Ally Kombo
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 11,429
- 2,650
Siku ya kwanza kuripoti, tukakuta skendo ya mauaji ! Kuna Sajenti taji, anakula wake za wenziwe kwa kitisho cha uchawi ! Mpaka C O anamuogopa ! Siku moja kaingia kwa jamaa ambae alikua lindo, jamaa alipopata taarifa akamzukia. Basi aligonga mlango afunguliwe, wakati wanajishauri jamaa akakimbilia dirishani, akiwa anamuona vizuri kutokea dirishani.......,..,...akampa 7 ! Kiuno kikajigawaMatangazo yalitolewa kama ORDER
Mama jeni! Mama jeni, we mama jeni.
Nyimbo zenu hizo na ile ya
Iddi Amin akifa, mie siwezi kulia, nitamtupa kageqa, awe chakula cha mamba!
Lol. Hapo wote weusi kudadadeki dume ,jike hajulikani.
Nakumbuka mashamba ya Idetelo, detach ya mifugo,kina afande Kingu, john's corner, c ya matron, smart area...
Mi nilikuwa intake ya miaka 20 ya azimio la Arusha.
Tukipewa hotuba siku ya kugawiwa combania,
Nikiwa A-coy.
Hapa tutakufundisha kula mboga ya aina moja kwa mwaka; kushindia kikombe kimoja cha chai.
Nakumbuka tukiwa kitengo cha kupasua kuni jinsi tulivyoweza kuchoma bisi bila moshi kuonekana, na kila mmoja alikuwa na uwezo wa kula mahindi manane ya bisi kwa siku.
Nilimalizia Mlalakua makao makuu ya JKT, enzi za marehemu colonel Msonge aliyekuwa CPNS.
Ila pamoja na mikwala yote hiyo ya JKT nilistahimili kwani nilikuwa nimetoka Chuo Cha maafisa wa jeshi nimeiva yaani NYAKATO SEC. Bukoba hii nayo ilikuwa zaidi ya Jeshi, Koma ya msosi, Karakana kila siku usiku, kujificha Nyamushongoma, Mchakamchaka hadi Nyanga we acha tu. Waliosoma nyakato enzi hizo wanalijua hilo na wengi walioingia jeshi walikuwa maafisa ndio maana naiita Nyakato chuo cha maafisa.
Nimekumbuka mbali wakuu! Op. Vyama Vingi- 91/92; Kikosi 836KJ, OLJORO JKT, MAKUYUNI subdetach Arusha, Force No XXXX. Mashamba makubwa ya Mahindi Oljoro, Dunia na Embakasi. Sehemu ya kujongo: korongoni.
Sir Major wenu alikuwa nani? Mwaka 1990/91 alikua afande Sanga. Jamaa alikua poa sana.Kwa wale waliokuwa RUVU JKT OPERATION OLJORO mwaka 1994 naomba tukumbukane.Mimi binafsi nilikuwa FCOY.Kilichonifurahisha nikiwa RUVU JKT.
.DISCO-mtu unaimba wimbo wowote hata kwa lugha ya kwenu.
.Kwa babu
.Kusimamisha minazi.
Sanctus,
Mimi niliamua kukwepa kwenda Tabora na kuamua kwenda Oljoro kwasababu nilikuwa na kakangu mjini Arusha. Nikajua nikitoroka nitakuwa na sehemu kwa kubugia ugali.
Basi kufika Oljoro, tukamkuta afande Dauda, (sijui kama linaandikwa hivyo) alikuwa ndio mkuu wa mafunzo. Akasema mwaka jana alitoa kibali cha kuua kruta watano, akasema aligundua haikutosha, anawaamrisha maafande mwaka huu kuua kruta mpaka 15.
Kesho yake watu kibao wakatoroka na kwenda ku report kambi zingine. Isingelikuwa kuwa na brother hapo mjini na mimi ningelirudi kule Tabora usiku huo. Baada ya muda tukaja gundua kumbe Dauda ndiye alikuwa afande poa kuliko wengine wote.
Tulikuwa na afande mmoja Mhehe alikuwa anaitwa Mduda. Alikuwa anajifanya anajua jeshi kweli kweli. Akaopoa mtoto wa maana sana. Siku moja tumemaliza jeshi tuko mlimani, akaingia mlimani hall D na magwanda, kaja kufuata mtoto wake. Maskini yule msichana alikuwa terrified, akajificha. Jamaa akasubiri pale wee, mpaka akaamua kujikata. Alifikiri yale ya jeshini yanaendelea uraiani. Tulimsanifu kweli siku hiyo.
Looh! ni miaka karibu 20 toka wengine tuondoke JKT lakini naona michapo yake inakuja tu. Waswahili tungelikuwa tunaandika vitabu, tuna mengi ya kusimulia.
