeleeni na mambo ya huko!
We ndo yule foxy? Ukiacha hilo jina la kwanza?
 
Nimekumbuka mbali wakuu! Op. Vyama Vingi- 91/92; Kikosi 836KJ, OLJORO JKT, MAKUYUNI subdetach Arusha, Force No XXXX. Mashamba makubwa ya Mahindi Oljoro, Dunia na Embakasi. Sehemu ya kujongo: korongoni.
 
Tupo ! TN Mlay, C.O, Basi bwana kuna mshikaji kwenye grup yetu alikua anapiga mkuu wa kombani C Coy, (Captain) sasa siri ikavuja na akatafutwa mtoa huduma ! Grup likatafutiwa visa (tulikuwa 4) mie by the time nilikua 'AWOL' (nimetoroka!) washikaji wakanitaja mimi ! We acha tuu ! Nilirudi kumepoa lakini nilitolewa katika tangazo (nimesahau jina la yale matangazo ya kijeshi) siku naripoti nikakuta bogi la mlalakuwa nikaunga ! Wanashtuka niko Dar !
Matangazo yalitolewa kama ORDER
 
Hii kweli imeamusha hisia zangu mwanzo mwisho. Wale wa Hanga La Mawe Butuku, 822 KJ Operasheni vyama vingi, 1993 mpaka 1994. Hebu tuwasiliane wakuu. Maana nikimkumbuka Afande Mazole, Chale,mashenene, WII Chacha,Luteni Richonjo ........................................................orodha ni ndefu CO Akiwa Colnel Ng'umbi. Wajeshi Bwana anaitisha kikao anawambia Kuruta hastahili kuonewa. Akitoka hapo anawa anaitisha kikao cha wakufunzi wakitoka huko moto mtauona bwana. WOII Chacha alikuwa naweza kuamurisha kikosi kizima mkurya yule bwana we acha tu...................... Siku yangu imekumbuka mbali hadi raha
 
Wengine tulikosa jeshi kwasababu ya sheria kuwa ilishafutwa lakini hapo Same Secondary napo ilikuwa kama jeshi tu.
Wengi sana tunatamani hy nafasi ila mfumo mgeuzo ndio umetutesa...Lakini mazingira 2liyopitia JKT tosha...Wale waliosoma Pomerini Sekondari(Iringa) ilikuwa ni JKT namba 2 baada ya Mafinga.
 
Nimekumbuka mbali wakuu! Op. Vyama Vingi- 91/92; Kikosi 836KJ, OLJORO JKT, MAKUYUNI subdetach Arusha, Force No XXXX. Mashamba makubwa ya Mahindi Oljoro, Dunia na Embakasi. Sehemu ya kujongo: korongoni.
Cha ajabu number yangu ya sim naweza isahau lakini si force number, mpaka leo naikumbuka !
 
Nilianzia Masange Tabora Danger COY ya Wella na Busongo, Busongo akisema wewe kama Ni form six yeye ni form seven, Degree normal vidato nothing, Tall water. Nikakatwa Bog kwenda Bulombora nikijua nimemkwepa Wella huko nikamkuta affande Chacha na JD aliyemtengua kiuno kuruta akafukuzwa jeshi. Baadae Wella akahamishiwa Bulombora akanikuta huko. Sitasahau Migebuka na mawesse. Tulikuwa tunakata magogo ya kuni kuchoma chokaa kwa jembe likitumika kama panga. Operation Miaka 30 ya Uhuru tulijenga nyumba za askari mwaka huo hadi Makame Rashid akafurahi Tukapunguziwa muda wa kukaa JKT. Ni mengi ila umenikumbusha Mbali Ubalikiwe. wasiopitia jeshi wana hasara. tuwape pole!
 
Luteni kanali wengi walikuwa CEO kama sikosei walikuwa hawa deal sana na makuruta....unamuona kwa nadra sana......

Baada ya chakula cha usiku nakumbuka oljoro watu walikuwa wanasimamisha minazi kinoma mitaa ya mgahawa kule duh!....Miye nilikuwa mtoro siku kaa sana olrojo nikaja kuhamia Mgulani kwa Kitomari!....na huko ilikuwa shushushu tuu!....Ila ilikuwa fun kusema kweli...pale oljoro kulikuwa na shamba linaitwa Dunia hujui mwanzo wake wala mwisho.....mtu unapewa mraba ulime umalize by lunch time..maselule wengi tulikuwa tunabakia kule hadi lunch ya "mchana" unakosa....

Dunia na Embakasi, haya mashamba ni makubwa balaa.
 
Ila pamoja na mikwala yote hiyo ya JKT nilistahimili kwani nilikuwa nimetoka Chuo Cha maafisa wa jeshi nimeiva yaani NYAKATO SEC. Bukoba hii nayo ilikuwa zaidi ya Jeshi, Koma ya msosi, Karakana kila siku usiku, kujificha Nyamushongoma, Mchakamchaka hadi Nyanga we acha tu. Waliosoma nyakato enzi hizo wanalijua hilo na wengi walioingia jeshi walikuwa maafisa ndio maana naiita Nyakato chuo cha maafisa.
 
Back
Top Bottom