Mkuu unakumbuka embakasi...Namkumbuka afande sijali??afande masabila,Kuna afande kafupi kalikuwa sijui kanaitwa nani kalikuwa kajamaa ka Dom kabila linaloongea kwa kusonya!! Sikonge..It was so fun guys!!Mie nilianzia Msange JKT na kumalizia hapo - OPERATION program ya chama. Tulikuwa na Afande Mohamed, Mrope, Odo, Mandevu, Matron Gwimo, Magege, na wengine kibao ila majina yashaanza kunitoka. Hii ilikuwa mwaka 1989/90.
Leo ntaweka kituko kimoja tu kutoka kwa jamaa mmoja aliyekuwa akienda kwa jina la Ukunu au Pepo. Huyu Matron Gwimo alikuwa na tabia ya kuja na kuingia bweni la wavulana na kuamsha bila ya kutoa warning. Hiki kitendo kilituudhi sana na siku ya mkutano watu wakapania kumsemea. Wengi wakawa wanalalamika ila wanaogopa kumtaja Matron huyo ni yupi. Ukunu alisimama na kusema Matron huyo ni Gwimo. Hapo niliona sura za Ma-afande zikianza kuwa nyekundu kwa hasira na nikajua kuwa wakitoka hapo watauwa mtu. Jamaa akaendelea ".. huyu afande alishasababisha mgomo kumbaini B watu wakakataa kula. Huyu alifanya ..... na afande unajua kuwa sisi wanaume tukilala, asubuhi tunapoamka huwa tunakuwa na MIGOGORO........" Lohhh, watu walicheka hadi wakalala na mkutano ukawa umefia hapohapo maana hata afande mwenyewe machozi yalikuwa yakitoka kwa kucheka. Mkutano ulifungwa na Sajenti Manyilizu na luteni Mohamed alijikaza kwa shida kupigiwa saluti. Alipovua tu kofia akaangua tena kicheko.
Ikawa kila siku wasichana wakimuona asubuhi wanamuuliza ".. kaka Manara, vipi leo mgogoro ulikuwaje?". Ila maajabu yalikuwa kuona wanawake na wanaume wakioga UCHI katika umbali wa mita kama 5 hivi. Na unapatwa na mshangao unapochota maji, vilikuwepo vi-plastic sijui vilikuwa vya nini, basi watu wakawa wanatekea maji kisimani. Sasa anakuja dada na kusema "..... na mimi naomba hicho kikondom cha tembo nichotee maji......" Kweli wanawake wakimaliza JKT huwaambii kitu. Tofauti yao na wanaume tuseme ukweli haipo.
Mkuu unakumbuka embakasi...Namkumbuka afande sijali??afande masabila,Kuna afande kafupi kalikuwa sijui kanaitwa nani kalikuwa kajamaa ka Dom kabila linaloongea kwa kusonya!! Sikonge..It was so fun guys!!
Kajamaa kalikuwa kashortii hivi sijui alikuwa anaitwa nani???hivi nitamkumbuka...Afande wera..dah!!!Niliamka usiku kwenda kufagia msituni shida aina adabu..leo hii hawa mabishoo wanaosoma hizi shule za fm academia wataweza???Kubeba mtulinga wa maji kutoka shamba la mdarasi hadi jikoni???Dah..nimekumbuka nilikuwa nikijipendekeza officers mess kula ubwabwa!!nilikiwa na kishtobe wangu kule basi mimi nagongelea misosi ya officers mess!!!Sijali namkumbuka kwa mbaali sasa. Huyu jamaa alikuwa B au D-Coy kama sikosei.
Mie nilikuwa A-Coy na Afende Moddy na Boss wake Mwiru. Enzi hizo kulikuwa na Odo, na MKurya mmoja mwenye Korokoro Mkononi. Daah, majina wengi nimeanza kuwasahau.
Huyu afande wa Dodoma, simkumbuki. Ila enzi zetu wasumbufu walikuwa Afande Wera? (sijui nimepatia, Muha wa Kigoma), Afande Magwega (sijui jina lake lilikuwa nani?), alikuwepo mtu anaitwa NGOMA, alikuwa akitesa sana watu.
Enzi hizo kweli UBONGO ulisimama kufanya kazi.
Kajamaa kalikuwa kashortii hivi sijui alikuwa anaitwa nani???hivi nitamkumbuka...Afande wera..dah!!!Niliamka usiku kwenda kufagia msituni shida aina adabu..leo hii hawa mabishoo wanaosoma hizi shule za fm academia wataweza???Kubeba mtulinga wa maji kutoka shamba la mdarasi hadi jikoni???Dah..nimekumbuka nilikuwa nikijipendekeza officers mess kula ubwabwa!!nilikiwa na kishtobe wangu kule basi mimi nagongelea misosi ya officers mess!!!